Nakumbuka Mitihani yetu ya Darasa la Saba ilikuwa inaanza ivi

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
*Nakumbuka mitihani ya Darasa la saba ilikuwa inaanza kama utani utani hivi*

19+87=
219-45=
12x34=
59÷7=

Halafu huko mbele sasa kuanzia swali la sita au la saba hivi...utajutaa!!

"Ndege inatoka Dar saa tatu asbh kwenda Chato. Na gari Toyota Land cruiser linatoka Chato saa nne asbh kwenda Dar.

Ikiwa spidi ya ndege ni 350km/saa na ya land cruiser ni km220/Saa, na umbali wa Chato-Dar ni KM 900, je, zitakutana saa ngapi?"

Ah, sasa mi ntajuaje???
Na hizi tochi zote barabarani na matuta na ishu ya kusimama kujisaidia...ntawezaje kujua watakutana saa ngapi.

Unajikuta umetoka kwenye pepa umejibu maswali manne tu ya mwanzo kati ya hamsini
 
Hahahahaa umenikumbusha mbaaaali sana, unasoma swali mara sita na bado hulielewi unasoma lingine yaleyale uwiiii
Hapo huja chungulia kwa jamaa yako wa pembeni unakuta naye hooolaa!!! Mnabaki mnatambuliana mimacho.

Hahaha Somo la hisabati ni ugonjwa wa Taifa likiwa sambamba na Somo la Kiingereza.
 
Hapo unafanya x ndio muda gari litakaotumia kukutana

gari litakuwa limesafiri kilomta 220x
ndege itauwa imesafisafiri kilomita 350(x+1), hiyo ni 1 sababu ya ndege iliwahi saa moja kabla ya gari

Kupata x ambayo ndio muda unatakiwa uzi equate hizo mbili, kwa kuwa jumla ya km ni 900, kilomita ilizosafiri gari lilipokutana na ndege itakuwa ni sawa na 900 utoe km ilizosafiri ndege

220x= 900-350(x+1)
Ukikokotoa utapata x ni 30/19 ya saa
ukitaka kuhakiki unatafuta kilomita ilizosafiri ndege baada ya 30/19 ya lisaa kisha unatafuta na km ilizosafiri gari baada ya 30/19 ya saa, hizo km za gari na ndege ukizijumlisha lazima zilete jibu la 900 kwa kuwa km zote zilikuwa covered.

Darasa la saba kulikuwa hakuna maswali magumu kama hayo, huo ni ukilaza wako unashindwa kutofautisha hata maswali ya la saba na sekondari
 
*Nakumbuka mitihani ya Darasa la saba ilikuwa inaanza kama utani utani hivi*

19+87=
219-45=
12x34=
59÷7=

Halafu huko mbele sasa kuanzia swali la sita au la saba hivi...utajutaa!!

"Ndege inatoka Dar saa tatu asbh kwenda Chato. Na gari Toyota Land cruiser linatoka Chato saa nne asbh kwenda Dar.

Ikiwa spidi ya ndege ni 350km/saa na ya land cruiser ni km220/Saa, na umbali wa Chato-Dar ni KM 900, je, zitakutana saa ngapi?"

Ah, sasa mi ntajuaje???
Na hizi tochi zote barabarani na matuta na ishu ya kusimama kujisaidia...ntawezaje kujua watakutana saa ngapi.

Unajikuta umetoka kwenye pepa umejibu maswali manne tu ya mwanzo kati ya hamsini
mkuu kama vile tulimaliza mwaka mmoja hahahahhaha, hali ikishakuwa ngumu hivi unaomba mungu kama mwalimu wako atapita angalau aweke kidole mahali, hapohapo unaweka kama jibu! wale jamaa askari polisi walikuwa wanakomaa ile mbaya hakuna mtu kuzengea eneo mnalofanyia paper
 
Tumvumilie (chinchilla) huyo kasoma drs la7 la math za multiple choice 2013>na kuendelea. Au ndo wale wa Feza schools ada milion 45
 
Darasa la saba kulikuwa hakuna maswali magumu kama hayo, huo ni ukilaza wako unashindwa kutofautisha hata maswali ya la saba na sekondari
Unaonekana wewe ni mtoto wa juzi , miaka ya 90+ kulikuwa na maswali zaid ya hilo darasa la saba. Unadhan ni awamu ya vilaza ile ambayo mnapewa maswali ya hesabu ya kuchagua?
 
sijafanya hesabu za multiple choice na hata ningefanya bado maswali ya miaka ya nyuma ipo kwenye vitabu vya necta vilivyokuwa vinatoka, hivyo haijalishi mtu kujua maswali ya la saba miaka hata ya 70s achilia mbali hiyo 90s yako yalikuaje,

na narudia tena kama unaamini hilo swali ni la darasa la saba wewe ni kilaza wa hesabu, hilo swali najua solution yake na mtoto wa la saba hawezi kupewa swali kama hilo
 
Tumvumilie (chinchilla) huyo kasoma drs la7 la math za multiple choice 2013>na kuendelea. Au ndo wale wa Feza schools ada milion 45
wewe ni kilaza wa hesabu, kwa mtu anayejua solution ya hilo swali anajua kabisa hilo sio swali la shule ya msingi, ulikuwa huelewi hata maswali ya maelezo inaonekana
 
sijafanya hesabu za multiple choice na hata ningefanya bado maswali ya miaka ya nyuma ipo kwenye vitabu vya necta vilivyokuwa vinatoka, hivyo haijalishi mtu kujua maswali ya la saba miaka hata ya 70s achilia mbali hiyo 90s yako yalikuaje,

na narudia tena kama unaamini hilo swali ni la darasa la saba wewe ni kilaza wa hesabu, hilo swali najua solution yake na mtoto wa la saba hawezi kupewa swali kama hilo

I'm not seeking forgiveness

Nakumbuka ya treni na masaa 24 ndio yalikua yanaletwa, ile masaa yanaandikwa 1900 au 2145. Mara nyingi ilikua kutafuta muda wa treni au basi kufika mahali na namna ya kuziandika hizo saa. Hesabu zingine zilikua za ankara na zile za kutafuta gharama ya kutuma maneno sijui kwa fax? (sina uhakika) unapewa gharama ya maneno kumi ya mwanzo na kila neno linalozidi kusha utafute gharama za kutuma maneno uliyopewa.
 
wewe ni kilaza wa hesabu, kwa mtu anayejua solution ya hilo swali anajua kabisa hilo sio swali la shule ya msingi, ulikuwa huelewi hata maswali ya maelezo inaonekana

I'm not seeking forgiveness
Hapo mtoa mada hajazungumzia hayo maswali manne ya kwanza yeye kazungumzia ugumu wa maswali ya mafumbo kwa nilivyomuelewa mimi
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Hapo mtoa mada hajazungumzia hayo maswali manne ya kwanza yeye kazungumzia ugumu wa maswali ya mafumbo kwa nilivyomuelewa mimi
nimemuelewa ila hilo swali la fumbo sio la darasa la saba, ni la sekondari, nasema hivyo sababu najua solution yake na sio ya la saba
 
sijafanya hesabu za multiple choice na hata ningefanya bado maswali ya miaka ya nyuma ipo kwenye vitabu vya necta vilivyokuwa vinatoka, hivyo haijalishi mtu kujua maswali ya la saba miaka hata ya 70s achilia mbali hiyo 90s yako yalikuaje,

na narudia tena kama unaamini hilo swali ni la darasa la saba wewe ni kilaza wa hesabu, hilo swali najua solution yake na mtoto wa la saba hawezi kupewa swali kama hilo

I'm not seeking forgiveness

Review za darasa la 7 zimeanza kutoka 2010, je wewe ndio ulikua darasa la 7?
 
Back
Top Bottom