Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
NAIBU WAZIRI KIHENZILE AIPONGEZA TCAA UIMARISHAJI ANGA
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile ametembelea na kuipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kusimamia kwa mafanikio utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoendelea kuboresha sekta ya usafiri wa anga.
Akizungumza katika ziara yake yenye lengo la kukagua miradi kwenye eneo la Lolkisale, wilayani Monduli mojawapo ya maeneo ya utekelezaji wa Mradi wa Mawasiliano ya Sauti baina ya Rubani na Muongozaji Ndege (VHF) — Kihenzile amesema TCAA imeonesha dhamira ya kweli katika kuboresha huduma za anga.
Ameongeza kuwa jambo hilo linaloongeza usalama na ufanisi katika usafirishaji wa anga.
Mradi huo wa mawasiliano kupitia mfumo wa VHF umegharimu serikali kiasi cha Sh bilioni 31.6 na unatekelezwa katika vituo vikubwa 18 na vituo visaidizi 12 kote nchini.
Kwa mujibu wa Meneja wa Mradi, Mhandisi Francis Chale, utekelezaji umefikia asilimia 90 na tayari baadhi ya vifaa vimeanza kufanya kazi katika kipindi cha majaribio.
"Mradi huu ni miongoni mwa hatua muhimu zinazolenga kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Tunaamini utasaidia kuongeza ufanisi na kupunguza changamoto zilizokuwa zikijitokeza awali," amesema Mhandisi Chale.