Najuta kufanya usafi jana

Najuta kufanya usafi jana

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
22,312
Reaction score
55,971
Zile taka tulizokusanya bado zipo tele hazijazolewa.

Naapa sitashiriki hili zoezi tena..
 
zile taka tulizokusanya bado zipo tele hazijazolewa.naapa sitashiriki hili zoezi tena ni ujinga

Usiposhiriki utapigwa tu, na mimi nasema upigwe maana hakuna namna nyingine ya kufanya.
 
Wewe huna akili, sasa ulivyokunya ulitegemea nani azoe??

Mjinga utakuwa wewe mkuu.Jana tumepiga kazi tukiambiwa kuwa jiji watakuja kubeba lakini sasa zimeanza kuoza na kukusanya nzi.
 
zile taka tulizokusanya bado zipo tele hazijazolewa.naapa sitashiriki hili zoezi tena ni ujinga



Yaani bado taka za majipu (Usaha) hadi leo hazijazoelwa! Mkuu itakuwa unaishi magogoni pale karibu na ferry wewe.
 
Mkuu uliwasiliana na wahusika?

Zoezi la jana ni siasa tupu hususani kwa jiji la dsm!! Tatizo kubwa ni hizo tenda za uzoaji taka walivyopeana, we una kuta mtu ana gari mbili, anapewa tenda kubwa ya uzoaji taka, magari yenyewe ni taka taka!! Likitoka tmk hadi pugu kumwaga taka taka trip moja siku imeisha, unategemea nini?? Nenda pale buguruni sokoni aibu, kidogo upande wa masaki, kuna kampuni ya kishua na magari special kwa uzoaji taka, kazi inafanyika, cha kufanya lazima magari ya uzoaji taka yatafutwe mengi ya kutosha, tena hii kazi wangeachiwa halmashauri husika, wakanunua magari na kuifanya wao, lakini hii ya watu binafsi, hela akadai mwenyewe kwa wananchi, tena wa dsm, mijitu ambayo kutoa 2000,kwa mwezi kama gharama ya uzoaji taka wanaona nyingi!!! Tutasubiri sana dsm kuna vichwa ngumu sana.
 
Kwani suala la kufanya usafi halihusishi kuzoa na kubeba taka kwenda kuzitupa?
 
Kwani suala la kufanya usafi halihusishi kuzoa na kubeba taka kwenda kuzitupa?

we unafikiri dar ni kama huko kijijini kwenu mnatupa taka mashambani?kutoka magomeni taka zinapelekwa pugu km kama 30.sasa ulitaka niende km 30 kwa miguu?
 
we unafikiri dar ni kama huko kijijini kwenu mnatupa taka mashambani?kutoka magomeni taka zinapelekwa pugu km kama 30.sasa ulitaka niende km 30 kwa miguu?[/QUOTE

Hawa wanaishi sigimbi sasa wanaleta mazingira ya huko dar!! Sio kosa lao mkuu
 
Hata huku mikocheni kuanzia shoppers plaza mpaka kawe ukwamani ni milima ya taka imepangwa barabarani! Huu ni wendawazim
 
Wewe huna akili, sasa ulivyokunya ulitegemea nani azoe??

Acha kukurupuka na kutukana watu, kawaida takataka zikisha kusanywa huwa zinapelekwa wapi, dampo au kwenye shimo lako?
 
Back
Top Bottom