Nimepitia mengi sana, Mungu amenipitisha kwenye mambo mengi, ameniokoa na kunitoa kwenye vitu vingi. lakini kuna kitu kimojawapo kilichobadilisha kabisa mwelekeo wangu kimaisha, ni kitabu cha ISAYA 53. soma yote, ni mistari michache tu hata dakika kumi haziwezi kumalizika. ndani ya sura hiyo, kauli moja tu ambayo Mungu aliitamka nikaelewa kwamba kumbe bila Yesu Kristo, Mungu hatutambui na hataki hata kutuona? ili Mungu akubali kutuona, tunatakiwa kwenda kwa mgongo wa Yesu Kristo, hapo ndipo ameahidi atatusamehe dhambi zetu.
sio kwamba hataki kutuona kwasababu yeye anatuchukia sana, hapana! Mungu ni mtakatifu sanaaa, hakuna uchafu wowote ndani yake, utakatifu wake ni sawa na moto ulao unaozidi moto uyeyushao dhahabu na kutenganisha makapi na dhahabu halisi, hivyo uendapo kwa Mungu kama una dhambi akikusogelea unaweza kuteketea kabisa kwasababu yeye ni moto ulao. ndio maana hakuwashukia waisrael hadi alipowaambia wajitakase kwanza. wakaomba na kufunga, wakakaa mbali na wake zao (hii ni fundisho, hata wewe ukitaka kufanya maombi ya kufunga, kaa mbali na mkeo, nafikiri ukiwa unalala naye akili yako huwa kwake zaidi zaidi ya kuwa kwa Mungu, hivyo hautajimimina absolutely kwa Mungu)......
Isaya 53, kuna mstari ulinichoma anaposema "and for his sake, I will forgive their sins"...kumbe God forgives our sins just for the sake of his servant Jesus Christ?....na hii ndio siri kubwa ambayo wengi hata walipoambia hawakuiamini, kwamba yalikuwa mapenzi ya Mungu Yesu azaliwe na aishi maisha ya aina ile, ateswe na kumwaga damu namna ile, siku ya tatu afufuke namna ile, ......ukimwambia Mungu, ukimkumbusha Mungu kwamba, Mungu akumbuke jinsi Yesu alivyomwaga damu yake, aikumbuke ile damu ashuke kukusamehe, na uingie kwenye agano naye, agano la damu ya Yesu awe Mungu wako na wewe uwe mtoto wake, yeye ashughulike na mambo yako na wewe umtumikie, kwasababu Mungu ni Mungu wa maagano, na kwenye agano la Damu hasa ya Yesu huwa hakwepeshi.....utaona maisha yako yatakavyobadilika. HIVYO NDIVYO nilivyopata siri ya namna gani kusogea mbele za Mungu.
Kusogea mbele za Mungu sio kwa utani utani kama vile Mungu ni binamu yako....lazima uende kwa unyenyekevu wa hali ya juu, uende ukiwa na moyo uliopondeka, kamwe usijihesabie haki usogeapo mbele za Mungu, mwambie Mungu mimi ni mwenye dhambi tu na ninasogea kwako kwa kupitia Yesu Kristo tu (asingekuwa Yesu nisingesogea kabisa), tunafanya dhambi sana kwa mawazo, maneno, matendo kwa kujua hata kwa kutokujua....Yesu alitoa mfano wa msomi wa dini aliyesimama akasema "Mungu, angalia mimi natoa sadaka, nafanya haya na haya, sio kama yule....etc", mtoza ushuru mmoja (kama sikosei) akasimama, hata mbinguni hakutazama, akajipiga kifuani na kusema "Eee Mungu nisamehe mimi ni mwenye dhambi"....Yesu alisema huyo wa pili ambaye hakujihesabia haki ndiye aliyeenda nyumbani akiwa justified (amesamehewa dhambi kabisa). Mungu anataka twende kwa unyenyekevu mbele zake, na kila unachofanya, iwe kwenye kuimba, kufanya maombi, fanya kwa njia ya Yesu Kristo ukijua ya kwamba Mungu hawezi kukupokea kama hautaenda kwake kwa njia ya Yesu Kristo. mwenye masikio na asikie neno hili.