Nahitaji tairi mpya za gari yangu Escudo

Nahitaji tairi mpya za gari yangu Escudo

mcharewamwika

Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
10
Reaction score
1
Ndugu zangu wana JF naomba ushauri,

Nahitaji kununua tairi mpya za gari yangu aina ya Escudo; size (215/75R15) kuna ambazo zimeishaa lakini kwa kweli hazikunitendea haki kabisa yaani hizi sio tairi ni uchafu (Ling Long).

Sina uwezo wa kununua hizi brand za bei kubwa kwa sasa ila naomba kujua kati ya hizi za china ni zipi zenye afadhali.
 
Dah......basi tena......nilitaka nikushauri lakini ushapiga stop........za China sizifahamu sana........
 
Sasa braza mali ya m30 unataka funga tairi za mchina? Kweli tunatofautiana, chukua bridgestone moja inauzwa Tsh 420,000 kwa bei ya mwanza. Kwani wewe kwako bei kubwa inaanzia ngapi?

Ukitaka kizuri sharti ukilee acha kufunga tairi za Ling Long bana
 
Kama unaona za China zinatesa. Tafuta brand ya Apollo ya India nazo zina afadhali kubwa sana.
 
Kwa usalama wa maisha yako na gari tairi nzuri ni BFGoodrich zinatengezwa USA!
 
Ndugu zangu wana JF naomba ushauri, nahitaji kununua tairi mpya za gari yangu aina ya Escudo;size (215/75R15) kuna ambazo zimeisha lkn kwa kweli hazikunitendea haki kabisa yaani hizi sio tairi ni uchafu (Ling Long); sina uwezo wa kununua hizi brand za bei kubwa kwa sasa ila naomba kujua kati ya hizi za china ni zipi zenye afadhali

Mkuu nunua jetking za india hizo ziko poa sanaa
 
nunua apollo ya india au good ride hzo ztakufaa mkuu unatumia mwaka na miezi 5
 
Back
Top Bottom