mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,729
Hodi humu ndani!.....
Mwenzenu nimetafakari sana juu ya hali ya hewa nchini, na matukio yooote ambayo yametokea nyakati hizi.
Binafsi kama Wapinzani wamehisi kuonewa kwenye uchaguzi na ushahidi wooote wanao,mpaka Leo nilitegenea kuona wakija pamoja vyama vyote na kutoa msimamo wao.
Pia na kuelezea wananchi mustakabali na maamuzi yaliyofikiwa, matokeo yake wanakimbili Instagram, Facebook na tweeter kulalamika bila kujua ni watanzania wachache sn ndio wapo huko mitandaoni.
HAWA WATU WAPO WAPI.?
1. Edward Lowassa
2. Frederick Sumaye
3. Prof. Lipumba.
4. Mbatia
5 Hashim Lungwe Sipunda
6. Maalim seif
7. Juma Duni
NB: NAWAZA KUJIUNGA CCM NA KITAMBI CHANGU.....
" If you can not defeat them,join them" yaani
"Kama huwezi kuwashinda ungana nao"
Hotuba ya Mbowe iliyosababisha mauti, ndiyo ya mwisho kwa viongozi wakuu uliowataja kujitokeza hadharani. Maneno aliyoyatamka na kuhamasisha wafuasi wake, wote wakiwa vijana, dizaini ya wabwia unga, ilishangiliwa na kuwaingiza vijana mitaani, kwa kile kinachodaiwa na Mbowe kushinikiza kudai haki yao.
Sidhani mtu mwenye akili timamu angefurahia maneno aliyotamka Mbowe na kusema yalikuwa sahihi.
Upinzani wa aina hiyo ni wa KITOTO Haswa