Naikumbuka TRC - Wewe je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naikumbuka TRC - Wewe je?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FUSO, Aug 4, 2011.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,809
  Likes Received: 2,293
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Leo nimeikumbuka sana TRC, nimeikumbuka baada ya kusoma habari kutoka kwa wenzetu wa South Africa wamezindua Treni iendayo kwa kasi toka Johannesburg hadi Pretoria. Nikafikiria sana kuona jinsi Shirika letu tulivyoliua kwa makusudi, Reli ya kati ipo hoi bin taaban - kwa mbali nikahisi kutokwa na machozi hasa nikikumbuka enzi hizo nikiwa mwanafunzi tukisafiri kwa Warrant Collectitive ambapo Serikali yetu wakati huo chini ya Mwalimu Nyerere ilitulipia BURE!! kwenda na kurudi majumbani kwetu baada ya shule kufungwa.

  Naenda mbali zaidi nakumbuka baadhi ya vituo maarufu, kweli inasikitisha sana, kwa mlio safiri kwa Treni enzi hizo basi mtajikumbusha baadhi ya Vituo.

  Station ya Salanda: (Moshi Hotel) Kuku choma, Pilau la nguvu, mishikaki bei cheee...
  Station ya Kitinku: Kuku mishikaki...Ubuyu.
  Station ya Itigi: Igalula na Goweko i: Asali Mbichi
  Station ya Aghondi: Ubuyu na vigoda asilia
  Station ya Bahi: Ubuyu na mikeka asiliya
  Station ya TABORA: Abilia chunga mzigo wako - ukizubaa tu WAFWAAAA......
  Station ya Fela: Hapo mzee unaliona jiji Hiloo la mwanza......aka ZOO...
  Station ya Mwandiga: (Kwa Mh. Zitto): Migebuka bei cheee....
  Station ya Vigunguti to DSM ... Walete haoooooo, waleteee haooo wa kujaaaaa, walete hao wa baraaaaa.....
  Jamani zamani RAHA tupu.......

  Sasa hivi hakuna habari inayofurahisha, ni huzuni kila kukicha hasa habari za WIZI wa mali za umma ndiyo zinatamba kwa sasa, watu wanafikia hatua hata ya kulihonga Bunge: kweli SHETANI yupo kazini.
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ha ha haaa Mkuu nimeipenda sana na umenikumbusha mbali saana, enzi hizo zilipendwa.
  Pale salander...sijui zile ni kuku kweli ama? maana wengine husema ni ndege pori wasiolika waleee.
  Pale Tabora...yaani pale ilikuwa ni zaidi ya 'danger', maana kulikuwepo na kila sampuli za wezi, wakwapuzi, vichaaaaaa ndio usiseme na ndio pakaitwa 'mboka'.

  Nyongeza;
  Station ya Muscut...Pale kuna chotara wengi wa kiarabu na utajipatia mchele kwa bei cheeeee kuwapelekea zawadi nyumbani
  Station ya Malampaka...Pale utajipatia viazi vya kuchemsha vilivyochacha, karanga za kuchemsha zilizochacha, mihogo ya kuchemsha, mahindi ya kuchemsha na 'makazalika'.
   
 3. Josephine

  Josephine Verified User

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwakweli mmenikumbusha mbali sana.Watanzania jamani hamkeni tuipiganie nchi yetu 30years back we were not like this,bora enzi zile kuliko ya leo.Leo sina hata cha kuwaadithia watoto,wanatoka shule hawana kipya cha kusisimua.
   
 4. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, umekumbusha mbali sana hivi pale Salanda wale kuku mbona walikuwa wakubwa sana halafu bei raisi,
  Nakumbuka Fela wakati wa likizo tukifika pale tunanunua zawadi za ndege za mbao za kuchonga, Sungura wa mbao, Kasuku wa mbao!
   
 5. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,192
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  cha kufurahisha zaidi nishawah kusafir kutoka tabora mpaka dom nimesimama, behewa lilikuwa limejaa magunia ya mahindi utafkiri gusi.
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,809
  Likes Received: 2,293
  Trophy Points: 280
  Kipindi kile nasoma nilitamani sana nikianza kufanya kazi niweze na mimi kwenda Baffect (Restaurant), yaani Behewa la Hotel kwa wale ambao hamkupata bahati kusafiri na TRC enzi hizo ili na mimi nipate msosi safi na kinywaji. Nilitamani pia nisafiri na familia yangu siku moja kwenye 1st class wakati nakwenda kwetu likizo ili mwanangu naye afurahie madhari na uoto wa asili katika nchi yetu, hizi ndoto zangu hazipo tena kwani TREN ndugu zangu HALIPO.
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,809
  Likes Received: 2,293
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu, kuna kipindi unakosa siti unasimama then bei lako unajitwisha masaa zaidi ya nane - yaani unatoka Tabora hadi itigi na begi lako kichwani. ha ha ha

  Mkuu ulishalala chini ya Viti, hasa wakati TT anapita kukagua tiketi? kuna those times tulifanya hivyo kumkwepa TT hasa ukichelewa tarehe ya kusafiri kwa collective warrant na wanafunzi wenzako. na huna hela ya ziada. it was so fun kumwepa huyu jamaa mkusanya ushuru. Hayo yalikuwa survival wakati wa maisha ya kishule.
   
 8. Tanganyika1

  Tanganyika1 JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  ndo mana mashirika yamekufa. Unajua nyie wa zamani mmesoma bure, afya bure, usafir ndo kama hvyo mtoa mada alivyosema. Na mlipo ingia madarakani mkawa na ule mtazamo wa bure bure tu. Hamuoni tabu kujichotea, mkiuza mnauza bei sawa na bure. Yaani nyie wazee mna matatizo sana. Afu mwaanza kulalamika ooh maadili yameshuka, wakati haya yote mmesababisha nyie. We unataka kijana afanye nn ikiwa wewe ulo mtangulia una chakachua?
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,809
  Likes Received: 2,293
  Trophy Points: 280
  wote wenye miaka 40 kwenda juu walisoma bure -- hao waheshimiwa wako wote asingekuwa Nyerere wangekuwa wanalima viazi vijijini kwao: Kwanza jiulize nani alibinafisha TRC? Kasome huo mkataba wote then then uje kuchangia.

  TRC haikufa kwa sababu unazodai wewe, imekufa sababu ya tamaa mbaya na urafi wa watu na ndiyo maana tunayalilia mashirika yetu, juzi mjomba wako naye kajiuzia UDA - aibu gani hii? in short hii ndiyo product ya poor leadership ya CCM na serikali yake.
   
 10. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Fuso umenitoa pangoni...make nakumbuka enzi zile kulikuwa na mabehewa ya wanafunzi hasa nyakati tunazofunga shule...yaan wale wezi wa Tabora nao walikuwa wanayajua mabehewa ya wanafunzi.. make akikamatwa mwizi alikuwa anashughulikiwa ile mbaya...................................
  Kuhusu kwamba kwa kuwa tulisoma bure ndo maana hatuna uchungu.. ni kukosa fadhila tu na ubinafsi...mtu aliyesoma bure ndiye anatakiwa aone umuhimu wa kuwasaidia waliomsomesha...bahati mbaya sana tumeamua kuwaibia waliotusomesha...............rejea hotuba ya Mwl.Nyerere kuhusu mtu alitumwa na kijiji kwenda kuhemea......
   
 11. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Tulikuwa tunaambiwa kuku wa salanda ni kunguru
   
 12. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Buffet car kulikuwa na msosi wa nguvu.
  Ukiwa 1st class,ukutaka huduma kulikuwa na kengele unabonyeza,
  Chakula wanaweza kukuletea chumbani,
  Usiku wankuja kutandika vitanda,mashuka meupe na blanketi la bluu,
  Na kulikuwa na spika unasikiliza mziki kwa mbaliiii
   
 13. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Na wewe kizazi kipya umefilisi ATC,TANESCO NA SERIKALI YENU
   
 14. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Siwezi kusahau hizo memories, ilikuwa raha kweli, pale tabora kulikuwa kunafanyika shunting kugawa mabehewa ya kigoma na mwanza, basi unaweza ukaenda mjini ukasalimia ndugu na ukarudi kuendelea nasafari. Ukianza kuingia mwanza unaona mawe yanayoning'inia kama yanaanguka vile.
   
 15. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,773
  Likes Received: 574
  Trophy Points: 280
  Aaaah miwaaaa Aaaah miwaaa........STATION YA kILOSA , usiku miwa mitamu...........Unanikumbusha Safari yangu ndefu,,,,kutoka Bush hadi wilayani then basi then Meli (MV mapinduzi) then GOGO then BUS to MAGANZO then miguu to SHY BUSH enzi zile sitasahau....
   
Loading...