ahsante mkuu kweli ukalimu umeniponza mimi.Pole sana Kaka. Mimi sioni kama kuna shida hapo...mtoto kazaliwa salama na mama wa mtoto salama.
Itabidi uanze taratibu za kisheria hapo kuhakiki wazazi kamili wa huyo mtoto. Itawagharimu kidogo ila utasafisha jina lako na kurudisha heshima kwa wahusika wote.
Ukarimu umekuponza pole sana.
Huna haja ya kumfuata, wewe tafuta mwanasheria anayehusika na matatizo ya familia atakusaidia na DNA sio lazima ihusishe wazazi wote...unaweza kufanya wewe na huyo mtoto tu.mkuu nitaanza vipi kumfuata kumweliza hilo?
Basi utakua na matatizo mkuu.mkuu huyo mlemavo ndo mchumba wa huyo dada nimejua hilo baada ya kuelezwa na shemeji yangu.
Karibu. Kwa sasa jaribu kufuata ushauri wa wazee wenye busara wanaokuzunguka (ndugu, Marafiki, majirani). Ukikwama kabisa ndio uangalie upande wa Sheria na nina uhakika wapo watakao pitia hii post na kukuelekeza mahali husika pa kwenda...usikose usingizi kwani dhamira yako ni safi.ahsante mkuu kweli ukalimu umeniponza mimi.
sasa huu utaratibu wa kisheria nitafanya vipi mkuu mana mimi mambo hayo ndo siyajui kabisa.
Hauna sababu ya kufeel guilt when you are not! Be a man and stand for the truth...unaweza kwenda mbali zaidi na kufanya vipimo vya DNA. Ingawaje siamini sana kama hukuhusika kwa lolote.Habari wanajamii, poleni kwa majukumu ya kutwa nzima ya leo.
Jamani naombeni mnisaidie nini cha kufanya nana roho inaniuma sana kwa jambo hili.
Kuna ndugu yangu naishi nae mtaa mmoja ila yeye ameo na ana watoto wawili. Mara nyingi huwa nakwenda kwake nahasa shemeji yeye huwa anata niende kula chakula kwake pindi ninapotoka kazini kwa kuwa mimi bado sijaoa so ananionea huruma kujipikia mwenyewe.
Sasa pale kwa huyu ndugu yangu kuna mpangaji ambaye anawatoto wawili mmoja ni binti mkuwa wa miaka 21 na mwingine ana miaka 13 kiujumla maisha yao si mazuri kila kitu wanamtegemea mama yao. huyu binti mdogo anasoma form one pamoja na mtoto wa ndugu yangu. hawa watoto wamenizoea sana . Nikajikuta namhurumia sana huyu mtoto wa jirani wakati mwingine anakosa hata vifaa vya shule kutokana na hali yao ya kimaisha basi nikaamua kumnunulia baadhi ya vitu pia na hata pesa za tution namlipia mimi.Mama yake pamoja na dada yake wakanishukuru sana.
Sasa ikawa kila siku dadayake akaanza kuwa karibu na mimi na hatimaye tukawa marafiki wakubwa tu hadi kwangu akawa anakuja kilichokuwa kikimleta ni CD huwa anapenda sana kuangalia seasons kama mimi so anakuja kuchukuaga kwangu.Ila hatukuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi hata siku moja Mungu wangu ni shahidi.
Kumbe huyu dada alitolewa mahari na bwana mmoja hapa mtaani mimi sikufahamu hilo na wala yeye hakunambia. Mara nikamuona huyu dada akiwa mjamzito sikuhoji kitu na sikuwa na sababu ya kuhoji kwa hilo.
Kumbe likawa kosa kubwa sana mchumba wake akawa analalamika kuwa mimi natembea na mchumba wake mimi sikuwa na habari kwasababu mimi si mkaaji wa vijiweni mimi nikiingia nimeingia nikitoka nimetoka ukibahatika basi utanikuta kwa shemeji yangu so story za mitaani zikawa zinanipita.
Imefika wakati huyu dada kajifungua tena kwa oparetion. na siku chache kabla ya kujifungua alikuja kwangu tuliongea sana kama kawaida yetu.
Kilichotokea jamaa kamkataa mtoto anadai sio wake ni wangu mimi na hii leo ni siku ya 6 tangu ajifungue jamaa hajaenda kumuona mwanae. dada wa watu analia anaomba nimsaidie kumwambia ukweli huyo jamaa. Shemeji ndo amenambia kila kitu kuhusu huyu jamaa.
Kinacho niuma zaidi mtu mwenyewe ni mlemavu masikini naumia sana moyoni sikutembea nae mimi hata mara moja jamini.
Nitafanya nini ili niaminike wakati watu walikuwa wanamuona akija nyumbani kwangu??.
NITAELEZA NINI MIMI WAPENDWA. NAJIONA MKOSAJI HASA MTU MWENYEWE KILEMA NITAANZIA WAPI KUMWAMBIA UKWELI .
NISAIDIENI MAWAZO YENU NDUGU ZANGU NIMEKWAMA HAPA.
Kama una uhakika hukutembea nae, cha kwanza mfwate face to face huyo jamaa (hapa mvizie akiwakwenye mood nzuri na akiwa free) mwambie hali halisi!!! akikataa mchukue shem wako na mzee/ wazee wenye heshima hapo mtaani, akikataa mnaweza kuonana na viongozi wa dini!!! na hapa akikataa mwambie mkapime DNA!!! na hii akigoma basi jua jamaa alikua natafuta gear ya kukimbia mimba na kashaipata hapo!!!!
Kwakua umeonyesha nia ya kuwasaidia incase akikataa basi wakihitaji msaada wape (ila hapa uwe makini maana wanaweza sema ndio unalea mwanao)!!!