Naitaji watu wenye uelewa mpana na busara wanishauri juu ya huyu mchumba wangu

Chagua moja, bora uwafurahishe watu uishi maisha ya machungu na majuto au ufanye maamuzi yatakayokupa furaha na amani kwenye maisha yako?
Kumbuka tunaongelea mtu utakaeishi nae maisha yako yote yaliyobaki hapa duniani, usiogope aibu ya watu ukang'ang'ania au kulazimisha ndoa, bora mambo yashindikane kwenye hatua ya mahari lakini sio ndoa kuvunjika.
 
Umepitia mangapi ana

Mbona haya mambo ya kawaida tu

Hili nalo litapita kama lile la kwanza

Leave your life mlee mwanao icho ndo muhimu kwako kwa sasa hakuna lingine
 
Shida ni mzee tunamwambiaje kwa hili??
Kwani lazima u mwambie? Wewe mwambie baba kwasasa nataka nifanye mambo yangu na nataka nichunguze maisha yake kwanza yashije kuwa kama ya yule mzazi mwenzangu, shost una maisha yako na mtoto unaye kwanini ujipe pressure zisizokuwa na maana anayekupenda wala hanaga shida wala kona kona nyingi kila kitu huja direct, inaonekana unapenda sana ndoa sasa hao watu unao waonea aibu sijui majirani walikula sana wakati wa mahari wanakusidia nini, wakati shida unapata wewe wanawake wengine sijui mpoje, usipo jijari mwenyewe nani akusamini? Sio kila anayekuja mme wengine vipanga hata mbwamwitu huweza kuvaa ngozi ya kondoo, tumia akili chuo ulienda kufanya nini ishi maisha amani bibie!
 
Ukivunja mahusianao jaribu kutulia na kujiuliza kwanini yamevunjika? Sio leo umeachana na mtu kesho anakuja mwingine bila hata kuchunguza eti kajitambulishe kwa wazazi kuchumbia si kuoa tuliza kichwa nahii haiwezi kuoza mpe mtu sahihi sio kila anayetangaza ndoa ni muoaji wengine vifimbo cheza
 
Naomba nikuukize swali kabla sijakushauri ukinijibu nitakusadia na naamini utapata pakutokea.
1.Unaona unamuongelea baba kama mtu ambaye haishi na mama ni kweli?wametengana au nini kilitokea

2.
 
Dada Anna mi ushauri wangu kwako ni mwepesi sana
Hebu punguza pressure ya ndoa, acha kufikiria watu watakuonaje
Sasa hivi fikiria mwanao utamleaje na pia jenga mazingira ya kukufanya uwe na furaha kupitia ndani yako mwenyewe, usiweke mazingira ya kupata furaha kupitia kwa mtu mwingine.
 


Wewe na wazazi wako muache kwanza usanii, muwe straight na msipike uongo, achana na hayo yote hayo, concentrate kwenye maisha yako na mwanao
 
Kikubwa ni uvumilivu umekutana na huyu akiwa mkubwa na miaka mingi tu na anatabia zake ambazo kazizoea kwa miaka hyo yote uliyomkuta nayo kwaiyo itakugharimu miaka mingne kama hyo uliyomkutanayo ili akae sawa wote mbatoka familia tofauti na katika kila familia kuna mila,desturi na tamaduni ambazo kila mtu kalelewa nazo so vumilia tu yanamwisho hakuna sehemu iliyonyoofu.
 
Sasa kaka wewe unaitaji ushauri au unaitaji watu wenye busara maana ivyo ni vitu viwili tofauti em specify unaitaji kipi kati ya ivyo viwili
Kaka anabeba mimba! Au mleta uzi ndo kajikoroga?
 
Tatizo lako neno 'ndoa' linakustua mno.. Pole, epuka kufanya maamuz ya kukurupuka. Pga chni jamaa, anza upza na uwe busy na maisha ya kiuchumi na kulea mwanao. Ndoa hailazimishwi
 
Focus sana on ur life na maisha ya mtoto wako... Hayo ya nyuma yaliyopita yatopezee kabisa..
Time itafika u wil get the right one for u n always usifanye vitu kwa haraka haraka
 
Mpotezee tu hamna jipya apo utakufa bure kwa presha wakat mwenzio anaenjoy mema ya dunia
 
pole kwa yote kwanza

then it seems like you are so cheap


then unaharaka na maisha

tulia kwanza


tena usiingie kwa mahusiano ukamuonesha live kuwa unataka ndoa ni mbaya sana
 
shule umemaliza???......kapime na afya yako.....then rudi kanisani.....mfuate mwokozi yeye anayaweza yote......wanaume hatuachi vya dezo.......vigumu vinalainishwa....vilaini vinamumunywa....
 
Shosti,natumaini u mzima na uko timilifu nikimaanisha una viungo vyote vimpasavyo MTU kuwa navyo,.piga moyo konde ona kama ulikengeuka tuu kibinadamu,.achana na mapenzi na kuota NDOA,tayari una mtoto PAMBANA kujiongezea kipato ili uishi maisha yako ya Amani na umtunze mwanao,.kingine KAA magotini pa Mungu omba huruma yake pengine kibinadamu ulienda kinyume na ulimkosea Mungu,Fanya toba na umtazame yeye tuu kwani yeye ni wa haki hata hutusamehe madhambi yeti,.tutafute UTAKATIFU kwanza na hayo mengine atatujazi..pole sana.
 
Mumu dadangu, ninafurahi kuona umepevuka kiakili, hii inatia moyo sana.
Mungu aendelee kukupa hekima uwasaidie ndg zako
 
Pole my dia,najua ni namna gani unajisikia lkn nikuombe utulie kwasasa,ebu weka kando maswala ya mapenzi fanya kazi kwa bidii lea mtoto wako jipendee jithamini kuwa karibu na Mungu wako
Wakati wa Mungu ukifika kila kitu kitanyookaa na haya unayopita itabak story acha kuangalia marafik zako wameolewa sijui umri,sijui baba hapana kila jambo na wkt wake sahihi,,mm niliolewa mdogo kdg marafikzangu hasa walionipita umri walikua wanapata mawazo lkn leo hii wote wameolewa na waliobak soon tutakula ubwabwa wao
Mwisho ukipata mchumba achana na biasharaa za kumpeleka nyumban tulia ujipe nao mda
Tulia Anna utapata presha mwanao aje kupata shida plz kuwa mwanamke jasiri kaza moyo songa mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…