Najuta kuwa na Akaunti CRDB

Najuta kuwa na Akaunti CRDB

Ndikwega

R I P
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,979
Reaction score
5,529
Hii Benki imekuwa na usumbufu wa hovyo kabisa.
Kwanza Mtandao wao muda ambapo upo Off ni mwingi kuliko unapokuwa ON. Yaani asubuhi hii nimetembelea ATM machines zao katika maeneo mawili tofauti kote hazifanyi kazi yaani ilipo Benki yenyewe hamna, na hili ni mfululizo tu wa kutopatikana kwa huduma zao na si kwamba bahati Mbaya maana ni kitu ambacho kimeota mizizi, imejirudia mara nyingi mno mpaka kero.

Na wakati mwingine ukiingia ndani ya benki ili uhudumiwe watumishi wao wana nyodo sana. Majibu mabovu pia wanawahudumia vizuri wawajuao tu.

CRDB ni Benki ya hovyo kwasasa hata kuizidi NMB. Mapema sana nitajiondoa kwenye huduma zao wasipojirekesha.

Najua mpo humu, UJUMBE umewafikia.
 
Wamekusikia mkuu na pole sana maana naelewa inavyokuwa unapokosa huduma ili kutatua mahitaji yako. Aisee na mie nina bank na crdb hizi tuhuma nyingi i'm seeing nakuwa shocked.
 
Una shilingi ngapi kwenye account? Usije letea wenzio inzi wakati una hela ya kuruhusu risiti ya muamala kutoka tu...
 
Sim banking isiwe kigezo cha kutuhaminisha kwamba crdb hawastahili kutoa huduma bora na kuweka hela kwenye atms, the fact hapa ni huduma mbovu ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wateja. Sio wote wana sim banking, 2. What if ur out of service yani upo eneo ambalo mtandao husika unasumbua au kukosa chaji kwenye simu! Sim banking ni alternative ila sio kwamba watu wasiende tena atms la hasha. Hata hiyo sim banking ambayo hata mimi naitumia kuna wakati iko slow sana kama leo kwa Nzega Tabora. Mtoa mada pia amelalamikia huduma na majibu ya kejeli yanayotolewa na wahudumu wa bank husika.
 
Khaa!!Usiweke mayai yote kwenye kikapu kimoja:A S-baby:
 
CRDB nimeshawahi kupata tatizo la PIN nikaenda customer care nikaambiwa itakuwa ok mbali na kuwaambia kuwa nina safari ya nje ya nchi walisistiza iko poa kufika Bondeni ikawa tabu tupu Card haifanyi kazi tatizo PIN nikatuma email na kupiga simu kadhaa bila mafanikio yaani najuuta kuwafahamu.
 
Hii Benki imekuwa na usumbufu wa hovyo kabisa.
Kwanza Mtandao wao muda ambapo upo Off ni mwingi kuliko unapokuwa ON. Yaani asubuhi hii nimetembelea ATM machines zao katika maeneo mawili tofauti kote hazifanyi kazi yaani ilipo Benki yenyewe hamna, na hili ni mfululizo tu wa kutopatikana kwa huduma zao na si kwamba bahati Mbaya maana ni kitu ambacho kimeota mizizi, imejirudia mara nyingi mno mpaka kero.

Na wakati mwingine ukiingia ndani ya benki ili uhudumiwe watumishi wao wana nyodo sana. Majibu mabovu pia wanawahudumia vizuri wawajuao tu.

CRDB ni Benki ya hovyo kwasasa hata kuizidi NMB. Mapema sana nitajiondoa kwenye huduma zao wasipojirekesha.

Najua mpo humu, UJUMBE umewafikia.

Tatizo lao ajira ki undugu na chupi mbele. Ndo mwanzo wa shida zote hizi.
 
Transfer your money to any other account achana nayo.
 
kama una master card kwa nini usichote hela kweny atm ya bank nyingine yoyote?

Kuna jamaa altoa kwa atm ingne hela haikutoka ila rct ikatoka kuwa hela imetoka,alilinda atm saa nzma asubr ztoke lakn hazkutoka!kaenda crdb wamemuambia mpaka baada ya cku 45 kwel???
 
Mbona mimi sijuti? Acha fitina wewe, nenda huko huko NMB kwenye FOLEN za ATM, naona Unawatangazia Biashara NMB utalipia!
 
Hakuna Benki makini kama hii CRDB. Nashauri ambaye hapati huduma ipasavyo/apendavyo ajikate kiaina. Acha kupiga debe.
 
Una shilingi ngapi kwenye account? Usije letea wenzio inzi wakati una hela ya kuruhusu risiti ya muamala kutoka tu...

We hebu heshimu pesa ya mwenzio hata kama ya kutolea risiti si yake umemtafutia wewe ? Ana haki ya kupata huduma ya benki cha msingi wajirekebishe tu CRDB maana nimesikia kama ni mabinti wengi wanaingizwa kwa rushwa za ngono kama ni wakaka asilimia kubwa wanaingizwa na ndugu zao.Sasa kwa mtindo huo lazima huduma ziwe hovyo tu.
 
like.....
 
karibu TPB bank bank halisi ya kitanzania tunahudumiwa na bank ya kitanzania wenzio
 
Mimi nimeumizwa na charges zao kwa kutununua ticket ya treni: Milan Central to Malpenza Int. Airport! Euro 12 wanachukua pesa nyingi tu.
 
Back
Top Bottom