Naibu Waziri, Kijaji: Serikali haiwezi kuondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye vifaa vya ujenzi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr Ashatu Kijaji amesema Serikali haiwezi kuondoa kodi ya VAT kwenye vifaa vya ujenzi kwa sababu ni vigumu kujua nani anajenga kibiashara na nani anajenga makazi binafsi.

Naibu Waziri ameyasema hayo leo bungeni wakati akijibu swala la mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema alilouliza "Kwa nini Serikali isiondoe kodi la ongezeko la thamani kwenye vifaa vya ujenzi".

Majibu yake yalikuwa hivi;

"Vifaa vya ujenzi hutumika kujenga miundombinu ya aina mbalimbali kiwemo nyumba binafsi na za biashara na barabara, umeme na maji. Hivyo basi kuondoa VAT kwenye vifaa vya ujenzi kama kigezo cha kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za makazi, yaweza kabisa kuwanufaisha wafanyabiashara wachache kuliko wananchi wa kawaida na pia kupunguza mapato ya Serikali na hivyo Serikali kuwa na uwezo mdogo wa kutoa huduma muhimu kwa umma"

"Bei ya vifaa vya ujenzi haipangwi kwa kupitia kodi ya VAT pekee bali hutokana na gharama mbalimbali zikiwemo za uzalishaji, malighafi na usafirishaji na msukumo wa nguvu ya soko, hivyo basi kuondoa VAT kwenye vifaa vya ujenzi si kigezo pekee kitakachopunguza gharama za ujenzi wa nyumba za makazi"
 
Useme sasa kwamba ni majibu ya kijinga kuliko kuleta ujinga huo ulioleta
 
Hoja dhaifu kwanini uondoe kodi kwenye vifaa vya ujenzi wakati makusanyo ya kodi bado yapo chini na bado hao wabunge wanataka posho na mishahara mikubwa.
Nilitegemea wabunge walete hoja ya kupunguza posho na mishahara yao.
 
Back
Top Bottom