Ulikusanya halafu bibi yako aje azoe??
we unafikiri dar ni kama huko kijijini kwenu mnatupa taka mashambani?kutoka magomeni taka zinapelekwa pugu km kama 30.sasa ulitaka niende km 30 kwa miguu?
Acha kukurupuka na kutukana watu, kawaida takataka zikisha kusanywa huwa zinapelekwa wapi, dampo au kwenye shimo lako?
Uzuri wa JF kuna majukwaa mengi ili kila mtu achangie kwenye jukwaa sahihi na analolipenda. Hoja yako hii ingependeza sana kama ungeitupia jukwaa la Utani. Hasara ya kutupa jiwe usiku (Gizani) inaweza kuwa jiwe hilo likamwangukia Mkwe/mzazi wako,utajisikiaje?
Wewe huna akili, sasa ulivyokunya ulitegemea nani azoe??
Mkuu labda wahusika wanajipanga.
mm naona ni ujinga wako unayesubiri karandinga la taka likupitiezile taka tulizokusanya bado zipo tele hazijazolewa.naapa sitashiriki hili zoezi tena ni ujinga
Zoezi la jana ni siasa tupu hususani kwa jiji la dsm!! Tatizo kubwa ni hizo tenda za uzoaji taka walivyopeana, we una kuta mtu ana gari mbili, anapewa tenda kubwa ya uzoaji taka, magari yenyewe ni taka taka!! Likitoka tmk hadi pugu kumwaga taka taka trip moja siku imeisha, unategemea nini?? Nenda pale buguruni sokoni aibu, kidogo upande wa masaki, kuna kampuni ya kishua na magari special kwa uzoaji taka, kazi inafanyika, cha kufanya lazima magari ya uzoaji taka yatafutwe mengi ya kutosha, tena hii kazi wangeachiwa halmashauri husika, wakanunua magari na kuifanya wao, lakini hii ya watu binafsi, hela akadai mwenyewe kwa wananchi, tena wa dsm, mijitu ambayo kutoa 2000,kwa mwezi kama gharama ya uzoaji taka wanaona nyingi!!! Tutasubiri sana dsm kuna vichwa ngumu sana.