Nakionea huruma Chama Cha Mapinduzi

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
By Malisa GJ,

Huu ujinga wa kutafuta U-DC kwa kujipendekeza utafikisha CCM kwenye mauti. Vijana wa Lumumba wamejifungia ndani wakasajili ki-NGO chao "uchwara" katika harakati za kusaka ukuu wa wilaya wamekuja na kiripoti hiki cha kijinga. Eti wamefanya utafiti wakapata list ya Wanaume 20 wa kitanzania wenye nguvu na ushawishi zaidi kwa mwaka huu (The most Powerful &Influential Men in Tanzania 2016).

KASORO ZA UTAFITI.

Nimesoma utafiti huu kwa haraka haraka mimeona kasoro kama 100 hivi ndani ya dakika chache za kusoma. Lakini kwa ajili ya muda nitaeleza kasoro mbili tu maana nikieleza zote nitamaliza mwakani.

#Kasoro_nambaMoja
Utafiti wowote duniani ni "retrospective" ndio maana unaitwa Research. Maana yake ni kwamba kitu kinatokea kwanza ndio unatafiti. Huwezi kutafiti kitu ambacho bado hakijatokea. Ili upate list ya watu wenye ushawishi kwa mwaka 2016 inabidi ufanye utafiti mwaka 2017. Yani ikishafika mwaka 2017 ndio unatafiti nani alikua na ushawishi mwaka 2016 kwa kutumia vigezo mbalimbali.

Huwezi kufanya utafiti wa watu wenye ushawishi kwa mwaka huu, wakati mwaka ndio kwanza uko mwanzoni. Umejuaje huyo mwenye ushawishi leo kama atapoteza ushawishi wake mwezi ujao? Au atafariki miezi miwili ijayo? Au kufika October atakua amefanya tukio litakalopoteza ushawishi wake kwa jamii?

Kwa hiyo ningewaelewa hawa vijana wa CCM kama wangesema hii ni list ya watu wenye ushawishi kwa mwaka jana (2015) lakini sio 2016. Huu ni utaratibu wa kitaaluma duniani pote. Ndio maana hata Tuzo za waandishi wa habari zilizotolewa juzi na MCT ni za waandishi bora kwa mwaka 2015 sio za 2016. Waandishi bora wa 2016 watapewa tuzo zao 2017.

Huwezi kutoa orodha ya kupima ufanisi au uwezo wa kitu ndani ya mwaka wakati mwaka huo haujafika mwisho. Kwa mfano MCT wangekuwa "machizi" kama wangetoa tuzo za waandishi bora kwa mwaka 2016 wakati mwaka bado haujaisha. Wangeulizwa wamejuaje kama mwezi ujao kuna waandishi watafanya vizuri zaidi ya hao waliowapa tuzo?

Kwahiyo utafiti wowote duniani ni "Retrospective" sio "retroactive". Huwezi kutafiti kitu ambacho hakijatokea. Ukianza kutafiti mambo ya baadae huo sio UTAFITI ni RAMLI. Kwa hiyo vijana hawa wa CCM wamejikuta wanapiga ramli ktk juhudi zao za kusaka UDC. Poor them.

Hivi walishindwa hata kuuliza kwa wasomi waliopo CCM angalau wawashauri. CCM ina wasomi wengi tu tena wenye weledi mkubwa, wana Researchers wanaohesbimika duniani. Ndani ya CCM kuna maprofesa na PhD wengi tu, mbona hawajawasaidia hawa vijana ili wasioneshe upumbavu wao hadharani?

Yani kitu kidogo tu kimewahiribia. Wameonekana wazi kuwa wamepika data. Babu yangu aliwahi kuniambia "If you want to cheat me make sure u are too smart upstairs than me".. Yani ukitakua kunidanganya hakikisha una akili nyingi sana kuzidi mimi. Vinginevyo nitakugundua na itakuwa kilio kwako.

Sasa hawa vijana wa CCM ni waongo lakini imeshindwa kuwa smart. Ni sawa na enzi zile za utoto unaiba sukari nyumbani halafu ukiulizwa unabisha wakati mashavu yote yamejaa sukari. Vijana wenzangu wa CCM acheni uzwazwa.

Hapa mmechemsha. Hii rioti ni fake. Na kwny jopo la hawa "wasaka UDC" yupo mmoja alifanya Press majuzi akimtukana ZZK kuwa hayuko smart ndio maana anataka kumhujumu JPM. Sasa baada ya ripoti hii sijui nani smart kati ya ZZK na huyu msaka UDC.

#Kasoro_nambaMbili
Vigezo vilivyotumika kutangangaza hii orodha ni irrelative and inverse to their findings. Vigezo vya kukubalika na jamii, kuheshimika, kujitoa kwenye maafa, kujali jamii, kushiriki shughuli za kijamii, kufahamika (umaarufu), kufanya matukio makubwa yaliyoacha alama chanya kwa jamii etc.

Hizi criteria ni inverse to their findings kwa sababu SI KWELI kwamba Mohamed Shein anakubalika na Jamii kuliko Diamond Platnamz. Hata tukisema tupige kura sasa hivi, nina uhakika Diamond akiwa anahesabu kura ya 1,000 Shein atakua hajafikisha kura 6. Lakini eti Shein ni wa 11 na Diamond ni wa 18. Acheni utoto vijana wenzangu.

Pili mnasema kutoa msaada kwa jamii. Hivi Mzee Warioba anatoa msaada kwa Jamii kuliko Mzee Mengi? Mengi ametoa misaada mingi sana direct ya kifedha kwa watu wengi na kwa mamilioni ya shilingi. Pia ana makampuni na viwanda ambavyo vimeajiri maelfu ya watanzania. Kwa kufanya hivyo anatoa msaada mkubwa sana kwa jamii achilia mbali CSR anazofanya kila mwaka za kusaidia walemavu. Sasa mzee Warioba katusaidia nini hadi amshinde Mengi kwenye rank? Kumnadi Magufuli wakati wa kampeni au? Acheni uzwazwa vijana wenzangu.

Kigezo kingine mmesema kufahamika. Sasa niwaulize, Hivi Peter Noni anafahamika kuliko Millard Ayo? U cant be serious aisee. Tupige kura hapa ili tuprove? Millard Ayo ni namba nyingine, anafahamika hadi na watoto walioko tumboni nyie mnasema anazidiwa na Peter Noni?

Nina uhakika nikiuliza watu 10 kama wanamjua Peter Noni, 9 kati yao watauliza "Ndio nani?" (Kwa sauti ya Joti). Simaanishi kwamba Peter Noni sio maarufu, namaanisha hajamzidi Millard Ayo kwa umaarufu. Labda huko baadae.

Au Mbwana Samatta anazidiwaje umaarifu na Makonda kwa mfano??. Hahahaa acheni utani. Wakati Samatta anauzwa milioni 150 kwenda TP Mazembe, Makonda alikua akisoma chuo cha Ushirika Moshi akivuta bumu ya 7,500/= kwa siku kutoka Bodi.

However Mbwana anafahamika Congo, Rwanda, Ulaya na Afrika kwa ujumla. Amekuwa hadi mchezaji bora wa Afrika (kwa ligi za ndani) leo mnasema anazidiwa umaarufu na Makonda? Acheni utani. Makonda umaarufu wake unaishia Bunju A, maana akisogea Bagamoyo anamkuta mkuu wa mkoa mwingine. Sasa mnamfananisha na Samatta ambaye ni maarufu hadi Ulaya.

Vijana kajipangeni upya. Huu ni utafiti wa hovyo kuwahi kufanyika duniani tangu kumalizika kwa vita vya Maumau. Nitamshangaa sana JPM akiwapa UDC kwa kukurupuka namna hii. Hivi mmetumia ubongo kupika hii Research au mmetumia mafuvu?? Hivyo vichwa mnavibeba tu kama matenga ya kubebea nyanya badala ya kuvitumia kufikiri.

Sasa naanza kuelewa kwanini Comrade Rashid Chilumba anasisitiza sana matumizi ya maziwa ya mama kwa mtoto hasa kipindi cha miezi 6 baada ya kuzaliwa. Si bure nyie mlinyonya ya ng'ombe. Poor you. Poor Research. Poor CCM. Poor Magufuli if u gona appoint these Poor Empty minded youth from your party.

Kama hizi ndio akili za vijana wa CCM basi nakionea huruma sana chama hiki kikongwe. Vijana ktk chama chochote cha siasa wanapaswa kuwa "Think Tank" ya chama. Sasa kama hii ndio "Think Tank" ya CCM aisee hiki chama kiko ICU. Kitakufa muda wowote kuanzia sasa kwa shinikizo la damu au kifua kikuu.

R.I.P CCM.!
 
nimegundua kitu kimoja ukiwa CCM hata uwe umesoma vipi lakini elimu yako haiwezi ikaonekana kwasababu unakuwa upo gizani.

CCM kuna wasomi wengi sana lakini walishindwa kuwashauri swala dogo kama hilo.
 
Kijana utafiti hupingwa utafiti,ni vema sasa TADIP chini ya Shumbusho iandae propaganda.
 
Katika maisha yangu ya miaka 30 sijawahi kumsikia Warioba akitoa misaada popote. Sijui labda huo anatoa kwenye chama chetu. Halafu huyo Peter Noni si yule mwizi wa EPA vile? Sina uhakika kwa hilo.

Vijana wa CCM si wa kulaumiwa, kwasababu vijana wote walio na vyeo vikubwa katika Serikali yetu kwa awamu zote huo wanafanya propaganda ndio wanapata vyeo.

Unafikiri bila ya Makonda kumpiga mzee Warioba na kufuta viatu vya Rz1 angepata UDC hatimaye URC?

Unafikiri bila ya Polepole kuwadanganya watanzania kuwa misaada ya MCC haina hadhari kwa Tanzania angepata UDC kule Musoma?

Unafikiri bila ya vijana wa UVCCM kutoa matamko mbalimbali ya ovyo huyu Katibu wa UVCCM angepata UDC Kinondoni?

Tambua kuwa huo ndio mfumo wa kuishi wa vijana wa CCM bila kufanya hivyo utaishia kuvaa nguo za kijani tu maisha yako yote.
 
Kwakweli hata mimi huyo mtu simjui, ngoja tusubiri msaada wa kuelekezwa hapa.
Noni ni mmoja wa wala matunda ya uhuru kwenye jamhuri ya Tanganyika. Kifupi, ana pesa ndefu kwahiyo usishangae kuona Vijana wa CCM wanampa hilo flag... wana CCM kwa ujumla wake wana mahaba ya dhati na wenye fedha!!

Wakati ule ambapo kesi za EPA zikiunguruma pale Kisutu Noni alikuwa ni mmoja wa mashahidi wa upande wa Mashitaka! It didn't happen by chance but alikuwa ni mmoja wa vigogo wa pale BoT aliyekuwa na ukaribu na Daudi Balali!

Jambo ambalo halieleweki ni namna gani basi nae hakuwa japo mmoja wa watuhumiwa wakati idara yake ndo hasa ilihusika na EPA... anyway, no offense!!

Mwenye kingi uongezewa kwahiyo forget about why hakuwemo kwenye EPA manake for what I know the guy is the current boss wa Tanzania Investment Bank kwa miaka kadhaa sasa tangu enzi nami nikiwa banker!

Nilitaka kusahau! Unakumbuka ile scandal ya wajanja wa Vodacom kupiga mabilioni hata kama sina uhakika ikiwa ni kweli? Labda nikukumbushe tu kwamba moja ya kampuni ambazo zilituhumiwa ni Planetel! Hii kampuni nayo ni ya Peter Noni huku nae akiwa ni mmoja wa Vodacom Shareholders!

Lakini sitamtendea haki nisipokiri pasi na shaka yoyote kwamba that old man is very smart and hard working. Kwa yeyote anayemfahamu pia analifahamu hili! Lakini kwamba eti nae ni among Top 20 Influential Figure is total exaggeration!!
 
NAKUMBUKA ilipitishwa sheria ya kupata baraka za NBS kabla ya kutoa taarifa za kitakwimu.Je. hawa wana baraka hizo?
 
Kijana utafiti hupingwa utafiti,ni vema sasa TADIP chini ya Shumbusho iandae propaganda.
Mkuu najua kutetea jambo unaloliamini ni haki kabisa ila ukweli waweza kuuona kuhusu mada hii. Mfano, Mimi namjua Peter Noni kwa muda mrefu na mambo yake mengi ila baada ya kusoma hili nimefanya kautafiti kidogo. Nimeita Vijana wangu wawili wanaonisaidia hapa kwenye ujasiria Mali wangu kuwauliza wanamfahamu mtu mashuhuri mwenye Nina la Peter Noni?
Wakwaza wa like ambaye ana elimu ya cheti na ana umri mkubwa kidogo akanijibu hajawahi kulisikia jina hilo hata mtaani kwake.

Huyu wa kiume ambaye elimu yake ni ngazi ya diploma, lakini namtegemea sana kwani ni "mtoto wa mjini' anajua mengi ndiye kanichekesha, kasema Peter Noni hawezi kuwa maarufu popote lands umaarufu wa kunywa pombe nikashangaa. Kumbe yeye anayemjua kwa jina hilo ni mjomba ake aliye kijijini.
Hiyo tafiti ya Vijana wa CCM imesaidia tuu kwa wale wanaofanya tafiti juu ya kwa nini CCM inapoteza hadhi?
 
Vijana wa CCM wamechoka kuuza tshirts na kofia za chama pale Lumumba. Waacheni sasa watafute U-DC kwa namna ambayo wao wanaona inafaa.
 
Back
Top Bottom