Sindano mwana ganzi,sije leta msiba.
Ukayaleta majonzi,chozi silo tiba.
Kwa kuleta weredi,injini kuzi chunguza.
Waweza leta ufundi,wenzio kwisha chakachua.
Walikuwapo wakwezi,mabingwa wa kupalamia.
Miembe na minazi,wako juu kudandia.
Matawi yakawa telezi,ahera kwenda mapema.
Magari sio nazi,ikivunjwa unaona.
Japo kwenye yadi,utacheza patapotea.
Yapo ya toka enzi,rami yana chubua.
Jaifongo na Bedifodi,yang'aa kama Korola.
Upwa injini si kazi,dukani wenda nunua.
Waweza pata uchizi,ukweli kuja fahamu.
Kuna yale Mashangingi,bei milioni mia.
Injini ni za Bajaji,zile kutoka India.
Bora kuacha chunguzi,safari unapo ridhia.
Ni kweli ukuzingatia mimi sio mmiliki, sasa kwanini nifanye service kwenye gari isiyo yangu
Haha, we unajua kupanda tu?
Ha ha ha ha ha ha!unaogopa Malori ya kubeba shehena sio!!!???.....na ya kubeba taka he he he he he nayale ya mnadani................!!!!!lol
Umeniacha hoi!
Magari ya mnadani unapotaka kulinunua ndugu yangu kuwa muangalifu, mara nyingi yana hitilafu ndio maana wanakwambia kabisa ' IT IS SOLD AS IT IS', Na yale ya kwenye yadi watu wanaonekana kuyaaminia sana, well yanaweza kuwa na unafuu kulinganisha na yale ya mnada lkn inabidi uwe mwangalifu kweli, twende sasa..........
Sanda ninakuja tena, naomba nisikilize
kuna jambo nimeona, wala usilipuuze
si kama nakudanganya, nenda ukapeleleze
Magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli
usizugwe na idadi, yanapokuwa 'pakini'
Sijaona la zaidi, moyoni hayajawini
uchache umaridadi, nduguyo siyaamini
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli
Angalia breki nyuma, kabla kulinunua
usije pata kununa, kwa nyuma linasumbua
Ukadhani ni hujuma, kumbe hukupambanua
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli
Injini zabadilidhwa, ya 'fuso' kwa ya 'nisani'
Lengo ni kuwaridisha, mnaokwenda yadini
kwa ndani yanang'arishwa, kumbe ni ya hali duni
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli
sisemi yote ni duni, sanda hapa nielewe
Yapo yabebayo kuni, na mihogo ya wenyewe
kwa hili sikurubuni, Wateja yatafutiwe
magari haya ya yadi, yana mwingi mushikeli
sindano mwana wa ganzi
MAGULUMANGU
Sindano mwana wa ganzi, magulu ninakuita
Nasubiri zako tenzi, uniondoe utata
Na sote tuwakufunzi, je nani wakutupata
E ndugu magulumangu, mistari sijapata
Mistari sijapata, nini unachongojea
Irushe yako karata, zinifike zako hoja
kichelewa takufata, lengo ni tuwe pamoja
E ndugu magulumangu, mistari sijapata
Sindano mwana wa ganzi
Ni vipi wayasifia, magari yale ya yadi
Mbwembwe wayamiminia, kuwa ni yamaridadi
Ulaya lishatumia, na sasa hayana hadhi
Magari haya ya yadi, yalisha pandwa kitambo
Elfu kwa maelfu, maili yametembea
Huku kwetu twayasifu, mjini twagereshea
Huu kwangu ni upofu, ya yadi nayabezea
Magari haya ya yadi, yalisha pandwa kitambo
Dereva walisha kaa, ndani wakayaendesha
Yalivyo pata chakaa, kwetu wakayasogesha
Mie leo nashangaa, wengi yawahamasisha
Magari haya ya yadi, yalisha pandwa kitambo
sindano mwana wa ganzi
Mwenzenu nilitamani, gari kulisafiria
Laonyesha la thamani, kwa nje na ndani pia
Kiumbo li wastani, mfano wa gari KIA
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Gari hili lavutia, kwa hilo nakubalia
Rangi yake kahawia, machoni imetulia
Wengi wanaliwazia, na sifa kulisifia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Kilitazama kwa mbele, pembeni limetanuka
Utapatwa na vipele, mwilini kusisimka
Natetemekwa vidole, nikipanda sita shuka
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Kwa nyuma linapendeza, napenda wake mbinuko
Na mwendo likiongeza, lapepea kama puto
Ni kweli sijalikweza, gari hili moto moto
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Muda nilipo patia, gari hili nilipanda
Tena nikashikilia, katikati nikatanda
Kelele nilisikia, ila gari halikwenda
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Gari lilikakamaa, lilishindwa nifikisha
Pale nilipo tazama, mafuta linavujisha
Si kama nalisakama, mashineni kulitisha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Nimebaki na majuto, gari limekinaisha
Sina tena ule moto, wa gari kulipaisha
Mwili bado umzito, bora nisinge liwasha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Bora kupanda bajaji, popote wajipitia
Hazina mwingi mtaji, injini ni ndogo pia
Beteri ukisha chaji, wajitambia na njia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
KLORO na SPRINI, mwaonaje hii hoja
SHOSI naye WAKIJIJI, mchango wenu nangoja
MAGULU uko kundini, LIZZY pia tupamoja
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Na wote nisowataja, msiache kuchangia
Nipeni nyingi faraja, hoja sitapuuzia
Safari niloipanga, katu haikutimia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Malenga wenu
Sindano ya ganzi (Local anaesthesia)
Hilo gari used au brand new?? Natania bana
Tatizo naona hukulifanyia service ya kutosha kabla ya safari kuanza hata hukucheki rejeta kama ina maji poa
Punguza zako jazba,upate kunisikia
Si zile yadi za jaba,huko uende chukua
Kwakuwa ni kaitaba,eti waenda nunua
Umakini watakiwa,si kila yadi watua
Kuna yale ya heshima,hata bei wayajua
Bora tumia hekima,uchague la kufaa
Ni aghali zake bima,hilo upate tambua
Umakini watakiwa,si kila yadi watua
Punguza wako wahaka,natumai waelewa
Usijefanya haraka,utakamatwa na chewa
Pole pole ni Baraka,utapata ulopewa
Umakini watakiwa,si kila yadi watua
Twashukuru Yakuonea.,
Maneno kuntu kutugea;
Ushairi kutumia;
Lugha yetu kukuzia...!
Hata kama ni used au brand new, usipokuwa mwangalifu majority yako hivyo. Hakuna cha service bali bahati tu. Ndio ulimwengu wa kileo.
Yadi hizi yadi gani, unazo zungumzia
Ni zile za baniani, ya zama watuuzia
Au hizi za njiani, ilala na mwenge pia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni
Hata kikuta pajero, sio walikimbilia
wasema kipenda roho, wadhani utatulia
Litakupa mgogoro, majuto utajutia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni
Benzi gari ya makini, dunia inatambia
Leo iweje kundini, yadini watuuzia
Hapa kuna ulakini, kiwango imechujia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni
Yangu nitainunua, mpya toka kwa 'dila'
Popote tatanulia, mashine haina hila
Pozi nitawazidia, za yadi zina msala
Gari nyingi yadini, zina viwango vyake ni duni
Msiojuwa viwango, za yadi mwang'ang'ania
Ondoa yako matongo, hayo walishatumia
Kaulize kule ng'ambo, huku wameyatupia
Gari nyingi za yadini, viwango vyake ni duni
sindano mwana wa ganzi
Sasa hapo ndo utajua mchina ni balaaa muziki mpaka kwenye bodaboda, hata mimi ile gari niliyoshindwa kusafirika nayo nafikiri kulikuwa na mikono ya wachina, maana kwa jinsi ilivyokuwa inaonekana usingedhani kama mashine iko vile
wamesema waswahili,kupanga ni kuchagua
Uepuke ubahili,gari lako kununua
Sije kuwa la wawili,mwisho kaja kujutia
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa
Nimeona kiwandani,wazi ya kijaribiwa
Wamejaribu nje ndani,bila wewe kuelewa
Wamepata burudani,kabla wewe kuletewa
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa
Sikila 'dila' minifu,hapo takuja jutia
Wengine wadanganyifu,wataka kuyapitia
Wamezidi maradufu,ufisadi kufanyia
Hakuna la peke yako,jipya nalo jaribiwa
Hiyo gari gari gani, unayoisema wewe?
Ukute hujui gari, ndo sababu ya kiwewe
Kumbe wewe wa bajaji, gari kwako vipi wewe?
Rudia wako usafiri, siparamie vya wenyewe!
Wewe umepewa lifti, mbio kupiga honi
Ni lazima uwe fiti, bila kuona soni
usije pigwa shuti, uone bora mkokoteni
unajuta kulipandia, kwani ulipandishwa?
Nunua gari lako, uli customize nakwambia
liwe la aina yako, uturi kulipakia
wasilete shokoshoko, wezi kujipakia
huwezi lipiga mnada, kwa jinsi utavolipenda
Mwenzenu nilitamani, gari kulisafiria
Laonyesha la thamani, kwa nje na ndani pia
Kiumbo li wastani, mfano wa gari KIA
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Malenga wenu
Sindano ya ganzi (Local anaesthesia)