Nahodha MV Spice Islanders kortini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,868
30,334
Nahodha Msaidizi wa meli ya MV. Spice Islanders iliyozama katika eneo la Nungwe, Zanzibar, Jumamosi iliyopita, Abdallah Mohammed Ali (30), amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya uzembe na kusababisha vifo vya watu 203.

Nahodha huyo alifikishwa mahakamani pamoja na maafisa wawili, akiwemo anayesimamia usalama wa abiria katika bandari ya Malindi,Yussuf Suleiman Issa na afisa anayesimamia usalama wa abiria na mizigo kutoka Mamlaka wa Usafiri Baharini (ZMZ), Simai Nyange Simai.
Nyange (27), mkazi wa Mkele na Yussuf Suleiman (47), mkazi wa Kikwajuni, wote hawakutakiwa kujibu mashtaka dhidi yao. Washitakiwa hao

walisomewa mashitaka katika Mahakama ya Mkoa ya Vuga, mbele ya Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, George Joseph Kazi.
Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Ramadhan Nasib, alisema washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa
hilo kinyume na kifungu cha 236, sheria namba 6 ya mwaka 2004.

“Siku ya Septemba 9 mwaka huu, majira ya saa 3:30 za usiku, huko katika Bandari ya Malindi Zanzibar, wote kwa pamoja mliruhusu kuingiza abiria na mizigo zaidi ya uwezo na kusababisha meli kushindwa kuendelea na safari yake na kuzama katika bahari ya Nungwi,” alidai mwendesha mashtaka huyo.

Alieleza kuwa, meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba na kuzama katika mkondo wa Nungwi, baada ya washitakiwa kupakia abiria na mizigo kupita kiwango, kitendo ambacho ni cha uzembe na kusababisha vifo vya watu 203 waliokuwemo ndani ya meli hiyo.
Hata hivyo, alidai kuwa upelelezi wakesi hiyo bado haujakamlika na kuiomba mahakama isiwape dhamana washitakiwa kwa sababu za kiusalama

kwa kuwa wananchi walioguswa na vifo hivyo wana hasira za kuondokewa na ndugu zao.
“Napinga dhamana kwa sasa kwa sababu ya maslahi ya washitakiwa wenyewe kwanza, ili wapate utulivu na wananchi walioathiriwa na ndugu zao waweze kupoa joto lao wasijewakawadhuru,” alidai.

Hata hivyo, wakili anaewatetea washitakiwa hao, Hamid Bwezeleni, alidai kuwa hakubaliani na ombi la upande wa mashtaka, kwa kile alichodai kuwa kuendelea kuwaweka rumande wateja wake ni kuwapa adhabu kabla ya mahakama kutoa hukumu. Alidai kuwa usalama wa wateja wake kuwa nje watakuwa salama zaidi kuliko kuwepo rumande kwa sababu hawajui ni wapi wataweza kukimbia pindi wakikutana na waathirika wa ajali hiyo wakiwa rumande.

“Nahisi usalama unakuwepo nje zaidi kuliko ndani kwani hujui pa kukimbilia pindi ukikutwa na tatizo, na pia wakati wanakamatwa si walikuwa nje, mbona hawakupata madhara yeyote?” alihoji.
Aidha, Bwezeleni, alidai kuwa dhamana ni haki ya mshitakiwa na kuiomba mahakama kuwapatia dhamana wateja wake. Mrajisi wa mahakama hiyo, George, alisema kwamba pamoja na dhamana kuwa haki ya mshitakiwa, lakini hutegemea na uzito wa shitaka kama alivyoeleza awali mwendesha mashtaka katika kesi hiyo.

Alisema suala la dhamana atalitolea uamuzi kesi hiyo itakapotajwa tena Septemba 19, mwaka huu, lakini aliwataka washitakiwa hao kutojibu mashitaka dhidi yao hadi kesi hiyo itakapopangiwa jaji na kuanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Mshitakiwa mwengine ni nahodha wa meli hiyo, Said Abdallah Kinyanyite, ambaye alisomewa shitaka hilo bila kuwepo mahakamani.

Meli ya MV Spice Islanders ilizama katika mkondo wa Nungwi na kuua watu 203 na 619 kusalimika, baada ya meli hiyo kupinduka na kuzama ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 600 pamoja na tani 425 za mzigo. Wazamiaji kutoka Afrika Kusini wameshindwa kuiopoa meli hiyo kutokana na kuzama katika kina kirefu cha maji mita 400 kutoka usawa wa bahari, wakati vifaa vyao vikiwa na uwezo wa kuzamia mita 54 tu.

UOPOAJI WASITISWA RASMI

Serikali ya Zanzibar imesema kuwa zoezi la uopoaji wa miili ya watu waliozama katika ajali ya meli ya MV. Spices Islanders limesitishwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema zoezi la kufatilia meli iliyozama limekuwa gumu katika mkondo wa Nungwi.
Alisema taarifa za awali walizopokea meli hiyo imezama katika mkondo wa bahari wenye urefu wa kina kati ya 300 mpaka 400 wakati uwezo wa wataalamu hao huzamia mita 54.

Alisema kwa msingi huo, kama wataalamu wameshindwa meli hiyo itakuwa ndio kaburi kama kuna watu walibakia kabla ya meli hiyo kuzama kina kirefu baharini.
“Itakuwa ndio kaburi lao kama wataalamu wameshindwa kufikia meli hiyo na kuangalia kama kuna watu waliobakia,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

 

Freema Agyeman

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
3,653
3,460
Nahodha wa meli ana umri wa miaka 30, afisa anayesimamia usalama wa abiria na mizigo kutoka Mamlaka wa Usafiri Baharini ana umri wa miaka 27.

Mwajiri wao pia ashtakiwe.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,868
30,334
Nahodha wa meli ana umri wa miaka 30, afisa anayesimamia usalama wa abiria na mizigo kutoka Mamlaka wa Usafiri Baharini ana umri wa miaka 27.

Mwajiri wao pia ashtakiwe.
pamoja na yote hayo uliyoyasema Mwajiri hana makosa wenye Makosa ni wafanyakazi wake. Mwajiri hakuwaruhusu wapakie kupita kiasi. waliohusika ni hao Serikali ilio wafungulia mashtaka.
 

Freema Agyeman

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
3,653
3,460
pamoja na yote hayo uliyoyasema Mwajiri hana makosa wenye Makosa ni wafanyakazi wake. Mwajiri hakuwaruhusu wapakie kupita kiasi. waliohusika ni hao serikali ilio wafungulia mashtaka.

okay kabla hatujaendelea, je waweza kujua sifa na uzoefu wa hawa washtakiwa katika kazi hii?
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,868
30,334
okay kabla hatujaendelea, je waweza kujua sifa na uzoefu wa hawa washtakiwa katika kazi hii?
Pamoja na yote hayo unayosema , wanazo sifa ndio maana walipewa chombo kukiongoza yaani hiyo meli na inaonyesha wanafanya kazi muda mrefu na huo waliofanya ni uzeembe wa tamaa ya fedha ndio uliosababisha kutokea ajali kubwa namna hiyo. Na mimi Pia nailaumu Serikali iwe ya

Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Seriakali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushindwa kuwaokoa Maiti zilizobakia ndani ya meli kwa kisingizio kuwa kina Cha Maji ya Bahari ni kirefu. Inakuwaje seriakali yetu iwalete wazamiaji wenye uwezo wa kuzamia mita 54? wakati hapo ni baharini pana zaidi ya Mita 400

kwenda chini?Huo ni Uzembe wa Viongozi wetu kuwaleta wazamiaji wasiokuwa na uzoefu wa kuzamia Baharini.Wahusika wanalichukuliaje hili suala kama ni mchezo tu? tumeondokea na ndugu zetu wengin ingawa seriakli inasema Waliokufa ni 203 kuna zaidi ya hao Watu waliotajwa na Serikali. Seriakli imewaleta Wazamiaji wa mita54 kwani hapo ilipozama Meli ni kwenye Ziwa au mtoni? Huo ni uzembe wa hali ya juu Viongozi wa Serikali yetu walioufanya.
 

lasix

JF-Expert Member
Mar 13, 2011
441
219
hainiingii akilini eti waliobakia kwenye meli ndo kaburi lao,nna hasira sana na hii nchi.watu wamepotelewa na ndugu kibao wasione hata maiti?this is quite unfair,halaf hawakuwasiliana na hao wazamiaji kabla hawajaja kuwaeleza mahali ilipozamia meli kina chake kikoje?hii nchi jamani
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,289
16,231
hawa manahodha wanashtakiwa kwa ajli gani?
.1.kama ni mimi nawashtaki sumatra kwa kosa la kutokagua kwa muda mrefu vyombo vyoote vya majini nji kavu anga hadi bodaboda
mpaka ajali zitokee,mandege km precission yanavuja why wanaruhusu zitumikee?,mabasi yana chases za fuso matairi vipara na matatizo chungu nzima kwanini wakop kimya,hayo majahazi na mameli ni makuu-kuu na yamezeeka kuliko vasco da gama yule wa ukweli?
2.ningewashtaki sumatra kwa rushwa sababu hayo mavyombo wanayakagua na wanajua kabisa si sahihi wala salama kwa matumizi ya binadamu lakini bado yapo njiani kama si rushwa ni nnini?
hawa mabaharia manahodha ,wanasaka mshiko kwenye life ngumu ya uongozi magamba sasa unapewa limeli libovu ufanyaje.unahangaika nalo mradi mkono uende kinywani kwani wao pia wanajua hilo takataka muda wowote litaondoa uhai wake nahodha na abiria!!!!!!!!!!!!
 

njumu za kosovo

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
902
1,635
Nilijiuliza leo hili suala baada ya kunifika baharini hivi nahodha mkuu capt kinyanyite hakuonekana tena?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom