data1
Senior Member
- Apr 20, 2014
- 136
- 3
Naamini serikali ya ccm haiendi na haitaangalia maslahi ya wananchi bila ya kusukumwa sukumwa na vyama vya upinzani, hususan chadema.. lakini pia naamini hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kuichukua nchi hii ya Tanzania kwa sasa.. hivyo basi waendelee kupiga kampeni ili wapate wabunge wengi zaidi na kuipa challenge serikali kwa maslahi ya wananchi!
Naisikitikia chadema kwasababu wanapoteza focus yao ya uchaguzi wa 2015, na kufanya mambo mengine yanayopunguza umaarufu wao. Wanapoteza nguvu nyingi sana kutengeneza mambo wanayoyaharibu wao wenyewe ambapo nguvu hizi zingetumika kuweka uimara wao katika uchaguzi ujao.
Chadema ikishika nchi hakutakuwa na mabadiliko watanzania wanayoyategemea kwasababu chama hakibadilishi tabia ya mtu. Chadema na CCM ni watanzania wenye chimbuko moja! na wote si wazalendo kwasababu wanapigania maslahi yao binafsi. Hivyo CCM wabaki wakishika nchi na chadema kibaki chama kikuu pinzani na waache upuuzi wanaoufanya ili waweze kuongeza wabunge uchaguzi ujao na labda watakuwa tayari ili kushika nchi mwaka 2020.
Mwisho wa siku, tunaona tofauti ya wenye experience katika siasa na wale ambao wana muda mfupi katika siasa. "siasa haihitaji kukurupuka na kuendeshwa kwa hisia tu, unahitaji kutumia akili kufanya decisions"