Nakungojea

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,335
Reaction score
23,951
Nakungojea...



​

Ngoja niombe kalamu, nitume zangu salamu,
kwa mtoto wa Kilamu, uzuri we ka tunda damu,
mwingine simfahamu, yeye tu anipa hamu,
kwake naziba fahamu, anipavyo nafahamu!

Wangu wa moyo kipenzi, uzurio nauenzi,
si kwamba hauna wenzi, ndo maana natunga tenzi,
wajapo wengi wakwezi, si wote wataka nazi,
wakileta upuuzi, watimue waziwazi!

Najua fimbo ya mbali, kamwe haina makali,
na sisi tulivyo mbali, penzi usilibadili,
nipende kwa kila hali, siku moja tule wali,
na nyama yake fahali, matunda ya kujijali!

Pendo la kweli hungoja, vumilia bila hoja,
hushinda vyote vioja, vya wale waso na tija,
kimbia wanapokuja, kasema dada mahija,
upendo ni namba moja, vingine vyajikongoja!

Si mwingi muda nadhani, utakuja wewe hani,
na siri iwe hewani, waelezwe na wageni,
"walopendana kifani, leo wako harusini,
waliitunza imani, sasa wamo furahani!"



Wasalaam wapendwa,
PM Moderator, Mentor.


"At the touch of love, everyone becomes a poet." - Plato
​
 
Pole kwa yako hamu, Nimepokea zako salamu
Shairi lako hakika ni tamu, na mie limenikata hamu
Maisha huku bado magumu, japo tunatoka kwa zamu
Mentor kaa huko huko mjini huku usirudi

Mie bado vile vile mzuri, Uzuri angu wamesha ukariri
Naomba nisikufiche hii siri, Maana wambea hawatonisitiri
Mwenzio nimekuchoka sio siri,wala sizitaki zako habari
Mentor kaa huko huko mjini huku usirudi

Nimelipata langu jibababa, Mapesa na mali limeshiba
Nalichuna kwa zangu nasaba, Kiganjani nimeliweka si haba
Mapesa lanimwagia bila uhaba, Nashukuru si haba nashiba
Manetor kaa huko huko mjini huku usirudi

Sikupenda kufanya haya, Msamaha nakuomba bila haya
Langu kabila muhaya, umasikini kwetu watia haya
Ukinisamehe si vibaya ukishidwa sitokufikira vibaya
Manetor kaa huko huko mjini huku usirudi

Mentor Pema ukishapema si tena pema
Siwezi kufa maskini kwa wema, japo nakuombea mema
siwezi tena kwako kuwa mwema , japo nitaukumbuka wako wema
Manetor kaa huko huko mjini huku usirudi
 

What the Hell!???????????????????????? Did this just come off your head...Nimeshindwa kuhuzunika maana ukipigwa kibuti kwa tungo murua kama hizi walahi huwezi kujihisi maumivu ya moyo!
lara 1 u got some talent in this hun...ila duh, hadi kwenye shairi bado unawaza pesa! we noma..

Cc: Mtambuzi, Nicas Mtei, Vin Diesel, Asprin, KakaKiiza - nahisi kuna libazazi limoja kati yenu limeniibia hiki kifaa changu.

Wapendwa: mwallu, miss neddy, Munkari, miss chagga, sister, Sista, King'asti, charming lady, Elizabeth Dominic, badiebey - namtafuta mrembo wa kumghania tungo hizi!!!!

Wenu PM Moderator, Mentor.
 
Last edited by a moderator:
Hivi PM Moderator anatukagua katika pm site zetu??ngoja niulize kwa Invisible yani Mentor ndo hawe ananikagua leo nimempm nani tukikutana awe annicheka PM nafunga now labda nijibiwe vingine huyu mwenyewe ni #Teambazazi
 
Last edited by a moderator:
He he he, mapenzi ya mbali yafaa vibogoyo tu. Hizi sindano zinazoshona hadi makoti haziwezi.

Hapana Kongosho, katika maisha ya kawaida ni lazima mtafikia kipindi mtakuwa mbali kwa muda. Je ndiyo mwisho wa mahusiano yenu?

Mtunzi wa shairi yamemkuta..anahitaji kutiwa moyo kuwa uvumilivu kidogo watajikuta wakila wali na nyama ya fahali, kwani..utabadili wangapi kwa kisingizio cha umbali Kongosho!??

Hivi PM Moderator anatukagua katika pm site zetu??ngoja niulize kwa Invisible yani Mentor ndo hawe ananikagua leo nimempm nani tukikutana awe annicheka PM nafunga now labda nijibiwe vingine huyu mwenyewe ni #Teambazazi

Bazazi ni wewe mwenyewe... Cc: Paloma

BTW, I know my ethics za kazi...la sivyo juzi ningekuwa nakucheka sana maana nimeona PM zako nyingi sana kwa wadada wewe #bazazi .

Aisee.... ntarejea.

Usikawie babu...


Wenu PM moderator, Mentor.
 
Last edited by a moderator:
matamu ukimpata, sifongo mkirushana. Na kuombea dua, muishi mmeshikana.
 


Hahahaaaaa!!!!!!!!! What do you mean i have got talent? DONT BE SO DRAMATIC!!!!!!! Talented walikuwa kina Shaaban Robert, Mloka (Diwani ya Mloka), Malenga Wapya, Kina mza Akhmed alikuwa ana ghai zaidi kuliko kufanya original ushairi pale RTD late 1990's. Those people arethe best! Japo kazi zao ni 30yrs to 50 yrs old ila ni TIMELESS! I liked shaaban robert na nimemsoma sanaa japo my all time favorite was DIWANI YA MLOKA!

The sister is learned Mentor! Chezea O- LEVEL major in LITERATURE!!!!!!!!!!! Mambo ya ze shairi in kingreza! Weeeeeeee!

Calling me talented i cheating before the masses! Shairi mizani imekongoroka, beti zinaning'inia, vina kushney babu j, uzani marehemu siku nyingi! Wakikusikia wenye fani yao huko mbele za haki watarudi ghafla!

Na vijana sio kuhinda kwenye TELEMUNDO, na DSTV all time, siku moja moja exploit your HISTORY and honor your ANCESTORS! Read African Literature. Chinua Achebe was the best for me.
 
Nice one,kip it up hehehehe aliyetungiwa mbona ana balaa
 
Mhmmm wewe ungejua wewe ungeisha sema!

Ili mradi usiwe mwoga.
Inamaana hata wewe babu utakuwa unakaguliwa na Mentor???
 
Last edited by a moderator:
He he he, maisha yenewe yako wapi ya kujibana?

Mkiwa mbali teknikale mmekubaliana mechi za mchangani, ila mwenye hati miliki anakuwa huyo ulomchagua. Ukiikubali hii basi mpenz ya mbali yanafaa.

Hata hivyo, kuna ile unamwambia mtu, ukimpiga chura teke umempunguzia mwendo - sosi King'asti
Kabla hajaenda unamdediketi huu wimbo



 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…