john mhagama
Member
- Jul 10, 2013
- 9
- 8
Migogoro migogoro migogoro,kuchafuana kuchafuana kuchafuana,siku za mwanzo nilipokuwa nasikia habari hizi kuwa Chadema yangu kuna migogoro na mitifuano ya ndani kwa ndani sikutaka kuruhusu moyo wangu kuyaamini haya nilijua ni maneno tu ya maadui wetu kisiasa,nikili wazi kuwa nilikuwa najidanganya sana na sasa nailaumu sana nafsi yangu kwa kutotaka kuyaamini yale,pengine ningeamini ningeweza kutoa mchango wangu wa mawazo kunusulu migogoro hii isiyo na maana yyt.
Siamini kama akili zetu leo zimeacha kutafuta wanachama wapya badala yake tunanyukana wenyewe,nafsi yangu inalia kwa uchungu kwa kuwa naona tunakokwenda ni kugumu zaidi ya tulipotoka,tulikaaa pamoja tukapanga,tukaonyana kwa hekima,tukaelekezana kwa busara,kwa umoja na mshikamano wa hali ya juu tukapiga hatua kubwa,ccm walituogopa kwa hoja nzito,tukazoa wanachama wengi waliondani na nje ya ccm,tukawafanya wasiopenda saisa wakatuunga mkono,na wengine wakamwaga damu zao kwa ajili ya hiki chama,kuna yatima kadhaa ambao baba zao wamefia chama,wapo wajane pia ambao waume zao wamefia chama,jamani naomba tujiulize kwa pamoja viongozi wetu wanawafikilia hawa kwa haya yanayoendelea?
Nimekuwa nikifuatilia kwa siku kadhaa zilizopita juu ya mgogoro wa kipuuzi kabisa aliouanzisha Mh Lema dhidi ya kiongozi wake Mh Zitto,jamani pamoja na yote yanayoendelea dhidi ya Mh Zitto ieleweke kwamba uchaguzi ndani ya chama bado hivyo Mh Zitto bado ni kiongozi wetu halali,huyu ni naibu katibu mkuu wa chama chetu,ana heshia zake na hadhi yake,hivyo siungi mkono aina yoyote ya udhalilishaji unaofanywa dhidi yake nje ya utaratibu wa kichama.
Mh Lema kwa nini kila siku ni wewe tu?hebu tuambie sasa kwa malumbano yale tumeongeza wanachama wangapi?malumbano yale yalikuwa na faida toyote kwa chama?Lema hivi ninyi nyote si mawazili vivuli ndani ya Bunge?mnaweza kweli kukaa pomoja kupanga hili na lile kwa manufaa ya taifa letu kama mawazili kivuli?Hivi leo Mh Lema unaweza kupokae maagizo yoyote ya kichama kutoka kwa naibu katibu mkuu wa chama kwa manufaa ya chama?
Ki ukweli sisi wanachama wenu tumekwazika sana na upuuzi uliouanzisha ambao hauna tija,nawasihi sana wanachama wenzangu tafakarini jambo hili kwa moyo mkuu mwone chama kinapoelekea.
Lema ulipaswa kufuata njia za kistaarabu na za kiuongozi za kurekebishana,tuna washauri wengi sana tena wenye hekima ya hali ya juu sana,Prof Baregu,Prof Safari,Dr Mkumbo mko wapi chama kinakufa hiki kutokana na vingozi wa aina ya kina Lema.
Slaa mlitumia nguvu kubwa sana kukijenga chama na naibu wako mlipokuwa pamoja bungeni inakuwaje leo husemi chochote mwenzio tena msaidizi wako anapodhalilishwa na mtu mnayemwongoza?
Mwisho naonamba nikutie moyo mkuu Mh Zitto kuwa sisi wanachama tunatambua wewe ni kiongozi wetu.
PEOPLES POWER.