Chimbuko la ugaidi duniani ulipoanzia mpaka sasa hivi ulipofikia.

  • Thread starter Kanungila Karim
  • Start date

Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
13,286
Points
2,000
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
13,286 2,000
"Katika dunia ya leo ambayo silaha za Kinyuklia zimeyafanya majeshi yasiwe na umaana wowote ule, ugaidi pekee ndiyo silaha yetu kuu" - Jenerali Aleksandr Sakharovsky mkuu wa idaya ya kijasusi wa K.G.B


SEHEMU YA KWANZA:
HISTORIA FUPI YA UGAIDI KATIKA HISTORIA YA UTAMADUNI WA MWANADAMU.
Kwanza kabisa chimbuko la ugaidi ni la muda mrefu hata kabla ya Marekani, Uingereza wala Urusi kuwepo, kama alivyosema mkuu MSEZA MKULU hapo juu. Miaka ya nyuma Ugaidi ulikuwa ni mlengo wa kisiasa, kifalsafa au kidini unaoamini katika kutumia vurugu, mauaji na fujo dhidi ya raia wasio na hatia au mali zao ili kuwafanya wakubaliane na matakwa yenu.
Mfano mzuri tu ni kile kilichowahi kufanywa na wapiganaji wa kanisa la Katoliki maarufu kama THE KNIGHT TEMPLERS dhidi ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kiyahudi mnamo karne ya kumi na moja wakati wa vita za kidini (Crusades).
Kwenye hiyo vita wapiganaji wa Kikatoliki waliwashinda Waislamu na kuwakamata wanawake na watoto na kuwachoma visu, kuwatesa na kuwachoma moto huku wakiimba "Tunakupenda Yesu". Dhana nzima ilikuwa siyo dini lakini ni kutuma ujumbe kwa Masultani wa Kiislamu kwamba msipokubaliana na Kanisa na mkiendelea kuwashambulia wakristo wanaokuja mashariki ya kati hasahasa Yerusalem ni lazima mtakufa kama wake zenu na watoto zenu.
Japo kadiri miaka inavyoenda ugaidi ukazidi kubadilika hasa hasa baada ya kugunduliwa kwa Unga wa bunduki barani Ulaya. Hili liliwezesha kufanya ugaidi ambapo mtu anaweza kujilipua mwenyewe akiwa na mlengo fulani. Mfano baada ya Vita ya mwaka 1601 ambapo Uingereza ilipundua utawala wa Kanisa la Katoliki nchini mwake na kuanzisha Uanglikani, na kulikuwa na hekaya nzito za kuwazima wakatoliki na wafuasi wake.
Mwaka 1605 mtu anayeitwa Guy Fawkes alitaka kujilipiua kwa baruti chini ya bunge la Uingereza lakini akashindwa.
Dhumuni la Guy Fawkes lilikuwa na mlengo wa kigaidi. Kuwatishia raia wa Uingereza kwamba hawawezi kushindana na Kanisa la Katoliki; maana angefanikiwa kuwaua Wabunge na Mawaziri basi utawala wa Katoliki ungerudi kwa kasi nchini Uingereza kwasababu raia wasingekuwa tena na Imani na serikali mpya hivyo kukubali kurudi kwa Papa ambaye aliaminiwa kuwa ni mwakilishi wa Mungu hapa duniani hivyo kumpinga isingewezekana kabisa.SEHEMU YA PILI: HISTROIA FUPI YA KUKUA KWA UGADI MNAMO KARNE YA 15 HADI 20.
Ikumbukwe kwamba kuanzia karne ya 15 hadi 19 kulikuwa na mabadiliko makubwa ya kifalsafa. Ambapo wengi hupenda kuuita wakati wa mnuruisho (Age of Enlightenment). Mataifa mengi yalianza kuachana na falsafa za kidini na falsafa za kifalme zisizokuwa na maana, mbele wala nyuma. wanadamu wakaanza kutumia ubongo wao kufikiri, walijiuliza maswali kama:
Je, kuna Mungu? Je, Kwanini Mfalme atawale bila kuulizwa? Je, Kwanini nisipate haki zangu? Je, nikinyimwa haki zangu nifanyaje?
Watu waliamini kwamba kila jawabu la mwanadamu linapatikana kwa kupitia ubongo na nguvu zake pekee. Na ni lazima kila mwanadamu aheshimiwe utu wake kwasababu tu ni mwanadamu.
Mfumo huu mpya wa kimapinduzi ya kifikra haukuwapendeza sana watawala wa Ulaya, pamoja na kanisa lililokuwa linanufaika kwa moja kwa moja na mfumo. Wafalme wakaanza kuwaua watu wote wanaoonekana wana fikra tofauti kidogo.
Mfano mzuri mwanasayansi Galileo Galilee, alipokuwa anatafutwa na kanisa kwasababu aliamini tu dunia ni duara. Baada ya kuona haya yanafanyika suluhu ikawa ni kufanya mapinduzi ili kuwafanya wafalme na kanisa wawaogope na kuwaheshimu watu.
Wanafalsafa kama Rousseau , John Locke, Hegel, Marx, Engels , Voltaire na nk waliamini kwamba mapinduzi pekee ndiyo yatakayoleta mabadiliko ya kweli. Kwa bahati mbaya watu walitumia ugaidi kuwafanya wafalme wawaheshimu watu hivyo kuleta demokrasia Ulaya.
Makundi ya wanamapinduzi wenye mlengo wa kigaidi waliua wafalme wao.
Mfano mzuri Ufaransa kundi la Kigaidi la Jacobins liliua Mfalme wao Luis , Uingereza matajiri na Puritans walinyonga mfalme wao Charles na Urusi walinyonga Nicolas.
Hivyo ugaidi ulikuwepo tangu miaka ya nyuma na mlengo mkubwa ulikuwa ni kulazimisha kufanyika kwa matakwa ya kisiasa au kidini. Japo zamani ugaidi ulikuwa unafanywa na kikundi ambacho kina imani fulani, siku hizi hata mtu moja tu anweza kuwa gaidi na akafanya vitu mbali na mlengo wa kisiasa au kidini.
Anaweza kufanya kwa dhumuni la kipesa, mfano mzuri Uharamia wa meli ni moja ya ugaidi dhidi ya raia na mali zao na mara nyingine kabisa ugaidi unaweza kufanywa na taifa kubwa kama njia ya kupigana vita na adui au kupenyeza maslahi yake ya kiuchumi katika eneo fulani.SEHEMU YA TATU:
UGAIDI KIPINDI CHA VITA BARIDI MPAKA SASA 1945-2016
Baada ya Vita ya pili ya dunia mataifa ya Marekani na Urusi ya Kisovieti yaliibuka kuwa yenye nguvu sana hapa duniani hivyo kufanya dunia kugawanywa katika kambi mbili. Wakati huu dunia ilishuhudia kukua kukua kwa teknolojia, mifumo ya kisiasa, mbinu za ujasusi, mifumo ya kisheria za kimataifa, muunganiko wa chumi za dunia na uwepo wa majeshi makubwa na yenye nguvu tofauti na miaka yoyote katika historia ya mwanadamu.
Ulikuwa ni Ulimwengu ambao taifa haliwezi kujitenga na mataifa ya duniani. Kwa bahati mbaya sana kukawa na kambi mbili kubwa duniani, Kambi ya Magharibi ikiongozwa na taifa la Marekani huku Kambi ya Mashariki ikiongozwa na taifa la Urusi ya Kisovieti. Kila kambi ilikuwa inataka kutawala dunia kisiasa na kiuchumi hivyo kuanza kuleta mnyukano mkali. Marekani anataka dunia huru ya kibepari, Urusi anataka dunia yenye utawala wa pamoja na Ukomunisti.
Kabla ya mwaka 1945 nchi zikiwa na mnyukano wa kisiasa zilikuwa zinamaliza mambo kwa kutumia nguvu ya kijeshi. Lakini baada ya Einstein kutuletea laana ya Nyuklia ambapo dunia ilishudia alichofanywa Japan kwenye visiwa vya Hiroshima na Nagasaki.
Raisi wa Marekani Truman akajua kwamba njia pekee ya Kumaliza vita ni kutumia silaha nzito za maangamizi ili kummaliza adui haraka na kupunguza athari za vita upande wake: Kwasababu kama Marekani ingeamua kuwavamia wajapani kichwa kichwa wangeshinda lakini wangekufa wamarekani wengi sana.
Mwaka 1949 Urusi naye baada ya kuona atazidiwa kivita na Marekani akaamua kutengeneza Makombora ya nyuklia na kuyalipua hadharani. Ikumbukwe kwamba Marekani na Uingereza walikuwa na Mkakati wa kijeshi uitwao TOTALITY ambao Jenerali Eisenhower alipewa ausimamie.
Kwa kifupi Winston Churchill aliwashauri Wamarekani walipue Urusi na nyuklia mara moja na vita uishe na Ukomunisti uwe historia, lakini baada ya kukuta Urusi ana nyuklia basi mpango ukasitishwa. Miaka imeenda Urusi na Marekani wanajitanua sana katika nyanja ya silaha za maangamizi kama silaha za kikemikali na kibaiolojia. Magonjwa kama Ndui, tetekuwanga, Sulua na hata Malaria sugu kutengenezwa ambapo mbu wa kawaida anaongezewa vitu kisha anapandikizwa sehemu.SEHEMU YA NNE:
UGAIDI MPYA WAANZA RASMI DUNIANI
Baada ya kuona kwamba Mrusi na Marekani hawawezi kupigana vita hata siku moja kwasababu vita ya Kinyuklia ya vingewaangamiza wote basi nchini Urusi K.G.B mwaka 1967 wakaona suluhu ni UGAIDI. Ikumbukwe kwamba kabla ya ugaidi walikuwa wanapigana kwa kupitia vivuli (Proxy War) ambapo Marekani anakuwa upande moja wa nchi fulani na Urusi anakuwa upande wa pili.
Mfano Vita ya Korea mwaka 1950-1953 Marekani korea Kusini na Urusi Korea Kaskazini, Vita ya China ya 1945-1949 Urusi upande wa Wakomunisti na Marekani upande wa Mfalme wa China.
Lakini baada ya kuona vita hazizai matunda Mazuri na kuna hatari ya kupoteza wanajeshi wengi na kutupa pesa au kuweza kutokea vita baina yao wenyewe kama ilivyotokea pale CUBA mwaka 1962 baada ya Mrusi kupeleka makombora ya Kinyuklia kwenye Kisiwa cha Cuba ili kujibu mapigo ya Marekani kuweka Makombora aina ya JUPITER NA THOR nchini Uturuki kwenye mpaka wake na Urusi.
Marekani na Urusi wote wakajifikiria na kuanza kujipanga upya. Hasahasa Urusi mwaka 1967 alipoteza pesa kibao na kupata hasara na madonda makubwa baada ya Israeli kuwatwanga waarabu na kulipua silaha zote ambazo Urusi alikuwa amewapa.
Mkurugenzi mpya wa Shirika la K.G.B Yuri Andropov aliwatafuta wataalamu wagundue njia mpya ambayo itawafanya wapigane na Marekani bila kwenda wao wenyewe wala kupata hasara kubwa. Walianzisha Ugaidi wa kidini ambapo ili kuendeleza adhma yao walianza kuwasomesha vijana wakiarabu waliooneka na uwezo wa kipekee.
Wakaanzisha Chuo Cha Lumumba ambapo C.I.A wanasema ulikuwa ni mtambo wa kuzalisha magaidi na majasusi wa kikomunisti. Vijana walikuwa wanachukuliwa na wakienda mle ndani wanaaminishwa kwamba wanapigana kwa ajili ya taifa na Mungu lakini kumbe ni njama za wakomunisti kupeleka sera zao mbele. Naomba niseme wazi kabisa kwamba Uislamu siyo ugaidi lakini magaidi wengi wanatumia uislamu kuhalalisha Ugaidi.SEHEMU YA TANO:
UGAIDI WAANZA KUTUMIKA RASMI NA URUSI YA KISOVIETI
Warusi walitumia mwanya wa ugomvi baina ya Israel na nchi za Kiarabu kutengeneza magaidi japo wao walijiita ni wapigania uhuru. Wasomi wengi wa kikundi cha P.L.O kuanzia Yasser Arafat walifundishwa Urusi na kurudishwa mashariki ya kati.
Pia kuna PFPL (Popular Front For Palestinian Liberation) ambapo mbali na kupigana vita walikuwa na mbinu za kuteka ndege na kufanya uharibifu ili kuwafanya watu wa Mashariki waogope na kukubaliana na kuiacha palestina peke yake.
Moja ya magaidi hatari kabisa alikuwa anaitwa Wadie Haddad ambaye alifundishwa na K.G.B na mwaka 1970 akapewa jina la siri (Code-name) NATSIONALIST. Huyu jamaa alipenyezwa kwenye makundi ya Ukombozi ya Kipalestina na akawa na anapenyeza ajenda za Kirusi na kusambaza ugaidi. Anakumbukwa kwasababu alishawahi kuteka ndege tatu na kuzilipua.
Mchezo wa kuteka ndege ukawa ndiyo unafanywa sana na P.L.O, K.G.B na G.R.U. Mara ya mwisho PFPL wanafanya utekaji wa ndege chini ya uratibu Haddad Wadie mwaka 1970 ambapo walimtuma gaidi wa kike kutoka Iraq anayeitwa Leila Khaleed kupeleka ndege Jordan lakini kwa bahati mbaya mle ndani ya ndege kulikuwa na jasusi la Mossad hivyo kuwathibiti vilivyo wakina Leila hadi kukamatwa.
Gaidi mwingine ambaye amefanya kazi na Urusi anaitwa CARLOS THE JACKAL na kwa jina halisi ni Illych Ramirez Sanches. Huyu jamaa ni mtu wa Venezuela lakini inasemekana mwaka 1966 alipelekwa CUBA na huko akapewa mafunzo na shirika la kijasusi la CUBA (DGI) na baada ya hapo akaenda kujiunga na chuo kikuu cha Lumumba nchini Urusi mwaka 1968.
Lakini ukweli ni kwamba K.G.B ilitafuta sababu ya kumpeleka Carlos mashariki ya kati. Jamaa atakumbukwa kwa unyang'au wa kuwa fundi wa kutoroka na kujua sana kujificha. Mwaka 1975 alienda Ufaransa na majasusi wakatumwa kumkamata jamaa akawaua na kutoroka. Carlos alikuwa anatumiwa sana kufanya mauji na viongozi wa nchi mbali mbali duniani wenye mlengo wa kushoto.
Mwaka 1975 alifanya shambulio la Vienna nchini Austria ambapo viongozi wa nchi za OPEC walikutana wakiwepo mawaziri. Carlos akaingia na kuteka na kuu watu. Baada ya hapo waliteka watu kama sitini na kuwapandisha kwenye ndege na kuanza kuwazungusha nchi mbali mbali. Lakini muda wote huu Urusi ya Kisovieti alikuwa nyuma ya vivuli na akiwatumia hawa jamaa bila Marekani na wenzake kujua.
Taarifa hizi kuhusu mitandao ya kigaidi zilivuja baada ya majasusi kutoka Urusi na nchi za Warsaw Pact kuasi ni kupeleke taarifa kwamba Urusi ndiyo inahusika na magaidi hawa. Jenerali Ion Pacepa ambaye alikuwa nchini Romania na kuasi
Anasema kwamba Jenerali wa Kirusi kutoka K.G.B Alexandr Sakharovysky alisema msemo ambao nimeuweka hapo juu mwanzo wa hii habari kwamba katika dunia hii ambapo silaha za nyuklia zimefanya majeshi yakose umuhimu basi ugaidi ndiyo suluhu. Kwenye kitabu chake kinachoitwa Russian FootPrints kwamba Jenerali Alexandry ndiye aliyebuni mbinu ya kuteka na kulipua ndege.
Mbinu ya ugaidi ilifanikiwa sana kupeleka mambo ya Urusi na kambi ya kushoto mbele ambapo ilitumika vema nchini Vietnam kwenye vita ya mwaka 1965 hadi 1975 hadi kumfanya Marekani na wshirika wake kukimbia. Hochi Minh alifundishwa vizuri sana na K.G.B na hadi kuanzisha kundi linaloitwa VietCong ambao walikuwa wanapigana kwa kutumia mbinu za ugaidi.
Raia wa vietnam waliogopa sana kuwapinga kwasababu kundi lilikuwa linaua wasaliti wa aina yoyote. Jamaa walijifanya raia wa kawaida na wakulima huku wanaenda kulipua sehemu yoyote ambayo wanajeshi wa Marekani wapo hata kama kuna raia. Mwishowe wamarekani walichanganyikiwa wakaanza kuua kila mtu wanayehisi hana makosa na huo ndiyo ulikuwa ni mpango wa K.G.B.
Nchini Marekani ilionekana C.I.A wanawaua raia na kweli walikuwa wanawaua raia wasio na hatia, maandamano makubwa yalitokea na serikali pamoja najeshi la Marekani walikosa imani ya Ummah wa Wamarekani na mwishowe wakakimbia Vietnam.
 
roservelt

roservelt

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2016
Messages
1,017
Points
2,000
Age
26
roservelt

roservelt

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2016
1,017 2,000
Hakika nimejifunza mengi. Nimepata connection ya mambo niliyokua najifunza kwenye History. Pia kipindi hichoo mauaji yakutisha yalikua yanafanyika kwa sababu sheria na haki za kibinadamu zilikua hazijaratibiwa vizuri. Japokuwa ugaidi hauangalii masuala ya sheria wala nini.. Wako kwa ajili ya kutimiza matakwa yao.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,417
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,417 2,000
Western propaganda!! Yaani ugaidi umeanzishwa na urusi?? Ina maana Umeshasahau taliban walipigana dhidi ya Urusi miaka ya 70????

Alafu kwanni unaonyesha ugaidi ulikua funded kwa wakomunisti tuu hauongelei makundi hatari ya kigaidi America ya kusini yaliofadhiliwa na marekani hta Congo DRC yalikuwepo kma simba mercenaries purely funded na wamarekani ila unayapotezea ili ionekane marekani ndio masteringi
 
Password

Password

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Messages
771
Points
1,000
Age
45
Password

Password

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2011
771 1,000
Kwanza unga wa bunduki haukugunduliwa ulaya uligunduliwa "UCHINA".pia Galileo Galilei alitafutwa sio kwa kuamini dunia ni duara bali alisema jua lipo katikati ya sayari zote na sayari ndizo zinalizunguka jua(holicentric),ambapo kanisa lilifundisha kwamba dunia ndio ipo katikati ya sayari zote(geocentric). Mengine tuendelee
 
inamankusweke

inamankusweke

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2014
Messages
5,211
Points
2,000
Age
31
inamankusweke

inamankusweke

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2014
5,211 2,000
Kwanza unga wa bunduki haukugunduliwa ulaya uligunduliwa "UCHINA".pia Galileo Galilei alitafutwa sio kwa kuamini dunia ni duara bali alisema jua lipo katikati ya sayari zote na sayari ndizo zinalizunguka jua(holicentric),ambapo kanisa lilifundisha kwamba dunia ndio ipo katikati ya sayari zote(geocentric). Mengine tuendelee
kanisa likalisha watu tangopori na kuleta umwambà koko..wakalipindua
 
Password

Password

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Messages
771
Points
1,000
Age
45
Password

Password

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2011
771 1,000
kanisa likalisha watu tangopori na kuleta umwambà koko..wakalipindua
Lilishindwa kula na kipofu,lilipuuza kwamba watu washalichoka.Jamaa alikuwa anareason kitu halafu na wewe unaamua kama ni kweli au sivyo,lakini kanisa linataka likisema basi ndio uamini hakuna kuuliza,wanamsemo wao et "Roma locusta,causa finita" kwamba Roma ikisha amua ndio mwisho wa mjadala, kweli alama za nyakati zinaenda haraka sana.Juzi kati hapo papa katupiwa kopo sijui jiwe hadharani.

"WE HAIL THIS DAY"
 
Poise

Poise

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2016
Messages
7,458
Points
2,000
Poise

Poise

JF-Expert Member
Joined May 31, 2016
7,458 2,000
Poise,
Huwa naandika comment humu JF platform kuwa magaidi na vita za hapa na pale zote hutengenezwa kwa faida za watu hasa mataifa yaliyoendelea ila naona kwa Uzi huu hata walio na akili ndogo sasa watanielewa.

Hata huu urafiki wenu wa jumba jeupe na jumba la damu la Rwanda inabidi watanzania wenzentu muwe nao makini sana.

MJUKUU WA CHIFU,
Mkuu,
Uzi umekaa vizuri sana.
 
Nuhu39

Nuhu39

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2018
Messages
697
Points
1,000
Nuhu39

Nuhu39

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2018
697 1,000
Nilikuwa Nikijua Marekani anatumia ugaidi kwa kivuli cha dini sasa nimejua Urusi ndiye aliyeanza.
 
Ephan

Ephan

Member
Joined
Oct 30, 2017
Messages
27
Points
75
Ephan

Ephan

Member
Joined Oct 30, 2017
27 75
Western propaganda!! Yaani ugaidi umeanzishwa na urusi?? Ina maana Umeshasahau taliban walipigana dhidi ya Urusi miaka ya 70????

Alafu kwanni unaonyesha ugaidi ulikua funded kwa wakomunisti tuu hauongelei makundi hatari ya kigaidi America ya kusini yaliofadhiliwa na marekani hta Congo DRC yalikuwepo kma simba mercenaries purely funded na wamarekani ila unayapotezea ili ionekane marekani ndio masteringi
Hapo ndyo mtoa maada sikumuelewa anapoongelea Urusi tu ndyo founder wa ugaidi hakuongelea USA, na makundi ya kigaidi yaliyoanzishwa na Marekani yako wazi kama Al qaida
 
Poise

Poise

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2016
Messages
7,458
Points
2,000
Poise

Poise

JF-Expert Member
Joined May 31, 2016
7,458 2,000
Hapo ndyo mtoa maada sikumuelewa anapoongelea Urusi tu ndyo founder wa ugaidi hakuongelea USA, na makundi ya kigaidi yaliyoanzishwa na Marekani yako wazi kama Al qaida
Nchi zilizo endelea zote siyo Russia na USA pekee huo ni mchezo wa kawaida sana kwa nchi zilizoendelea.

Changamoto ipo katika kugundua kuwa hapa mhusika ni yupi ila hiyo ndiyo kawaida yao.
 
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
13,855
Points
2,000
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
13,855 2,000
MJUKUU WA CHIFU
Mkuu kwanini umenakili Uzi wangu: Ugaidi katika utamaduni wa binadamu bila kufanya Acknowledgement yoyote ile ???

Huu uzi utaishia kuwachanganya watu kwasababu haukuisha wote na bado mimi naendelea kuuandika!
Lakini wewe umefanya uonekane ni kama vile nazungumzia upande moja wa Warusi na Waarabu...
 

Forum statistics

Threads 1,295,954
Members 498,495
Posts 31,228,989
Top