Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
MwanaJF mwenzetu barafu ni kati ya weledi, werevu, wajenga hoja wazuri na wabobezi mbalimbali waliosheheni humu. Kufuatia uwepo Wa taarifa za 'kugongwa' kwa ndege yetu ya Dreamliner, Mkuu barafu anayeaminika kubobea katika masuala ya ndege aliibuka na kuweka mambo sawa.
Mkuu barafu ,pamoja na mambo mengine ameeleza wazi kuwa katika masuala ya ndege na usafirishaji kwa njia ya anga kwa ujumla, masuala hayo yaliyoripotiwa ni ya kawaida. Matengenezo hata ya injini Si mambo ya kushangaza, kwa mujibu wake. Hakika, maelezo ya Mkuu barafu yanashibisha na kuelimisha Sana.
Katika mada hiyo, Mkuu barafu alidokeza tatizo linaloendelea kukomaa katika Tanzania yetu. Tatizo linalotikana na watu kugawanyika kwa misimamo yao badala ya hoja na uhalisia. Wapo wanapinga kila jambo lifanywalo na Serikali. Wapo wanaounga mkono kila jambo lifanywalo na Serikali.
Wapingaji na waunga mkono hao Wa kila jambo hawafuatilii wala kuzingatia hoja zilizopo au hali halisi iliyopo na kuzungumza Kama watanzania. Wanachojua ni kupinga au kuunga mkono tu. Wana upofu Wa vyama na kuchochewa na itikadi zao tu.
Wapingaji na waunga mkono hao Wa kila jambo huparurana kwa matusi, kejeli na dhihaka badala ya kushindana kwa hoja na kukubaliana kukubaliana au kutokukubaliana kwa hoja na hali halisi. Hakika, makundi haya yanayoshamiri kwenye jamii ni tatizo. Yanapanda chuki na kuleta mgawanyiko. Ni ya kukemewa na kuachwa.
Kupinga au kuunga mkono kila jambo la Serikali bila hoja au hali halisi Si jambo jema. Kama taifa lenye wasomi Wa kutosha tunapaswa kujadili kwa staha na kutetea au kupinga kwa hoja. Si kujiweka kwenye nafasi ya kutetea au kupinga kila jambo.
Tanzania ni nchi yetu, Serikali ni yetu.