Nahodha wa Timu ya Taifa Afrika Kusini Auawa

Nahodha wa Timu ya Taifa Afrika Kusini Auawa

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,493
Reaction score
18,387
Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi. Jeshi la Polisi la nchi hiyo limesema.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya taifa katika mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya Afrika.

Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika Kusini.
Katika maelezo yake Jeshi la Polisi la afrika kusini limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.

R. I. P Senzo Meyiwa.


Supersport
 
Yaonyesha huko miguu ya kuku kama karanga, mtu akiingia tu kwenye laini yako, unampa 'say hallo to my little friends'.
 
Hamba kahle Senzo. Namhlanje wena. Kusasa mina
 
Dah!! inahuzunisha sana kwa kijana mdogo kama yule bwana kukatishwa uhai ghafla hivyo...
 
Yan SA inabidi ukienda kwa mpenzi uvae bullet proof kabisa
 
Dah!! inahuzunisha sana kwa kijana mdogo kama yule bwana kukatishwa uhai ghafla hivyo...

yah inahuzunisha sana, mbaya zaidi alicheza mechi iliyo pita na alikuwa captain wa timu zote, taifa na Orlando P
 
Back
Top Bottom