Najichukia kwa hili tatizo langu la ngozi, nimekosa mwenza

am a girl

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
748
504
Mamboz,

Jamani kama mnakumbuka nilikua natafuta mchumba na hali yangu niliyonayo, wengi walijitokeza wakidhani natania labda, walihisi mimi ni mzuri sana ila natania.

Kusema ukweli nipo kama nilivyosema na nimerudi tena kuomba msaada kwa anaejua dawa ya makovu tafadhali, sio ya ajali yani yanatokea tu hata nikijikuna kovu linabaki, pia nikiumwa na mdudu lazima kovu libaki,nikijikwaruza kidogo bas kovu hilo.

Wanaume pia hawaniangalii hata mara mbili, niko mpweke, sina hata mwenza.

Nachukia sana ngozi yangu na sijui shida ni nini, naomba tafadhali kwa anaejua dawa ambayo itanifaa.

Wanawake wenzangu nisaidieni, kina baba, kina kaka naombeni mnitajie dawa itakayoondoa makovu haya jamani.

Bio oil nimejaribu haifanyi kazi, aloevera hua napaka sioni matokei, limao pia hakuna kitu.

Najisikia vibaya sana, mda mwingine hua nikijiangalia nalia tu, why me?

Msaada wenu ndugu zangu tafadhali.
 
Hapana,ndio ikoje hiyo.
Nitajaribu kupima.
huwa ni mbaya sana maana hupelekea mtu kuugua majipu, upele au vidonda ndugu na wakati mwingine hata mjamzito anaweza kujifungua mtoto ameoza kabisa au yuko hai ila anakuwa kama vile kaunguzwa na uji au maziwa ya moto. Kapime fangasi ya damu na magonjwa mengine ya damu, utapata kupona tu. JIKAZE.
 
huwa ni mbaya sana maana hupelekea mtu kuugua majipu, upele au vidonda ndugu na wakati mwingine hata mjamzito anaweza kujifungua mtoto ameoza kabisa au yuko hai ila anakuwa kama vile kaunguzwa na uji au maziwa ya moto. Kapime fangasi ya damu na magonjwa mengine ya damu, utapata kupona tu. JIKAZE.
Uwiii jamani dah,asante nitajaribu kupima
 
Nikukague kwanza nijue haswa tatizo lako linasababishwa na nini... na matibabu yake yaweje....
 
Njia nyingine ya uhakika kwa wenye uhakika.

Amua kuokoka kweli kutoka moyoni, nenda kwenye kanisa la watu waliookoka KWELIKWELI kama T.A.G au E.A.G.T kisha wambie watumishi UNATAKA KUOKOKA, kisha watakuongoza kupokea wokovu.

NB: Si kila tatizo linaweza kutibiwa kwa dawa. Mengine yanasababishwa na nguvu za giza hivyo JINA LA YESU PEKEE LINAWEZA KUKUOKOA.

Kama kweli umeamua kuokoka kutoka moyoni, wambie wakuombee tatizo lako la ngozi, watakuombea utapona kama una imani kwamba Mungu anaweza pia kama umemaaishisha kumfata Mungu/kudumu katika wokovu mpaka mwisho wa maisha yako.

NB: Usiende kuokoka kama unakwenda kujaribu utapona au la! Bali nenda kaokoke kwa kumfata Mungu bila kujali kama atakuponya au hatakuponya. Kwani Wokovu utakupeleka mbinguni. Pia Ukiokoka Mungu anaweza kukuponya magonjwa na matatizo yako yote.

Wokovu si dini, bali ni mabadiliko ya NAFSI yanayofanywa na Mungu kwa yeyote anayempokea Bwana Yesu ili amuokoe na dhambi na jehanamu ya moto.
 
Back
Top Bottom