Nahitaji ufafanuzi kuhusu ITV kutorusha live mkutano mkuu wa CCM

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576
Nimeona orodha ya vituo vya televisheni vitakavyorusha live mkutano mkuu wa CCM kutoka Dodoma, vituo hivyo ni TBC1, Clouds Tv, ZBC, Star Tv na Azam.

Katika orodha hii sijaona ITV, swali langu ni hili, Je, vituo hivi hurusha shughuli hizi bure au vinalipwa? Kama ni bure kwanini ITV wasituletee uhondo kama kawaida yao? kama vinalipwa kwanini CCM wasingeilipa Super Brand ili tupate uhondo? nadhani ITV nao wangekuwa hewani tukio lingenoga zaidi.
 
Watanzania television yetu ni ITV na sio tbccm wala nyinginezo, wataangalia wenyewe
 
Mimi kwangu tbc na clouds nilizifta baada ya kuona hawapo kwaajili ya watanzania bali wapo kwaajili ya viongozi wa ccm tu.
 
Inaonekana CCm hawaipendi ITV kwani ina anika kila kitu wazi bila kufichaficha. Super Brand ni kiboko yao.
 
Superbrand inafanya biashara ni sio vitu vya bure ccm walipe ela
 
Nape na mengi maji na mafuta

Kumfanya Nape awe msemaji wa CCM kuta licost CCM. Akiachiwa atoe mawazo yake kwenye uteuzi ataweza kumpendekeza Membe au Kigwangala aingie ikulu na hii itatupa ushindi wa bwelelelee. M4C oyee, Bavita oyee, madaraka kaskazini oyee.
 
Kwani Lowassa anakatwa kwa ukasikazini wake au Ufisadi wake
 
Back
Top Bottom