Naibu Meya Arusha `atekwa’ Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Meya Arusha `atekwa’ Chadema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  JOTO la kisiasa mkoani Arusha limezidi kupanda kiasi cha kumlazimu Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Michael Kivuyo wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) aliyechaguliwa na madiwani wote wa CCM, kutangaza kujiuzulu.

  Sababu kubwa aliyoitoa wakati anatangaza uamuzi huo ni kwamba, hawezi kuendelea kuwa kiongozi wa cheo hicho wakati damu ikimwagika kwa ajili ya cheo hicho.

  Kivuyo alichukua uamuzi huo mbele ya Kamati ya Utendaji ya TLP Mkoa wa Arusha na Wilaya katika kikao kilichofanyika katika Shule ya Msingi Mkombozi iliyopo Kata ya Sokoni One, ndani ya Jiji la Arusha.

  Mara baada ya kutangaza uamuzi huo, Kivuyo ambaye ni Diwani wa TLP kwa miaka mingi, alisema sasa ataungana na Chadema katika kuombeleza msiba na pia kuwajulia hali watu waliojeruhiwa katika maandamano ya kudai kurudiwa kwa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

  Alisema TLP imesikitishwa na hali iliyojitokeza Arusha, Jiji lenye hadhi ya kimataifa kwa Jeshi la Polisi kuchukua uamuzi wa mabavu kupita kiasi na kutumia risasi za moto kuua na kuwajeruhi watu wasiokuwa na hatia.

  Alieleza kuwa, alishiriki katika uchaguzi aliouita uliopindishwa sheria na kanuni za uchaguzi na yeye kuchaguliwa kuwa Naibu Meya, lakini kwa hali iliyojitokeza hawezi kuendelea kuwa na cheo hicho kwani yeye ni moja ya sababu yaliyotokea mpaka sasa ikiwa ni pamoja na watu kuuawa na kujeruhiwa na Polisi.

  “Siwezi kuwa Naibu Meya wakati damu inamwagika na siwezi kuona sheria na kanuni inachakachuliwa na mimi nang’ang’ania madaraka, hilo kwangu haliwezi kuingia akilini,’’ alisema.

  Katika uchaguzi uliomweka madarakani Kivuyo, huku madiwani wa Chadema wakidaiwa kususia, Gaudence Lyimo wa CCM alishinda nafasi ya umeya.

  Akizungumza jana, Mwenyekiti wa TLP Mkoa wa Arusha, Leonard Makanzu yeye alisema wanawaunga mkono wenzao wa Chadema katika wakati huu wa majonzi ya watu kuuawa na kujeruhiwa kwani hali hiyo si ya kufurahiwa kama watu wanavyoropoka ovyo.

  Makanzu alisema yeye kama kiongozi wa Mkoa wa Arusha alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha wanapaswa kuwajibika kwa hilo bila pingamizi.

  Alisema na kusisitiza kuwa kitendo cha Polisi mkoani Arusha kumwaga damu za watu wakati wanadai haki yao ya msingi, ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote bila ya woga.

  Mwenyekiti huyo alisema TLP itakuwa bega kwa bega na Chadema katika kila kamati ili kuona wale wote waliokufa na kujeruhiwa katika vurugu hizo wanapata huduma zote za msingi bila ya kujali chochote.
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  safi sana naibu meya hyo ni demokrasia
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hii habari inakuwa recycled sasa mara ya 5...!
  Hivi hamsomi majukwaa ndipo mbandike ?
   
Loading...