Nahodha timu ya taifa kukaa benchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahodha timu ya taifa kukaa benchi

Discussion in 'Sports' started by Manyanza, Jan 30, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nimeandika hii thread baada kuangalia mechi ya jana usiku katiya Barcelona na Hercules... kuna mchezaji anaitwa javier Mascherano huyu ni nahodha wa timu ya taifa ya Argentina aliyehamia barcelona akitokea liverpool msimu uliopita kwa madai ya shinikizo la mkewe wake ambaye ni mhispania aliyekua akisema kwamba maisha ya Uingereza hayafurahii kutokana na hali ya hewa ya baridi kali, ndio ikawa sababu kuu ya Mascherano kuhama club ya Liverpool ambapo alikuwa ana namba ya uhakika kikosi cha kwanza na alikuwa anonekana ni kiungo mzuri ambaye kazi yake ilikuwa ni kuharibu mipango ya timu pinzani... na ilifika wakati kocha wa Argentina wakati huo Diego Maradona alisema kwamba yeye mchezaji anayemkubali katika first eleven ni huyu jamaa....... sasa tatizo ambalo lipo sasa ni kwa huyu jamaa kuwekwa benchi kula siku na kocha Pep Guardiola na mbaya zaidi kilichokera mechi ya jana ni kuingiza vichipukizi visivyo na jina akimwacha mascherano nje... je wana JF ambao ni wapenzi wa soka mnalizungumziaje hili la Kapteni wa timu ya taifa kuwekwa bechi katika club yake???....
   
 2. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Barca ni chanzo cha masuper star walio wengi na pia ni tim yenye masuper star wakati wote kuliko timu yoyote duniani. Majina hayachezi wanaocheza ni watu, hatupo uingereza hapa ambapo asipo kuwepo drogba ujue anaumwa, hivyo kocha anajitahid kutumia vipaji vyote alivyonavyo. Wangekuwa hawashindi ningesema sawa. Hadi sasa amecheza mechi 15 mfululizo bila kufungwa na pia kacheza mechi 28 mfululizo bila kufungwa msimu huu. Mwache kocha apange kikosi usilinganishe hapa bongo na uingereza ambapo mashabiki wanaweza kushawishi kocha ampange mtu hata kama uwezo wake mdogo hasa kwa wakati husika. Barca fun.
   
Loading...