Haijawahi kutokea CHADEMA wakakubali matokeo ya uchaguzi, haijawahi kutokea. Mwaka huu Lowassa aliwaambia kuwa atalinda kura yeye lakini cha ajabu sasa hivi analalamika wa kwanza. Ukweli ni kwamba Wananchi wameamua kumchagua Magufuli na ameshinda kwa haki kabisa. Hizo fomu zilizosainiwa na mawakala wenu zimetoka wapi???? Acheni kuipeleka nchi hii kwenye vita ninyi. Ukishindwa unakubali tu kushindwa basi maisha yanaendelea. Kama mlikuwa mnasoma posts zangu humu JF nilisema mimi Magufuli atashinda urais halafu CHADEMA watakataa matokeo kwa kisingizio wameibiwa kura. Tatizo lenu mnafikiri watu kujaa kwenye mikutano ya kampeni ndio matokeo ya kura. Niliwaambia mimi hapa hapa JF kama mnakumbuka, nilisema CCM ina mtaji mkubwa sana wa wapiga kura na itashinda. Unajua kwenye kampeni watu wengi wanajaa kutokana na hamasa tu ya kampeni lakini sio kweli kuwa watakupigia kura. Kingine nilichosema mimi ni vijana wengi sana under 18 kujaa kwenye mikutano ya UKAWA. Hawa vijana sio wapiga kura, lakini cha ajabu UKAWA hawakuliona hili, vijana waliokuwa wanajaza hii mikutano wengi wao ni wanywa viroba tu, ni vijana ambao hawakuwa serious katika kupiga kura. Matokeo yake wengi sana hawajapiga kura. Wameandikishwa watu millioni 22 lakini waliopiga kura hawazidi millioni 12, milioni 10 wote hawajapiga kura. Mimi hili nililijua tokea mwanzo kabisa ndio maana nilikuwa naandika kwa kujiamini kabisa kuwa Magufuli atashinda urais. Kingine ni kuondoka kwa Dk Slaa na Prof Ibrahimu Lipumba. Hawa viongozi hawakuondoka peke yao, waliondoka na watu wengi sana, hasa watu makini walikuwa pamoja nao. Amini nawaambia kama hawa viongozi wasingeondoka, leo hii Lowassa angekuwa anasubiri kuapishwa. Wapo mtakaobisha sana lakini huo ndio ukweli wenyewe. Mimi nakuambia hakuna kura iliyoibiwa. Sio rahisi kuiba kura kama mnavyofikiri. Magufuli ameshinda kihalali kabisa. Kitu kingine kilichomuangusha Lowassa ni kuongea kwa dakika mbili, Watanzania wanapenda mtu muongeaji, hawapendi mtu mkimya mkimya.