6. Mrusi ni baba wa heavy machines duniani. Ukitaka kujua heavy machines ninini basi nenda urusi.
Hee Mkuu unasisitiza huu uzi usifutwe kwanini? unakijua lakini ulichokiandika na kinachoendelea kutokea? Russia ni taifa la propaganda kabisa hata mimi kabla nilikuwa naisikia Russia hivyo ulivyoisikia wewe na hilo neno Mrusi lilikuwa linatisha na kuhofisha sana kwenye masikio ya watu lakini kumbe ilikuwa ni hofu ya woga.
Kinachotokea kwenye hii vita na Ukraine nimekuja kuijuwa kumbe Russia ilipandishwa hadhi sana na Putini lakini na wafuasi wao kuliko uhalisia., Russia ilipoivamia Ukraine nilijua hardly itawacost siku 2 au 3 hivi kumaliza mchezo na kukamilisha malengo yao, wakaivamia ukraine na mabomu kila upande yakitokea lakini baada ya siku 30 sikuona malengo yao hata lengo 1 likiwa limetimia, zaidi niliona wamepoteza wanajeshi wao wengi sana kwenye hiyo waitayo operation kuuliwa na hatimae kurudi nyuma na kwenda kushikilia Donbas ambayo kabla walishapachika bendera zao. mpaka naandika hapa leo ni takriban siku 60 sijaona malengo yake yakitimia
Juzi Putini ameilalamikia Marekani kwamba isiisadie Ukaraine kwenye vita, nikaja kufahamu kumbe Russia atakuwa hana ubavu Marekani anapoamua kupigana naye na ndio mana amechukua muda wote huo na hana uhakika ni lini atafanikiwa.,
Natafakari kwamba Marekani pale Ukraine hakuingia fully, ni vile anakuwa anapeleka silaha zake chache chache tu lakini Russia imemcost muda mrefu sana sasa miezi miwili ana struggle napata jibu kwamba Urusi ilishamiri kwenye masikio ya watu tu lakini sivyo ilivyokuwa inapambiwa pambiwa. SWALI linakuja je NATO wangeingia fully huyu Putini angekuwa na hali gani???
Na juzi meli yake ya kivita ambayo Russia ikijivunia na waliitumia sana kwenye vita ya Syria ikaripuliwa na kuzamishwa nikasema kumbe Russia hawako salama kumbe ni visible sana lakini pia zile helkopta 2 zilizoenda kuripua ghala lao la mafuta mpakani na ukraine ambapo wakitumia kwa shughuli zao za kuweka mafuta nk, kwenye hiyo operation nikasema kumbe Russia ilipaishwa sana kumbe hata anga lao liko visible wameshindwa ata ku-control, kwa ufupi ni kwamba Russia inapigika iwe mchana au usiku.
Nimekuja kugundua kwamba kumbe Russia uchumi wake mkubwa ukitegemea ulaya na Marekani sasa baada ya vikwazo kumbe hana ubavu wa kujiendesha ni zile zile tu kelele za majigamo kwa wasiojua nini kinaendelea kule urusi.
Nimeona nijibu kwa ufupi hiyo no6. tu hayo mengine nimepuuzilia mbali naona hana mana