Mwandishi nguli wa kujitegemea Idris Sebuleni ameandika katika ukurasa wake wa Twitter (x) maneno haya. Namnukuu"
"Nimesoma ripoti yote ya CAG, Taarifa za LAAC, PAC na PIC hakuna mahali Mwigulu ametajwa kuhusika na wizi wa hata thumuni.
Hakuna sehemu hata moja imetaja ameshiriki kusababisha hasara ya hata senti moja.
Facts zimeongea, Propaganda dhidi yake zimeshindwa kwa mara nyingine" Mwisho wa kumnukuu.
MAONI YANGU MIMI KUHUSU HIKI ALICHOANDIKA MKONGWE HUYU;
Ni kweli Mwigulu Nchemba hajatajwa kokote kuhusika na wizi yeye kama mtu binafsi, lakini wizara yake imetajwa japokuwa kipindi tukio hili la upigaji linafanyika yeye hakuwa waziri wa fedha, bali mtangulizi wake.
Nilitegemea Mwigulu Nchemba amtaje mhusika wa hilo tukio bungeni lakini aliufyata, na hilo ndo linamfanya aonekane anahusika kumbe angaweza kumtaja mhusika na mambo yakaisha.
Alamski.