Nakubaliana na Mkuu Barafu Wa JF, Kama Taifa tuna tatizo linakomaa. Tufanye nini kujinasua?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,176
25,446
MwanaJF mwenzetu barafu ni kati ya weledi, werevu, wajenga hoja wazuri na wabobezi mbalimbali waliosheheni humu. Kufuatia uwepo Wa taarifa za 'kugongwa' kwa ndege yetu ya Dreamliner, Mkuu barafu anayeaminika kubobea katika masuala ya ndege aliibuka na kuweka mambo sawa.

Mkuu barafu ,pamoja na mambo mengine ameeleza wazi kuwa katika masuala ya ndege na usafirishaji kwa njia ya anga kwa ujumla, masuala hayo yaliyoripotiwa ni ya kawaida. Matengenezo hata ya injini Si mambo ya kushangaza, kwa mujibu wake. Hakika, maelezo ya Mkuu barafu yanashibisha na kuelimisha Sana.

Katika mada hiyo, Mkuu barafu alidokeza tatizo linaloendelea kukomaa katika Tanzania yetu. Tatizo linalotikana na watu kugawanyika kwa misimamo yao badala ya hoja na uhalisia. Wapo wanapinga kila jambo lifanywalo na Serikali. Wapo wanaounga mkono kila jambo lifanywalo na Serikali.

Wapingaji na waunga mkono hao Wa kila jambo hawafuatilii wala kuzingatia hoja zilizopo au hali halisi iliyopo na kuzungumza Kama watanzania. Wanachojua ni kupinga au kuunga mkono tu. Wana upofu Wa vyama na kuchochewa na itikadi zao tu.

Wapingaji na waunga mkono hao Wa kila jambo huparurana kwa matusi, kejeli na dhihaka badala ya kushindana kwa hoja na kukubaliana kukubaliana au kutokukubaliana kwa hoja na hali halisi. Hakika, makundi haya yanayoshamiri kwenye jamii ni tatizo. Yanapanda chuki na kuleta mgawanyiko. Ni ya kukemewa na kuachwa.

Kupinga au kuunga mkono kila jambo la Serikali bila hoja au hali halisi Si jambo jema. Kama taifa lenye wasomi Wa kutosha tunapaswa kujadili kwa staha na kutetea au kupinga kwa hoja. Si kujiweka kwenye nafasi ya kutetea au kupinga kila jambo.

Tanzania ni nchi yetu, Serikali ni yetu.
 
Sasa hii umeileta ya nini?
Si unge comment huko kwenye hiyo thread?
Au unapenda ganda la ndizi
 
solution ni moja tu msajili wa vyama vya siasa avifute Chadema, ACT na CUF. hivi ndio vyama vinavyoeneza chuki kwa jamii

Hata akifuta hivyo vyama bado huwezi kufuta mitazamo yao. Watu wameshatoka kwenye dunia ya ukondoo. Tena sio kuvifuta tu, ikibidi ccm wafanye mauaji ya halaiki kuwaua wapenzi na wanachama wa hivyo vyama, bado watatokea wengi tu kupinga dhuluma. Tatizo la chuki nchi hii limeletwa na ccm na kukaziwa na jiwe kwa kutumia madaraka yake fullstop.
 
solution ni moja tu msajili wa vyama vya siasa avifute Chadema, ACT na CUF. hivi ndio vyama vinavyoeneza chuki kwa jamii
Unadhani vyama hivyo vya siasa, kwa akili uliyojaliwa na Mungu wako, ndivyo vinaleta mgawanyiko uliobainishwa? Umekurupuka kuandika kwa mapenzi yaleyale ya chama chako, au umechuja na kuelewa hoja? Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisoma vizuri hilo bandiko neno Barafu limerudiwa mara 5, kipindi tupo shule tulikua tukiaswa juu ya kutorudia jina au uandishi maana utamchosha msomaji
Yote tisa , kumi naona upo sahihi hii nchi ni yetu sote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom