Naibu waziri alizwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu waziri alizwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by yeromin, Mar 11, 2012.

 1. y

  yeromin Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Aug 8, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ameibiwa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.3milioni (Hapa yupo safarini je akiwa home) katika Hoteli ya Nashera mjini hapa.

  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Hamisi Seleman alisema kwamba uchunguzi wa tukio hilo lililotokea jana alfajiri unaendelea na kwamba taarifa za awali zimeeleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichokuwa amepanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo.

  “Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni (Laptop 3 za nini kwenye safari? za nn zote hizi,). Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh milioni moja, simu tatu (hili siwezi kuuliza kwani ndio maisha yetu bongo kwa sasa), ya kwanza Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry yenye thamani ya Sh5.5 milioni,(Wadau hii ni aina gani ya blakberi, maana hata Blackbery porches sio bei hii?)” alisema kamanda huyo na kuongeza:

  “Vitu vingine ni Pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola za Marekani 4,000 ambazo ni sawa na Sh6.5milioni,(Bora wamezichukua kwann utembee na mihela yote hii tena ya Kigeni, halafu nyie ndio mnalalamika kuwa hamjui kwann thamani ya Tsh inashuka). Fedha taslimu Sh1.5 milioni (Unatembea na hela mingi hii ya nn wkt nowaday ATM mashine kibao na kadi nyingi ni VISA), kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo (alikua anahama mji nn) baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.”

  Hata hivyo, Kaimu Kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola (Fine kwa Personal defensive) na bunduki aina ya SMG (Jamaan huu mbunduki wa nn?Tanzania siku hizi kuna vita) alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu ya wazi (Sheria ya utumiaji na Utunzaji wa silaha binafsi inasemaje).

  Source: Mwananchi Newz Pepa
   
 2. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah! Mkuu we ndio umeinyaka leo hii habari!!?
   
 3. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  aisee unaishi dunia gani?
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Wewe vitu anavyobeba mtu awapo safarini vinakuhusu nini?, Ngosha alisema sh.Bln moja iliyohifadhiwa bank ya kigeni ni vijisent nyie mkamjia juu!, sasa tazama mtu aliyehudumia uwaziri kwa miaka saba anatembea na dola elf 4, analala hotel ya sh laki 4.
   
 5. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Aseee Yeromin bonge la BUREKINGI NYUUUZI.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  habari ishachacha wewe ndo unatuletea mkuu
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna nyuzi zaidi ya 20 kuhusu hayo makitu na hiyo inasiku karibia tatu sasa!! Ulikua porini nini ambapo hakuna radio wala mtandao?
   
 8. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ni ajabu saaaaaaana. inakuwaje mtu upo kwenye safari za ndani ya nchi yako unatembea na vitu vingi namnahiyo pamoja na fedha za kigeni zote hizo ili uzitumie wapi??????. Huyu naibu waziri anazuga tu ili asiumbuke, alichukua changudoa na ndo amemwibia vitu vyote hivyo.
   
 9. Mabwepande

  Mabwepande JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kalizwa na Changudoa aliye lala naye. Mwizi wa kawaida hawezi kuiba hadi pete.
   
 10. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  sijaelewa vinasa sauti vya kazi gani kwa yeye kama naibu waziri..,
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Thinking loud: naibu waziri alikuwa na masanduku mawili ya nguo, kwa hiyo alikuwa na safari ya siku nyingi. Alikuwa na laptop 3, kwahiyo alikuwa na kikosi kazi kwani mtu mmoja hawezi kutumia laptop 3. Alikuwa na SMG-hili siamini kama kuna raia anaruhusiwa kumiliki SMG, hata hivyo inaoneshakuwa huenda alikuwa na safari ya kutembelea maeneo hatarishi kama vile kwenye mbuga za wanyama ama alitaka kwenda maeneo yenye vita kama east Congo etc na ndiyo maana alikuwa na us dolari za kutosha. Natumai iko siku serikali itatoa maelezo juu ya mh waziri kuwa na vitu vini namna hii.
   
 12. y

  yeromin Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: Aug 8, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Umejuaje kaka..utakua na undugu na marehemu shehe Yahaya
   
Loading...