Nakushauri kabla ya kukopa popote tafiti kwanza riba na namna ya malipo yakoje. Kuna asasi nyingi zinarubuni wananchi. Utasikia wanasema ukienda bank riba asilimia 18. Ila kwetu sisi riba ni asilimia tatu kwa mwezi. Unaweza kuona ndio nzuri kumbe maana yake ni 36% kwa mwaka.Habari wapendwa, nimesikia kuna uwezekano wa kupata mkopo online kutoka kwa Tanzania Vision Fund. Je, kuna mwenye ufahamu na jambo hilo na inakuwaje?
Hebu fanya kama ndio unaelezea ni kina nani hawa, wanatoa huduma zipi, kwa wenye sifa zipi n.kMkuu haukopi online, Mimi ni mteja wa Vision Fund; Wana huduma kama uko mbali na mjini/ Mbali na bank basi unaweza kupata mkopo wao kwa njia ya simu, Mpesa/Airtel money, wametuambia na Tigopesa nao wanajiunga mwezi wa nane; pia unaweza kufanya marejeshio kwa njia ya Simu. Hicho ndio ninachokijua mkuu
Mwenye mpya atujuze.