ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Jana alisikika akitoa maagizo yanayohitaji utekelezaji . Maagizo hayo ni yale aliyo waagiza wakuu wa mikoa nchi nzima kuanzisha utaratibu wa kuwa na kliniki tembezi ili watu wa vijijini nao waweze kufurahia huduma bora za afya.
Wazo lake ni nzuri lakini kilichowashangazi wengi wanao jua taratibu ni kwamba anatoa maagizo ya kiutekelezaji kwa watu walio juu yake. Kwa utaratibu Wakuu wa mikoa siyo ranki yake ,wakuu wa mikoa wapo ranki ya mawaziri na hata mishahara yao ya mawaziri na wakuu wa mikoa haipishani sana. Manaibu mawaziri wapo ranki ya wakuu wa wilaya na hata naibu waziri akienda mikoani utaratibu unamtaka mkuu wa wilaya kumpokea na si mkuu wa mkoa. Waziri akienda mkoani sheria inamtaka mkuu wa mkoa kumpokea na kumtembeza kwenye mkoa hadi siku atakapo ondoka.
Kwa mazingira kama hayo unatoaje maagizo kwa mtu aliye juu yako ayatekeleze , yeye alipaswa kuwaagiza wakuu wa wilaya tu na si wakuu wa mikoa. Labda atuambie sheria imebadilishwa lakini mbona tunaona huku mikoani wakija mawaziri wanapokelewa na wakuu wa mikoa na wakija manaibu mawaziri wanapokelewa na ma- dc.
Huu utaratibu ukiachwa kuna siku utasikia mkuu wa mkoa anamwagiza waziri mkuu atekeleze majukumu yake. na kwa jinsi pm alivyopoa na yeye akajikuta anatekeleza maagizo ya RC , hii inaweza kuwa comed .
Viongozi wajifunze kufuata taratibu . Hiyo kauli ya naibu wa afya ilipaswa kutolewa na waziri wake na si yeye .
Kingwagala ni mtu mwenye upeo mkubwa sana kuliko hata waziri wake sasa sijajua labda ulimi uliteleza .
Zamani enzi za mwalimu mtu akiteuliwa alikuwa anaenda kozi maalumu mwezi mzima kwa ajiri ya kupewa maelekezo ya jinsi ya kufanya kazi yake . Leo mtu akiteuliwa moja kwa moja anaanza kazi , vile vyuo vimekufa , ipo haja ya kuvifufua vile vyuo.