Najuta kuoa mapema, miaka mitano baada ya ndoa ndio nakutana na mwanamke wa ndoto yangu

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,039
35,922
Ndivyo navyoweza kusema, nilioa miaka mitano iliyopita ila huyu mwanamke ni kiboko niliwahi kutupiwa begi la nguo nje kama Dk Slaa kisa nimerudi saa nne usiku nilichelewa baada ya kutoka kwenye kiako cha harusi ya mshkaji, nami kwa hasira nikaenda kulala kwa wazazi wangu.

Visa vilizidi ikabidi nichukue hamsini zangu,nikiwa na upweke ndio nikakutana na mdada mwenye sifa zote za mke, mrembo sana, msomi, ana adabu na kila sifa nzuri ya mwanamke ikabidi nimfiche kuhusu ndoa yangu, japo nilimwambia kuwa nina mtoto alikuwa tayari.

Ila wiki iliyopita ikabidi nimwambie ukweli kuwa nina ndoa, japo kila mtu anaishi kivyake, dada wa watu kanuna, hataki hata kuniongelesha, najuta kuwahi kuoa huyu ndio alikuwa mke wangu, kwani tulipendana sana na tulimatch vitu vingi sana.

Natamani Yesu arudi afanyie mabadiliko sheria ya ndoa kwa sisi wakristo ili niuoe huyu dada
 
Asante Evelyn. Nakubaliana na wewe. Joto la penzi jipya kama si mstahimilivu unasahau yale ambayo inapaswa usimamie.
kumbuka hapo kati nimeshachepuka sana ila huyu wa mwisho nimemvulia kofia
 
Amini amini nakuambia, baada ya kuachana au kupotezana na huyo utampata mwingine tena ambaye utamuita wa ndoto zako.
natamani kuweka picha yake humu ungeniambia kuwa amini amini kijana ulikuwa na bahati
 
natamani kuweka picha yake humu ungeniambia kuwa amini amini kijana ulikuwa na bahati

Kwahiyo kilichokuvutia zaidi ni umbo la nje?
Basi kama ndio hivo 'utatuoa' wengi tusiotazamika kwa tabia.....(mimi sikuhisi)

Mwanamke tabia kaka.
Maana ulivyosema kuwa utuwekee picha, inasadifu ni jinsi gani 'mkeo' alivyo kisu zaidi ya 'mwenye nyumba'
Hongera.

Kama ni hivi mjini wako wengi sana
 
Hahahaa.. Umenichekesha sana ukatupiwa bag kama nani?? Papa alisharahisisha sheria za talaka kwa wanandoa ila sababu yako hiyo haitawezekana. So rudi ukavumilie umwite na mshenga wenu awasuluishe
 
Kwahiyo kilichokuvutia zaidi ni umbo la nje?
Basi kama ndio hivo 'utatuoa' wengi tusiotazamika kwa tabia.....(mimi sikuhisi)

Mwanamke tabia kaka.
Maana ulivyosema kuwa utuwekee picha, inasadifu ni jinsi gani 'mkeo' alivyo kisu zaidi ya 'mwenye nyumba'
Hongera.

Kama ni hivi mjini wako wengi sana
asikudanganye mtu,mwanamke hata kama anatabia nzuri kiasi gani lakini sura na umbo havina mvuto ni shida usiku unakuwa kama umelala na mwanamme mwenzako
kuna watu wanalalamika kuwa hawana nguvu za kiume kumbe wameoa wanawake hawana mvuto waliangalia tabia peke yake wakipiga moja ndio mpaka wiki ijayo
kuna wanawake wanamvuto huchoki usiku kucha ni gwaride,
 
Naona una udugu na Bikira wa kisukuma.
Anakwambia "utaoaje mwanamke ana shepu kama tangawizi?"
Haya kaka.....

Ukimchoka huyo uliyempata sasa, uje na kwangu kama huangalii tabia ili sasa uweze 'kupata usingizi'
 
Ndivyo navyoweza kusema ,nilioa miaka mitano iliyopita ila huyu mwanamke ni kiboko niliwahi kutupiwa begi la nguo nje kama Dk Slaa kisa nimerudi saa nne usiku nilichelewa baada ya kutoka kwenye kiako cha harusi ya mshkaji,nami kwa hasira nikaenda kulala kwa wazazi wangu.

1. Mwanaume wa ki-Africa hafukuzwi kwake kamwe. Haijalishi umekosea, ama lah.

2. Kwenda kulala kwenu ni udhaifu mwingine mkubwa. Ungetafuta pengine popote pa kulala, ila kwenda home ulitengeneza picha mbaya.
 
Naona una udugu na Bikira wa kisukuma.
Anakwambia "utaoaje mwanamke ana shepu kama tangawizi?"
Haya kaka.....

Ukimchoka huyo uliyempata sasa, uje na kwangu kama huangalii tabia ili sasa uweze 'kupata usingizi'

niliyempata kaishanisusa hanitaki tena anasema mi mume wa mtu,sasa ukinikaribisha kwako nitashukuru sana madame B
 
niliyempata kaishanisusa hanitaki tena anasema mi mume wa mtu,sasa ukinikaribisha kwako nitashukuru sana madame B

Haya njoo tuyajenge.
Ila uwe na pesa.

Ila serious ......mpende mkeo, michepuko tupo na kazi yetu ni kuharibu na kuchonganisha ndoa kama zenu zenye kulegalega.
....ila yawezekana wewe una vi-element vya ukorofi ndio maana anakuletea tabia hizo usizozipenda.

GD...!!!
 
Basi na mkeo huko anajuta maana nje ana mwanaume ana mlizisha kuliko ww sema tu hawezi kusema..
 
Back
Top Bottom