WanaJF,
Nawasalimu.
Kama mtakumbuka mimi Onambali, nimetanagaza nia yangu kupitia JF ya kugombea urais wa nchi yetu mwaka 2030. Nashukuru kwa maoni yenu. Nina sababu nyingi kwa nini nataka kuomba ridhaa ya wananchi ili niwe mtumishi (rais) wao na nilishaeleza mambo machache katika thread yangu iliyopita.
Ninaumia sana kuona nchi yetu inaharibiwa mbele ya macho yangu. Tunahitaji viongozi watakaoweza kutafsiri wakati tulionao na ule ujao yaani kuamua na kupanga muelekeo wa taifa. Ni aibu na hatari kubwa katika maendeleo yetu kuwa na kiongozi wa uma ambaye ni mbinafsi (anayefikiri yeye na famila yake tu ndo wanastahili kufaidi mema ya Tanzania aliyotukirimia Mungu), mchoyo (anayenyima haki ya watu kumkataa- yaani mpenda madaraka), muongo (anayeongea bila facts kwa lengo la kuwadanganya wasiobahatika kwenda shule), mtapanya mali (anayetumia utajiri wa uma kwa mambo yasiyokuwa ya lazima), mlafi (anayekula hadi chenga ambazo waliokosa fursa wangezitumia kujiendeleza), fisadi (anayekumbatia ufisadi kwa sababu ya ufisadi), mropokaji (anayeongea bila kufahamu kwamba kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko yeye), mtaka starehe ( kwa sababu hana uchungu na wanaoteseka kwa maisha), mzinzi (kwa sababu hajajiwekea taratibu za kuutawala mwili wake, hivyo pia kutumia nafasi hiyo kulipa fadhila katika utoaji wa huduma za kiuongozi). Ndugu wanaJF, viongozi wa aina hiyo niliyoeleza hapa hawawezi kutufikisha popote. Wataendelea kuwafanya waafrika watumwa wa umaskini. Maskini wa kufikiri sio mbunifu, hana maona ya mbali maana kwake uongozi ni kama ‘uungu' wa kuwafanya wengine kuwaabudu na kutokuwa na haki ya kufurahia urithi na utajiri wa nchi yao.
WanaJF,
Watanzania wengi wanachukizwa na mambo mabaya yanayoendelea katika nchi yetu na huishia kusema...'tunahitaji viongozi wasafi, watakaofanya jambo hili au lile'..., lakini wengi hawapo tayari kujitoa kuanza mashambulizi ili kufanikisha nia yao kwa nchi yao. Hufikiri kazi ya kukomboa nchi kutoka katika mikono ya umaskini na ujinga ni ya watu fulani na haiwahusu wao. Mimi Onambali, nimeamua kabisa kutoka moyoni kuwa kiongozi wa Tz. Naamini ninauwezo wa kuitoa Tanzania katika maji taka na kuifanya (kwa nguvu yetu wenyewe na rasilimali alizotujalia Mungu) kuwa nchi itakayotoa matunda mema ya upendo, amani, furaha, na umoja wa kweli wa kizalendo utakaotawaliwa na haki, usawa katika fursa zote na matumizi mazuri ya sayansi na tekinolojia. Nafahamu ukweli unauma na waweza kunigharimu kifo lakini heri nife kama shujaa kwa manufaa ya uma kuliko kuishi kama dhalimu.
Naipenda nchi yangu na watu wangu. Ee Mwenyezi Mungu, naomba uibariki nchi yetu TZ.