Nakubaliana na Mkuu Barafu Wa JF, Kama Taifa tuna tatizo linakomaa. Tufanye nini kujinasua?

Ukisoma vizuri hilo bandiko neno Barafu limerudiwa mara 5, kipindi tupo shule tulikua tukiaswa juu ya kutorudia jina au uandishi maana utamchosha msomaji
Yote tisa , kumi naona upo sahihi hii nchi ni yetu sote

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo lipo hapo hii nchi sio yetu wote Sisi wengine ni wakuja wenye nayo nafikiri unawajua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye hakuwa na mada hii kama mada take kuu. Soma uelewe
Nimeilewa, inafaa kuwa comment ktk uzi wake. 100% umemsifia na kukubaliana na hoja yake. Na kuna copy and paste za kutosha za hoja zake kwenye hoja yako. Kilichoongezeka ni kuhitajia maoni ya nini kifanyike. So kupunguza repetition na kujaza Threads. Ni vyema ikawa comment ktk uzi mkuu. Tuta quote na kupendekeza cha kufanya huko.

With all due respect

Sent from my SHV-E330K using Tapatalk
 
Nimeilewa, inafaa kuwa comment ktk uzi wake. 100% umemsifia na kukubaliana na hoja yake. Na kuna copy and paste za kutosha za hoja zake kwenye hoja yako. Kilichoongezeka ni kuhitajia maoni ya nini kifanyike. So kupunguza repetition na kujaza Threads. Ni vyema ikawa comment ktk uzi mkuu. Tuta quote na kupendekeza cha kufanya huko.

With all due respect

Sent from my SHV-E330K using Tapatalk
Hakuna copy and paste hata mstari mmoja
 
Hebu tuingie ndani kidogo na kujiuliza.
Mfano kuna ununuzi wa ndege unafanywa kwa pesa za kodi ambazo zinapatikana kutoka kwa watanzania wote bila itikadi. Sasa serikali inapokea ndege kwa sherehe za kiccm huku TOT wakiimba nyimbo za kejeli kwa wapinzani wa ccm kama kwamba waligoma kutozwa kodi hivyo wajionee ccm walivyokusanya kodi yao kununua ndege. Wanasimama viongozi mbalimbali wanakuja na vijembe vya kufa mtu kwa watu wote wasio ccm na kila mtu anashangilia.
Mie nawaambia acha kugongwa tuu, hizo ndege moja ikiungua moto ndio mtajua kuwa huwezi kumkebehi mtu na kitu halafu akakipenda, huyo atakuwa mnafiki kabisa. Na wapinzani sio wanafiki wanataka nao msikie maumivu yale waliyo sikia kwenye kebehi.
Hata watoto ndani ya nyumba kama hutaki kuwaweka pamoja na unawagawa kwa makundi subiri nyumba ikiungua utaona wengine wakichekelea.
 
Mkuu sio Barafu tuu hata ashuke nani kuelezea au kutetea ubovu wa ndege yetu itabaki kuwa ni mbovu tuu...kunahitaji weledi gani kuelezwa kitu kibovu ili kionekane kizima.
 
Hata akifuta hivyo vyama bado huwezi kufuta mitazamo yao. Watu wameshatoka kwenye dunia ya ukondoo. Tena sio kuvifuta tu, ikibidi ccm wafanye mauaji ya halaiki kuwaua wapenzi na wanachama wa hivyo vyama, bado watatokea wengi tu kupinga dhuluma. Tatizo la chuki nchi hii limeletwa na ccm na kukaziwa na jiwe kwa kutumia madaraka yake fullstop.
Nimeshangaa sana mkuu Petro E. Mselewa ame like kilicho andikwa na huyu jamaa yako? Nimeshangaa sana, hivi Msomi kama Petro nae anakubali kwamba wapinzani ndio wameleta chuki nchi hi na sio ccm? Nimeudharau hadi na UZI wenyewe, kama kuna kitu ambacho sisiem wanatakiwa kujisifia sana kwa kukifanya na kimefanikiwa sana, basi ni kuwafanya Watanzania kuongea mambo wasio yaamini, yaani wanafiki. UOVU mkubwa na mengi mazuri yaliofanyika nchi hi, ccm haiwezi kuyakwepa, hata hili la mgawanyiko wa Watanzania by now, is them who did it but hadi "wasomi" nao wanasingizia wengine. Balaa kubwa
 
Hata akifuta hivyo vyama bado huwezi kufuta mitazamo yao. Watu wameshatoka kwenye dunia ya ukondoo. Tena sio kuvifuta tu, ikibidi ccm wafanye mauaji ya halaiki kuwaua wapenzi na wanachama wa hivyo vyama, bado watatokea wengi tu kupinga dhuluma. Tatizo la chuki nchi hii limeletwa na ccm na kukaziwa na jiwe kwa kutumia madaraka yake fullstop.
Chuki ni zao la ubinafsi..baadhi ya makabila na watu wa maeneo fulani ni wabinafsi, mtu mbinafsi hata atendewe wema wa kiwango gani hawezi kuridhika na matunda ya ubinafsi ni wivu na chuki dhidi ya watu wengine.
 
MwanaJF mwenzetu barafu ni kati ya weledi, werevu, wajenga hoja wazuri na wabobezi mbalimbali waliosheheni humu. Kufuatia uwepo Wa taarifa za 'kugongwa' kwa ndege yetu ya Dreamliner, Mkuu barafu anayeaminika kubobea katika masuala ya ndege aliibuka na kuweka mambo sawa.

Mkuu barafu ,pamoja na mambo mengine ameeleza wazi kuwa katika masuala ya ndege na usafirishaji kwa njia ya anga kwa ujumla, masuala hayo yaliyoripotiwa ni ya kawaida. Matengenezo hata ya injini Si mambo ya kushangaza, kwa mujibu wake. Hakika, maelezo ya Mkuu barafu yanashibisha na kuelimisha Sana.

Katika mada hiyo, Mkuu barafu alidokeza tatizo linaloendelea kukomaa katika Tanzania yetu. Tatizo linalotikana na watu kugawanyika kwa misimamo yao badala ya hoja na uhalisia. Wapo wanapinga kila jambo lifanywalo na Serikali. Wapo wanaounga mkono kila jambo lifanywalo na Serikali.

Wapingaji na waunga mkono hao Wa kila jambo hawafuatilii wala kuzingatia hoja zilizopo au hali halisi iliyopo na kuzungumza Kama watanzania. Wanachojua ni kupinga au kuunga mkono tu. Wana upofu Wa vyama na kuchochewa na itikadi zao tu.

Wapingaji na waunga mkono hao Wa kila jambo huparurana kwa matusi, kejeli na dhihaka badala ya kushindana kwa hoja na kukubaliana kukubaliana au kutokukubaliana kwa hoja na hali halisi. Hakika, makundi haya yanayoshamiri kwenye jamii ni tatizo. Yanapanda chuki na kuleta mgawanyiko. Ni ya kukemewa na kuachwa.

Kupinga au kuunga mkono kila jambo la Serikali bila hoja au hali halisi Si jambo jema. Kama taifa lenye wasomi Wa kutosha tunapaswa kujadili kwa staha na kutetea au kupinga kwa hoja. Si kujiweka kwenye nafasi ya kutetea au kupinga kila jambo.

Tanzania ni nchi yetu, Serikali ni yetu.

Waasisi wa chuki katika taifa hili wanjuliƙana, lawama ziende kwao.
 
Back
Top Bottom