Ahahaha...dogo anatafuta business partner kama anatafuta demu kona baa. ahahahha...hiyo ni kazi ngumu sana kuliko hata kutafuta rais wa tanzania.
Umemaliza chuo jana kwanini unataka kuanzisha company ya umeme ya ukandarasi?....kazi utapata wapi?...unayo network ya kazi?...mtaji wako ni nini hasa ili umvutie huyo partner kukujoin?.....angalia dogo usikute una tester na screw drive ukaona unaweza ku-run electrical company....bado sana.
Ushauri wangu kama kaka mkuu.
1- Endelea kufanya kazi kwa waajiri wako ili ukuze uzoefu na client base yako ikuwe.
2- Tunza kiasi unachokipata na kusajili kampuni yako kwanza
3- Anza kuomba kazi toka kwa clients uliowahi kufanya nao kazi kupitia waajiri wako ukiwaambia umeanzisha kijikampuni chako wakusaidie kazi kikuwe.
4- Kusanya msingi wa kutosha kununua kazi moja ya kutokea kisha ukishapata kazi moja hiyo jienguwe kwenye ajira ya maboss wako.
5- Serious partner atatoka huko utakakokuwa unafanya kazi na wenzako au ma-clients waliofanya kazi na wewe.
Kama unaona ushauri wangu unafaa niambie nijuwe nimechangia kubadilisha maisha ya kijana mmoja wa kitanzania, ila kama unaona haufai pia nijulishe nijuwe nimemuharibia maisha kijana mmoja wa kitanzania ili jumapili niwahi kanisani kufanya sala ya toba.
Ni hayo tu.