Naisubiri kwa hamu tathmini ya miezi 6 Magufuli akiwa Ikulu

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Waje watwambie bomoa bomoa na tambo za kubomoa hotel za ufukweni na nyumba 5000 kila jiji ziliishia wapi?

Waje watwambie elimu bure ilivyofulisha wanafunzi na leo miti inakatwa nchi nzima kutengeneza madawati ambayo baada ya muda yataharibiwa na mvua na jua maana hakuna madarasa.

Waje watwambia baada ya juhudi za kurekebisha bandari kwa ziara za PM leo bandari mizigo inayopita ni chini ya 40%. Wafanyabiashara wamekimbilia Mombasa, Beira na Duban

Waje watwambie imekuwaje baada ya siku 30 walizopewa waliotelekeza viwanda wavirejeshe wamerejesha vingapi? Maana nilimsikia waziri wa viwanda akisema wananchi wajue kuna suala la mikataba. Kumbe! hakujua?

Waje watwambie ile amri ya daladala za Dar zisisimamishe abiria lilifanikiwa kwa kiasi gani?

Waje watwambie tr 1.3 zinazokusanywa kila mwezi zinaenda wapi? Halmashauri zinalia fedha kiasi wamekopa posho za madiwani ambazo hutokana na OC. Madiwani hawajalipwa posho zao kwa miezi zaidi ya miwili.
 
kwa hiyo kwa sasa una hamu?? Lowassa au Mbowe wanayo taarifa?

umewezaje kukaa na hamu kwa kipindi chote hiki? unafika mpaka miezi sita?

Utaandika sana, sana, sana, utajaza server na kuandika kwa uchungu wote-sidhani wala sifikirii hamu yako itakatika

wala hautapata unachokitaka
 
Mtoa maada umekurupuka kama chadema walivyokurupuka kuuza chama kwa makapi ya ccm..

Ulitakiwa umulike na upande Wa pili.

Makusanyo ya tra kwa mwezi.

Elimu bure

Ujenzi Wa kinyerezi two

Ujenzi Wa flyover

Vitanda muhimbili.

MSD kuwa na maduka yake
 
Makusanyo ya TRA yamebadili kwa kiasi gani maisha ya watu?
 
kwa hiyo kwa sasa una hamu?? Lowassa au Mbowe wanayo taarifa?

umewezaje kukaa na hamu kwa kipindi chote hiki? unafika mpaka miezi sita?

Utaandika sana, sana, sana, utajaza server na kuandika kwa uchungu wote-sidhani wala sifikirii hamu yako itakatika

wala hautapata unachokitaka
kama wewe ni mwanaume, hutakiwi uandike hivi
 
Mtoa maada umekurupuka kama chadema walivyokurupuka kuuza chama kwa makapi ya ccm..

Ulitakiwa umulike na upande Wa pili.

Makusanyo ya tra kwa mwezi.

Elimu bure

Ujenzi Wa kinyerezi two

Ujenzi Wa flyover

Vitanda muhimbili.

MSD kuwa na maduka yake
Nina uhakika 100% wa ninachosema
 
Back
Top Bottom