Naiomba serikali yangu kupitia ma Afisa uhamiaji watoe elimu ya uraia katika kata zote zilizopo mipakani na nchi zingine hii iwe awamu ya kwanza, watu wengi mipakani hawana uhakika na uraia wao, hivyo naomba ma afisa uhamiaji wafanye kazi hiyo na wawajibu maswali mengi waliyonayo wananchi zoezi hilo liwe kata hadi kata, hili litasaidia kuondoa wasiwasi mwa walio wengi na wengine watafuata taratibu zinazotakiwa ili wawe raia na wawe na uhakika kuwa sasa ni raia.
Imetokea sehem mbali mbali kama Bukoba, Namanga, Mara... Mtu akiingia kwenye siasa ndipo huchomekewa na kuanza kuhojiwa ili kuujua uraia wake, elimu ipelekwe huko maana hadi sasa wapo watu ambao wanatakiwa kukana uraia wa (wa) mzazi wake, na wengine wanaogopa kuingia kwenye shughuli za jamii au kisiasa maana hawajiamini wanaona kama vile watachokoza ambayo hayakuwepo kwenye ajenda kuhusu wao wenyewe.
Nimetoa wito huu kwasababu nimeenda sehem kufanya tafiti ya biashara za mipakani ili kujua vikwazo wanavyokutana navyo tutafute namna ya kuwasaidia ili waondokane na vikwazo hivyo ili wachangamkie fursa ndani ya jumuia ya afrika mashariki, nimekutana na wengine hata kiswahili hawajui na wanasema ni watanzania ila wanaongea lugha ya nchi jirani.
Nashukuru endapo serikali yangu itanisikiliza kwa hili.