Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,910
- 1,340
DAVID KIHENZILE: SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA BANDARI KATIKA MAZIWA MAKUU
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza na itaendelea kuwekeza Katika Maziwa makuu kwa kuboresha Bandari, Kuendelea kukarabati Meli na Kujenga Meli Mpya.
Naibu Waziri David Mwakiposa Kihenzile amesema hayo wakati akihitimisha ziara na Kuendelea kufuatilia utendaji wa Meli za Serikali katika Ziwa Nyasa kwa kuzungumza na Viongozi wa Wilaya za Kyela - Mbeya na Ludewa - Njombe.