Mbii mbwane! Ni vizuri umeahidi kufundisha uraia mkoani kwako. But nijuavyo hata mikoa mingine kama Arusha wapinzani wamepata mbunge mmoja ama hamna kabisa. So ni bora hata ya sisi. Kuna mikoa mingine pia CCM hawajapata kitu kama ukienda kule Pemba, nk. Kuna mikoa mingine pia Chadama wameambulia patupu, zaidi hata ya Singida. Ndugu yangu badala ya kumsifia Tundu Lisu ni bora kufanya upembuzi yakinifu. Ninachosisitiza pia sio majimbo kwenda upinzani bali utendajiwa mbunge, awe Chama Tawala ama pinzani. Kuna wabunge Iramba naamini wanaweza wakawa wazuri kuliko hata Tundu Lisu. Kuyaamrisha mashirika ya hiari yaende Singida si hoja bora kwani pia ni kuyadhalilisha mashirika ambayo tayari yapo Singida yakitekeleza ukisemacho. Zaidi nakuhakikishia Tundu Lisu hana tija sana, subiri utaona.
teh ! teh! teh! kikwete kashinda bana ndo hivyo tena vumilia tu kaka jk ni moto chini 2010-2015
Naomba sasa tufunge mjadala huu ,majadiliano ya watu kumi na tano yanadhirisha kuwa Iramba inatatizo,tunahitaji kuikomboa bila kujali itikadi zetu.Tuendelee kupambana ! MWASONGELA SANA , KARIBUNI TUUNDE IRAMBA VISION.
Nendeni Kilimanjaro mkajifunze nini maana ya maendeleo. Watu wana maji, umeme, shule za kila namna, barabara za lami na bado wanaendelea kutafuta maendeleo kwa nguvu zote kwa kuchagua viongozi makini, huko kwenu wamebaki kushabikia t-shirt! hatari sana hii
hapo sibishi, Maendeleo ya Tanzania Kaskazini yaani mikoa ya Arusha na Moshi yametokana na juhudi ya wananchi wa maeneo hayo na wala si upendeleo wa serikali kama wengi tunavyofikiria.
Sisi tuliotoka mikoa ya kati ambayo wananchi bado wanamelala fofofo ni shughuli kubwa sana kuwaamsha.
a) Watu hawataki mabadiliko
b) Wameridhika na hali ya maisha waliyonayo.
c) Hawana uchu wa maendeleo
d) Hawajui umuhimu wa elimu
Sitaki kuitaja mikoa hii lakini ni ukweli kwamba kuna Makabila mengine kwao maendeleo ni adui, sasa kama mtu kama hataki maendeleo, hataki elimu -- ni kazi kweli kweli.
Kukubali Changamoto na kukubali Tatizo ni mwanzo mzuri wa kutatua tatizo.Nendeni Kilimanjaro mkajifunze nini maana ya maendeleo. Watu wana maji, umeme, shule za kila namna, barabara za lami na bado wanaendelea kutafuta maendeleo kwa nguvu zote kwa kuchagua viongozi makini, huko kwenu wamebaki kushabikia t-shirt! hatari sana hii