Mvumbo
JF-Expert Member
- Aug 20, 2015
- 3,485
- 12,108
Kutokana na mauaji ya kuchinjwa watu nane nje ya nyumba zao wakiwemo viongozi wa mtaa huko jijini Tanga, leo umefika msafara mzito akiwemo naibu waziri wa ulinzi, Mkuu wa Jeshi la polisi nchini pamoja na Mkuu wa Jeshi Mwamunyange.
Pia wameambatana na vikosi maalum vya jeshi vyenye silaha tayari kuhakikisha nchi yetu inakuwa katika amani tuliyoizoea.
Pia msafara huo umefika moja kwa moja nyumbani kwa wafiwa kuwapa pole pamoja na kuongea na wananchi.
Tujikumbushe; hapo juzi usiku kuna kundi la watu lilivamia Mikocheni karibu na Amboni jijini Tanga,na kuwashutumu viongozi wa mtaa kuwa wanashirikiana na polisi kufichua siri zao, kisha wakawachinja na kuvunja maduka na kuchukua unga, sukari na biskuti na kisha kuingia mapangoni.