Nahitaji ushauri kutoka kwa Wazoefu

... na ambaye atakupenda kwa vipindi vyote.

Ulianza vizuri ila hapa mwishoni umeboronga. Utampata wapi katika wakati huu atakayekupenda katika vipindi vyote?

Mnajiwekea mategemeo makubwa halafu mambo yakiwa kinyume mnabaki na maumivu. Pata mwanamke mwenye vigezo ulivyojiwekea lakini haya ya eti sijui kupendwa vipindi vyote hayako realistic na huna uwezo nayo.

Focus on things that you can control. That's where your power is....

Ukifulia utaachwa tu!
 
Vijana sikuhizi mnatafuta wanawake Kwa kigezo cha pesa?

Tafuta mwanamke atakayekuwa mama mzuri kwa wanao na ambaye atakupenda kwa vipindi vyote.
Simple and clear mengine yata ji sort tu
 
Nashauri endelea kujitafuta.....usioe mfanyakazi mtakuja pigana risasi.oa mwanamke unaweza kumtawala...pesa na mafanikio yapo ila amani ya moyo ni muhimu sana
 
Hata tukushauri vipi leo, kumpata huyo mwanamke unafikir ni rahis kama unavyodhani ?
 
Kila aliyefulia ameachwa?

the easiest answer is no.

Mpenzi mstahimilivu ni muhimu saana. Sikuzungumuzia kuishiwa pesa tu...kuna ups and downs nyingi kwenye maisha..Kuna siku utampiga tukio kama sio mvumilivu umekwisha..

Wanawake wapo/wanaume wapo watakao kupenda kwa nyakati zozote..mimi ni mmoja wao. Naamini kuna maelfu kama mimi.
 
ACHA ujinga mkuu!

Tafuta mwanamke wa kukuzalia WATOTO na kukulelea familia Bas!!

Usitafute wa kusaidiana nae MAISHA utakuja lia na kusaga meno!

Tanya biashara,jenga nyumba vuta Binti mrembo mzalishe alee familia!tena asijue hata unapataje mali zako yaani awepo tu kama house girl mwenye hadhi ya kupandwa na Boss na kuhudumiwa!!!

Ukimweka kazini utampa connection hela itamkaa ataanza kuimarika KIUCHUMI bila we kujua Mwisho wa siku majibu na dharau utaanza na Mwisho mtaachana kwa mgao wa mali kwamba nae alikua anafanya biashara eti mmechangia mali!!
 
....wanaume wapo watakao kupenda kwa nyakati zozote..mimi ni mmoja wao.

Men! We will always be men!

Always hunting! πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈπŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈ
 
Vijana sikuhizi mnatafuta wanawake Kwa kigezo cha pesa?

Tafuta mwanamke atakayekuwa mama mzuri kwa wanao na ambaye atakupenda kwa vipindi vyote.
SAFI SANA
 
Sasa unatafutaje kitu usichokijua, yaani watu wakushauri ujue unahitaji nini au sio? Hata wewe mwanaume hujui utakacho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…