Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu ameunganishwa kwenye orodha ya Viongozi wa CHADEMA wanaohusishwa katika mpango wa kuhamia CCM.
Tangu Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole atoe angalizo kwa wana-CHADEMA wanaotaka kuhamia CCM kufanya hivyo kabla ya mwishoni mwa Disemba 2018, ni Wabunge watatu pekee katika orodha ya Wabunge 15 walikuwa wakitajwa kutaka kuhamia CCM.
Katika hao wanaotajwa, wote ni Wabunge tu lakini ni John Mnyika pekee mwenye wadhifa mkubwa wa utendaji ndani ya CHADEMA, pamoja na Saed Kubenea, hivyo kuhusishwa kwa Salum Mwalimu kunaongeza zaidi shinikizo kwa Chama hicho.