Jana wakati Mhe.Waziri wa fedha akisoma BAJETI YA MWAKA 2016/17 alisema kuwa kuanzia Julai Mosi Serikali imefuta KODI YA ZIMA MOTO. Naipongeza Serikali kwa hatua hii ya kufuta Kodi ya Zima Moto kwa sababu zifuatazo:-
- Hakuna faida inayotokana na kodi hii. Wafanyabiashara wamekuwa wakinyanyaswa kila kukicha.
- Hakuna fire extinguisher unayopewa pindi unapolipa kodi,inabidi uinunue nje ya kodi uliyolipa.
- Hakuna ushauri wanaoutoa, kipaumbele ni kodi tu.
- Kwa hili naipongeza Serikali ya Mhe. Magufuli.