Nahodha: Wanaobeza Muungano watimuliwe CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahodha: Wanaobeza Muungano watimuliwe CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Sep 30, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][​IMG][/h] Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha
  Written by Ghalib // 30/09/2012 // Habari // 19 Comments


  Na Mwinyi Sadallah

  30th September 2012
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha amesema viongozi wanaokejeli na kubeza Muungano hawastahili kuendelea kubaki ndani ya chama tawala na serikali zake.
  Nahodha alitamka hayo wakati akifungua mkutano wa uchaguzi wa viongozi wanaogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ujumbe wa halmashuri Kuu ya Taifa ya CCM NEC wilaya Dimani mjini Unguja jana.
  Alisema kimantiki viongozi wanaodiriki na kuthubutu kusimama hadharani bila aibu wakipinga Muungano uliopo amewafananisha na watu waliokosa utu na shukrani.
  “Wanaopita na kusema Muungano haufai hata kufika kwao mahali walipo wakipata hadhi na heshima ni kutokana na nguvu za CCM na serikali zake,” alisema Nahodha.
  Aliwafananisha watu hao na wasaliti wanaotoboa jahazi wanamosafiria huku wakiwa kwenye kina kikubwa cha bahari.
  Nahodha ambaye ni Waziri Kiongozi mstaafu wa SMZ alisema yuko tayari kupoteza marafiki kwa na kubaki kuwa mtetezi na muumini wa Muunagno wa serikali mbili.
  “Sitajutia kupoteza marafiki wanafiki katika mambo ya msingi yanayogusa umoja wa kitaifa, potelea mbali liwalo na liwe,” alisema Nahodha.
  Akizungumza na kuufanya ukumbi kukaa kimya, Nahodha aliwataka viongozi wenye fikra mbadala kupitisha mawazo yao kwenye vikao vya kikatiba na wakishindwa watoke kama hawakubaliani na misimamo ya kisera ya chama hicho.
  Alisema siri ya Muungano huo chini ya waasisi wake hayati Baba wa Taifa na Sheikh Abeid Karume ni dhahiri walizingatia na kuweka mbele maslahi ya umoja kwa kupinga utengano.
  Akizungumzia umuhimu wa kuwachagua viongozi bora kwa miaka mingine mitano ijayo wanachama wenzake kuchagua wenye sifa za uadilifu, uaminifu na majasiri katika kutii sera za chama na kuheshimu katiba yao.
  “Huu si wakati wa kuchagua viongozi kwa pupa na papara, chagueni kwa umakini, msichague viongozi mamluki wanaojibadili rangi zao kuliko kinyonga na kuhatarisha uhai wa chama chetu,” alisema Nahodha.
  Kauli hiyo ya Nahodha imekuja huku baadhi ya makada na viongozi wa juu wa CCM Zanzibar wakipigania kuwepo kwa Muungano wa mkataba agenda ambayo pia inapigiwa upatu na Jumuiya ya kidini ya Uamsho visiwani humu.
  Hata hiyo viongozi hao wamekumbana na upinzani mkali toka kwa waaasisi wa Mapindzi na Muungano ambao wanapinga vikali wazo la Muungano wa mkataba wakiamini mpango huo umebeba ajenda ya siri ya kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI  [h=4]Related Posts[/h][h=3]Wizi Bahari ya Hindi[/h]
  [h=3]MOTO WALETA MAAFA MAKUBWA TUMBE- KISIWANI PEMBA[/h]
  [h=3]UCHANGIAJI WA WALEMAVU ZANZIBAR[/h]


  [h=3]makampuni ya simu Zanzibar yawahadaa wateja[/h]
  [h=3]VUAI ALI VUAI: NJE YA MUUNGANO HAKUNA ZANZIBAR, KUNA UNGUJA NA PEMBA[/h]

  [h=3]19 Comments on "Nahodha: Wanaobeza Muungano watimuliwe CCM"[/h]


  1. Abaazanzibar 30/09/2012 kwa 8:55 mu · Ingia kujibu
   Fupa ilo Nahodha limemtamukia. Anadiriki hata kutusaliti wazanzibari wenzake na dini yake kwa maslahi yake binafsi akitegemea kuupata Urais wa Zanzibar lakini inshallah thuma inshallah Allah amdidimize kama alivyomdidimiza Kaaruni na mali zake. Huyu ni msalini na mpiga debe wa sera za kikanisa za Tanganyika inshallah Allah hatompa nguvu za kutumaliza na kuza visiwa vyetu vitukufu.
   Watu kama Nahodha ni hatari kwa mustakbali wa visiwa vyetu na dini yetu, yuko tayari kutuangamiza sote kwa maslahi yake ya kupata cheo cha Urais. Nlikuwa namuangalia kwenye semina ya Mzee moyo jisnsi mzee moyo alivyokuwa akimfajamisha na nafsi yake naamini ilikuwa inamsuta ila Wazanzibari tusivunjike moyo na watu kama hawa kwani Allah ameshawapiga muhuri wa usaliti ndani ya moyo wake.
   Allah ibariki zanzibar Allah wabariki wazanzibari
   Na naona muandishi kaamuwa kuwapigia debe kwa speed zote ( nahodha, Vuai na Seif Iddi) Kiasi kwamba kila habari ya sadallah huwa inawazungumza watu hawa.
   Naomba jambo muhimu tuzidi kuwazinduwa wazanzibari wajielewe then automatic hawa watu watakosa support ya kutosha ya wazanzibar na watapotea kwenye siasa.
   • zinjibar.asli 30/09/2012 kwa 3:16 um · Ingia kujibu
    Uko wapi ndugu yangu msemaji mkuu umpe maneno yake huyu baradhuli mwengine anoitwa Nahodha??
    Sijui ni nahodha wa jahazi ya mabaradhuli wenzake au vipi all I know he is one stupid guy hana hata personality, qualities or confidence ya kuongea mbele ya watu wenye akili zao according to the comments & questions alomuuliza mzee NASSOR MOYO juzi katika seminar inayoendelea.
    As I said its the only time nimemuona huyu mpumbavu akiongea and I wondered hivo kweli huyu jamaa ndio aliwahi kua waziri Kiongozi wa nchi yetu Zanzibar? ama huu ni msiba mkubwa kwa nchi yetu.
    WE REALLY NEED CHANGE & MAJOR RESHUFFLE UKISHAVUNJIKA HUO MUUNGANO.
    Mimi nawambia huyu Nahodha, Vuai Ali na wenzao wote walongangania Muungano wamskilize Mzee Nassor Moyo na Mheshimiwa Mansour Y Himid itawatosha kujua kua huu muunganoi hauna maana yoyote kwa ZANZIBAR.
    MUNGU IKOMBOE NCHI YETU KUTOKA HUU MUUNGANO PAMOJA MADHALIM KAMA HAWA KINA NAHODHA NA VUAI  2. Foum 30/09/2012 kwa 9:00 mu · Ingia kujibu
   Hahahaha..Naona babu wa makunduchi anapagawa kidogo kidogo. Hakuna haja ya kujibishana na mtu kama huyu, na abakie na imani yake na sie wengine tubakie na imani yetu. Ila naona na yeye pia anapayukwa, kama anahoja ya kuwafukuza walio na msimamo tafauti na wake basi njia rahisi kama alivyosema mwenyewe huko vikaoni akaseme sio barabarani, asitishe watu wazima. Kinachompa uhuru yeye nini wa kusema hadharani wasiokubaliana naye wafukuzwe na kuwanyima wengine uhuru wa kutokubaliana na mfumo wa muungano hadharani. kwani chama nacho si kina vikao vyake, basi na aende akazungumze huko vikaoni si walishasema mukitupokonya kadi hakuna neno sasa mnashindwa nini?
   Your days are numbered vibaraka na vitimba kwiri. Zanzibar ilikuwepo, itakuwepo na itaendelea kuwepo mukipenda musipenda, na huu mfumo butu utarekebishwa tu kukidhi mahitaji ya wananchi, mukipenda musipende.
  3. buhanan 30/09/2012 kwa 9:41 mu · Ingia kujibu
   Uraibu wa uongozi umekulevya kweli kweli lkn ujue tu unamwisho wake .Chukuwa kipande kidogo hicho .WAJIDAI UNAHODHA KUSAFIRIYA UBAO.
   BARA ZOTE UMEZISHA HUJUI IPI WENDAYO.
   ULIMWENGU WATELEZA WANGAPI WAANGUKAO.
   Tuacheni tupumuwe ,laana za alla ziwe juu yenu, shamsa vuai nahodha na wenzako wote.
  4. sale 30/09/2012 kwa 10:01 mu · Ingia kujibu
   Kila linapotokea jambo ndio hujidhihirisha ukubwa wa mwenyezi Mungu, sasa huyu angalipewa uraisi wakati ule sijui ingekuwaje ya Rabi salama,,kumbe wewe ni mnafik mkubwa, hao marafiki zako walikuamini wewe kwa sababu za kiurafik na kwa si lolote, kumbe wewe ulikua nao kwa ajili ya msimamo mbaya wa nchi yao na urithi wa watoto zao? Basi leo wamekusikia saa nyengine bora ya huyu mpuuzi raisi Sheni kila siku huzungumza” SIMUOGOPI MTU, HAKUNA MTU WAKUNITISHA,,,,LAHAJA LAHAJA” hana alifanyalo,,laiti ingekuwa miaka miwili tu zaidi, basi Amani Karume angekwisha yamalza mambo na mafuta yetu tushachimba
  5. Salem 30/09/2012 kwa 10:06 mu · Ingia kujibu
   Sasa huyu mwinyi sadala kwanini lazima habari zake aweke uongo kidogo
   ni mwasisi yupi wa mapinduzi na muungano aliepinga muungano wa mkataba? Nassor moyo au
  6. pambanua 30/09/2012 kwa 10:09 mu · Ingia kujibu
   nahoza anasema hapo walipofika ni kutokana na nguvu za ccm na serikali zake
   kashamsahau hata Muumba mtwana uyu, yeye anaona ccm inampa nguvu tu na si chengine,,,Subhaana LLah,,ama kweli shibe yalevya,,,,uyu mjinga huyu alikuwa aliuza maji tu kwenye madumu M/Mungu akamuonea huruma Karume akampa uwaziri leo anasema ccm na nguvu zake ndizo zilizompa hadhi,,,,,itaondoka iyo ccm tuone atabaki na hadhi uyu?
   sadala amerudi huyu wananchi mumemuona?
  7. elbattawy 30/09/2012 kwa 10:34 mu · Ingia kujibu
   Nahodha ni mnafiki na msaliti na Inshaalah Mungu hatompa hatua kufikia hayo malengo yake binafsi ili wazanzibari kudhalilika.
  8. fey 30/09/2012 kwa 10:35 mu · Ingia kujibu
   Nahoda imekua hadi hao rafiki zako kina Amani walokupa madaraka, wamekua mahasimu zako? Innalillahi wainna illaihi rajiun, naona dua za muamsho zishaanza kukupata. Kibaraka cha waTanganyika wewe, huna uchungu wa nchi yetu na waZanzibari na ndio wewe unetuletea jeshi kufanya fujo misikitini na Ktk majumba ya viongozi wetu wa dini, lakini inshallah Mwenyezi Mungu yupo na jicho lake halifumbi yote hayo anayaona ni siku moja tu na wewe anakuteremshia jeshi lake sijui utajihami vipi?
  9. NKARAFUU 30/09/2012 kwa 11:29 mu · Ingia kujibu
   NDUGU ZANGU Msipate taabu na watu kama hawa hata kidogo, HAYA NI MATOKEO YA DUA ZA WAZANZIBARI WALIOWENGI ALLAH anazikubali. nimekua nikisema kila siku kwamba Mungu anawafichua wanafiki wa wazanzibar kokote waliko na kuwatoa hadharani. ANGALIA NAHODHA NI MTOTO MDOGO SANA KATIKA SIASA ZA ZANZIBAR NA TANZANIA,lakini Mungu amemleta juu na kupayuka,kuadhirika,kufedheheka hadharani na kuwaonyesha wazanzibari usaliti alionao na unafiki na dharau kwa wenziwe. KUNA CCM KINDAKINDAKI ZANZIBAR TENA WAZAWA NA WAUMINI WA ZURI WA CHAMA CHAO LAKINI KWA HALI WAIONAYO na wao wenyewe wanavyojiheshimu na kuwaheshimu wenzao zanzibar,basi huamua kukaa kimya na si kupayuka kama huyu kijana aliepewa fupa juzi,maskini kasahau utu wake na uzalendo wake.
   NIAMBIENI NI CCM GANI AU MTANZANIA GANI atakaemsikiliza nahodha katika siasa za zanzibar? huyu ni mtoto sana sana katika siasa.MNAKUMBUKA HUYU ALIKWENDA MPAKA MUSOMA KWA MKE WANYERERE KUOMBA APEWE URAIS? wasomeni watu na vijana chipukizi kama hawa wasiokuwa na elimu ya nyakati wala elimu ya kuwaongoza katika maisha.yeye alipokwishafika kesharidhika kama anavyosema yuko tayarikupoteza marafiki (ndugu zake) wa kizanzibari lakini TONGE ALIONAYO isimtoke….lahaula!!!! huku ni kupotoka kwa mwisho. Mungu waone watu kama hawa na wenye nia mbaya na watoto,vizazi,wanawake na wazee waliodhulumiwa wa kizanzibari.
   NDUGU ZANZU WATAJITOKEZA WENGI WENGINE KAMA HAWA na historia iatakuja kuwahukumu….subra tu.MAANA KAMA UNAAMINI MSIMAMO TAFAUTI NA WENZIWO KAMA UNAELIMU YA KUTOSHA BASI UTABAKIA NA BUSARA YA KUSUBIRI NA HASA KAMA WEWE SIO MSEMAJI AU MWENYE DHAMANA YA KUTOA KAULI,kwanini usikae kimya kwa usalama wako? lakini kupayuka huku ni udhaifu mkubwa unaouonesha mbele ya jamii.
   HAYA MUNGU ATAITIZAMA ZANZIBAR KWA JICHO LA HURUMA,,REHMA NA AMANI. NA ATANDELEA KUWAFICHUA KOKOTE WALIKO WANAFIKI WA NCHI HII….AMIN AMIN AMIN
  10. Ghalib 30/09/2012 kwa 11:31 mu · Ingia kujibu
   Madaraka mabaya sana,Nahoza amekosa sifaa hata ya kugombania urais kabisaa hata ule usheha hafai kabisa, huwezi kuiyuza nchi yako kisiasa bwana,Ajifunze scottland.
  11. santorini 30/09/2012 kwa 11:42 mu · Ingia kujibu
   Shamsi ni mtu mapepe,wazungu wanasema (a person who has no confidence) na waarabu wanasema( galil hayaa mustareh) wakimaanisha kwamba mkosefu wa haya hustarehe.
   Anaongoza wizara isiyo ya muungano wala hajui yeye yumo tu.
   zanzibar tunayo yetu ya jeshi la kujenga uchumi bara jeshi la kujenga taifa ,ama kweli amelewa madaraka.
   sasa atasema kila kitu lakini majuto mjukuu huja mwishoni,akiwa mkereketwa atamshinda amani karume ? wakati karume anaweka utaifa kwanza? na ndie aliemtoa tongo tena tongo mzito za upofu hasa.
   Sawa nahodha tunakusubiri ngamani chukulubumbu.
  12. santorini 30/09/2012 kwa 12:19 um · Ingia kujibu
   Shamsi umeshaadhirika,akufaaye kwa dhiki ndie rafiki ,kwa hivyo uko tayari kuwapoteza marafiki waliokuondoa katika dhiki?Historia inakuandika na panapo uhai na majaaliwa tutakukumbusha maneno yako haya ,usije ukatutolea tafsiri nyengine,kama potelea mbali liwalo naliwe, kae huji kuwa na rafiki utabaki kama ngombe aso pembe kwa maneno ya waswahili,
   Chunga mdomo wako japo huulipii kodi lakini maneno mazuri hunukia uzuri nawe sasa unatoa maneno yenye harufu mbaya,utakimbiwa kwani utakuwa ukinukia vibaya.mti na macho
  13. NKARAFUU 30/09/2012 kwa 12:46 um · Ingia kujibu Santorini
   Huyu hayatambui hayo uliomwambia keshanogewa na fupa kijana kwa hio hajui siku ya kurudi kae huyo…mwache historia itamkumbusha. MDOMO UMEMPONZA KIJANA nakusahau yote yaliopita. mwambie amuulize mwenziwe Mapuri aliekua na tamaa hizohizo na akija kifua mbele.lakini lahaula!!!
  14. Elbattawi 30/09/2012 kwa 2:02 um · Ingia kujibu
   WANAMAPINDUZI waliyobaki hai ukimuondoa Hassan Nassor Moyo, labda ni Hamid Ameir, mtu wa Donge na sijawahi kumsikia kusema lolote katika suala hili la Muungano.
   Hassan Nassor Moyo, ambaye ametangaaza wazi wazi msimamo wake kuwa yeye ni muumini asieyumba wa Muungano wa Mkataba, na hayo ndio maoni yake.
   Labda Mwinyi Sadallah, anaposema waasisi wa Mapinduzi na Muungano, anakusudia kina Vuai Ali Vuai, Ali Mohamed Ameir, Shamis Vuai Nahodha, Ali Juma Shamuhuna, Samia Hassan Suluhu, Dk Gharib Mohamed Bilal na kadhalika ambao wengine licha ya Muungano hata Mapinduzi hawayajui.
   Hassan Nassor Moyo, alisema Ali Mohamed Ameir hakuwahi wala hajawahi kuwa member wa Baraza la Mapinduzi, lakini akasema Hamid Ameir kweli ni member wa Baraza la Mapinduzi.
   Hapa inaonekana Mwinyi Sadallah, amebeba ajenda rasmi ya kutaka kuwapotosha watu kwamba kuna waasisi wa Mapinduzi wanapinga kuwepo kwa Muungano wa Mkataba, jambo ambalo ni uongo.
   Hamid Ameir, lini na wapi katoa kauli (maoni) yake kuhusu suala la Muungano tangu kuanzishwa kwa mjadala wa mabadiliko yanayodaiwa na Wazanzibari, juu ya aina ya Muungano wanaoutaka? Mwinyi Sadallah…twambie..
  15. Foum 30/09/2012 kwa 4:09 um · Ingia kujibu
   Sababu za wahafidhina wapendao muungano ni kama sifuatazo:-
   a) Kurejeshwa kwa waarabu – Shamte wa Kisonge
   b) Kufukuzwa kwa wazanzibari bara na kuporwa mali zao – Borafya wa Kisonge
   c) Bila ya Muungano hakuna Zanzibar – Mheshimiwa Vuai (NK)
   d) Wanaoujadili hadharani muungano wamekosa fadhila – Mhe Nahodha
   e) Kupinduliwa kwa serikali – Nahodha
   f) Ni urithi wa Mwalim Nyerere – Nape Nauye (NKU)
   Nukuu za wasioutaka mfumo wa sasa:-
   a) Rais wa Zanzibar kukosa status yake kamili – Amani Karume
   b) Mfumo ulioanzishwa bila ya ridhaa la BLM na kuipokonya hadhi ya nchi – Mzee Moyo
   c) Mfumo unaotifanya kuwa ombaomba na usio na heshima – Mansour Himid (W)
   d)mfumo usio na upeo wa maendeleo ya kiuchumi zanzibar – Yusuf Mzee (WF)
   e) Mfumo unaoinyima Zanzbar uwezo wa kufunga mikataba ya maendeleo – Hassan (MBLW)
   f) Miaka 20 tume zimeundwa za kuondosha kero bila ya maridhio ya bara – Raza (MBLW)
   e) Kama wewe Nyerere mimi Karume mdogo – Dr Salmin Juma
   Wananchi uwanja mweupe huo, angalia hoja za wanaoutaka mfumo wa sasa butu na wenye kutaka mabadiliko ya msingi.
   Sema Ndio kwa Muungano wa Mkataba.
  16. chidi 30/09/2012 kwa 4:17 um · Ingia kujibu
   Salaaam…..i
   Chama chochote cha siasa hujivunaa kuwa na wanachama zaidi. CCM imekuwa na wanachama wengi hata wapo tayari kuwafukuza waanzilishi wa chama hicho.
   Maoni yangu mimi watu
   Wale waliokuwa hawatakiwi CCM wasije kuingia akili wakadai au kurejesha chama chao ASP – CCM Zanzibar watajuta majuto ya mjukuu.
   ASP na CUF waingie baraza la wawakilishi CCM watatia akili.
   Vuai fikiria tena……… Ulimi usije ukakuponza. Ikiwa watu hawakutakeni basi hamna namna, seriikali mtaitema tuu
   Wasalaaaaam
  17. Stonetown (Kiongozi) 30/09/2012 kwa 4:54 um · Ingia kujibu
   We march and fight, to death or on to victory. Our might is right, no traitors shall prevail
  18. makame silima 30/09/2012 kwa 6:20 um · Ingia kujibu
   Inna Lillah wa Inna Ilayhi Raji’un Ama kweli njaa ina mitehani yake, huyu jamaa anasema yuko tayari kuhasimiana na ndugu Zake wa damu wa Kizanzibar kwakuisaliti Zanzibar kwa utapia mloo tu, dooo hatari hii ilotufika Wazanzibar.
   Huyu jamaa amshukuru sana Mh Amani Karume kumpa chart ya kumpa uwaziri kiongozi lakini imekuwa kumpe ni wrong choice kwa Wazanzibar katika maslahi ya Zanzibar hatma ya kizazi chake.
   Tatizo la watu kama huyu Nahoda wako wengi na hutetea Muungano wa Zanzibar na ilokuwa Tanganyika kwa kigezo kimoja tu, wengi hutowa sababu za kuiuza Zanzibar eti tu , kwa kuwa wemeweka vitega uchumi vyao Bara vya biashara na Kujenga nyuma.
   Jee Wazanzibar tuko tayari kuza nchi yetu na utaifa wetu kwa jili tu ya kuwa na Nyumba,biashara na machamba Bara?.
   Wako watu kama huyu Nahodha wenye matamanio yao Binafsi tayari wana agenda ya kuikokota Zanzibar kwenye mfumo wa Serekali 1 ambayo kwa njia hii au nyengine Tayari Watanganyika wana itumia Sera hio ya kuifanya Zanzibar powerless.
   Hivi sasa na mabadiliko yote ya Katiba ya Zanzibar yaliofanyiwa Marekebisho kuwa Zanzibar ni nchi na mipaka yake yote lakini wenzetu baado wanatubinya kimataifa kutokuwa na voice Zanzibar .
   Yani wanatuchinja majini bila damu kujitokeza hata damu ikijitokeza maiti tayari inaelea imechakata roho.
   Wenzetu wa Tanganyika wanafanya kila wawezavyo nafasi zote za kimataifa ziwe katika mikono yao ili kuiuwa na kuimaliza Zanzibar punzi yake ya Mwicho kupumua, hivi sasa ma mabadiliko yote tuliofanya lakini kimataifa Zanzibar haijulikani nchi ni Tanganyika ilovaa koti la Tanzania.
   Na ukitaka kujuwa hivyo nikuwa mifano iko mingi tu yakutoa ya Zanzibar kuto kutendewa haki kama vile sio nchi ilio ungana na mwenzake, Wazanzibar wenye kulinda Muungano na wasio taka Muungano wa mkataba kuwa Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili ,basi wana agenda wao ya kuiteketeza Zanzibar kwa kuitowa kwa Mlango wa Nyuma.
   Zanzibar ni mali ya Wazanzibar wote na swala likiwa Zido warudishiwe Wazanzibar wenyewe waamue hatma ya nchi yao sio watu walojikubalicha kuiuza Zanzibar kwa maslahi yao binafsi hii sio mali urisi peke yao ni ya wazanzibar wote.
   Tayari kuna viongozi wako tayari kubeba zima Mbele ya Allah na wameshajisahau kuwa leo wapo baadae maiti, wasisahau tu kuwa duwa ya wazulumiwa na Adhabu yenye kumiza alio itaja Allah.
   Wenyesifa na Fahari na kujinasibu leo hatukonao kwa hio safari ipo wakati wowote na M/mungu hatokuliza amali ya kuwekeza Tanganyika kuwa una machamba,biashara na Nyumba a/c yako ni amali njema mbele ya Allah.
   Hivi sasa umri unakimbia kwa haraka ukifika miaka 30 basi tayari unaanza kuiona Chumbe ile kwa misukosuko ya dunia kwa hio kila ukila vizuri na marazi ya kila aina yanakutambalia nusu ya viongozi wetu niwabavu kwa Bresha,sukari na marazi mengine muda muda wa kutanabahi ndio huu.
   M/mungu ibariki Zanzibar na watu wake ishaallah na utulinde na maduwi waliotuzungumka na njama zao chafu.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nahodha amelewa madaraka. Waachwe watu wajichagulie muungano wanaotaka
   
Loading...