Najiuliza maswali sipati majibu

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,011
2,165
Habar za midaa hii wana jf?

Wacha niende kwenye mada husika.Mara nyingi huwa najiuliza maswali hii hali inatokana na nini?
Unakuta kuna wakati mambo yako yote yanaenda kombo.mfano marafiki wote wanakukwepa,hakuna anayekujali,hata ukisalimia staff wenzio hakuna bashasha.ama wakati mwingine wanakausha kama vile wako mbaali kwenye mawazo mengi.Dili zako zinabuma unakuta unatumia nguvu nyingi sana lakin mafanikio ni kidogo ama hakuna kabisa.Na ukiangalia vizuri hakuna ulipokosea.

Kuna wakati from nowhere unashangaa kila unachofanya ni super.kila mtu anataka kuwa rafiki yako.wanawake wote mlioachana hata kama ni vibaya wanaonesha dalili ya kurudi.mahusiano na staff unakuta yanaimarika.dili ndogo.nguvu ndogo mafanikio makubwa yana unafanikiwa mambo yako mpaka unashanga!!

Lakini ukikaa ukajiuliza hakuna chochote ulichobadilisha katika mfumo wako wa maisha ukachukiwa au ukapendwa.

Ndo nashindwa kuelewa hii hali inasababishwa na nini?sijui labda wenzangu mmeshawai kutokewa na hali kama hii?je sababu ni nini
 
Ndio maisha jinsi yalivyo kuna kupanda na kushuka... CHANGAMOTO KWENYE MAISHA NI LAZIMA...Usiwaze huenda ni mapito tu
 
Wale wanaojiita wanajimu au wasoma nyota watakuambia nyota yako imeingia giza na unahitajika kusafishwa. Usipokuwa makini unaliwa pesa. Huo ni mzunguko wa kawaida wa maisha.
 
Kuna msemo huwa unasema hivi: sio lazima rafiki yako wa zamani aendelee kuwa rafiki yako siku zote.

Na mwingine unasema hivi: mpende umpendaye Upendo wa Kiasi kwani huwenda siku moja akaja kuwa rafiki yako, na mchukie rafiki yako chuki UA Kiasi kwani huwenda siku moja Inaweza kuwa rafiki yako wa dhati.
 
Hauko peke yako maisha ndio yalivyo hata mimi kuna kipindi wanawake nilikua nikiwasalimia wanauchuna lakini sasa hivi siwasalimii lakini wanaitikia.Muombe sana mungu maisha ndio yalivyo na watu wenye historia ya kutokewa na hali kama hiyo mara kwa mara huwa ni watu watakaopata mafanikio makubwa hapo baadae
 
Maisha ya binadamu ni kama rangi ya kinyonga,nje yanabadilika lakin Ndani yuko vile vile..
 
simply kupanda na kushuka, ila linaloniumiza mimi upande wangu ni kuwa kuna siku kila kitu nakiona kizuri kinapendeza kinavutia ila kina siku kila kitu nakiona kibaya hata watu na vitu ni vile vile vya kila siku inajirudia rudia
 
simply kupanda na kushuka, ila linaloniumiza mimi upande wangu ni kuwa kuna siku kila kitu nakiona kizuri kinapendeza kinavutia ila kina siku kila kitu nakiona kibaya hata watu na vitu ni vile vile vya kila siku inajirudia rudia
Utakuwa unasumbuliwa na msongo wa mawazo, jaribu ku note down hizo siku unazojisikia kila kitu kibaya....halafu ungalie huwa inajirudia kila baada ya mda gani? Au pengine kuna kitu kinasababisha hujakielewa bado.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom