Nahitaji support kwenye Tech entrepreneurship

abdulqadirj

JF-Expert Member
Jan 8, 2021
1,020
3,207
Habari za wakati huu JF Members.

Dhumuni la thread hii ni kutafuta partners wa kushirikiana nao Kuunda team kudevelop ideas na kuzibadili ideas hzo kuwa ajira kwetu na kwa vijana wenzetu.

Nimekuwa nikiwasoma baadhi ya wajasiriamali waliofanikiwa katika ujasiriamali teknolojia, Namna walivyohustle kufika walipo, trials and errors, Attitude zao, passion na ethuasism walizokuwa nazo. Hawakuwa watu wa kukata tamaa, sio waoga kujaribu na kupresent wanavyofikiri, waliinvest much time kwenye fikra walizokuwa nazo na namna zitakavyobadilika, kusaidia jamii na kuwa hela.

Kupitia wao nimeona kuna kitu sisi wengine pia tunaweza kufanya na attitude yangu ipo kwenye entrepreneurship kama mkombozi mkuu kimaisha .Nimeshafikiria ideas tofauti till now, nimeshajaribu kufuatilia na kushiriki startup challenges tofauti japo sijafanikiwa hata moja ila sijawahi kukata tamaa, Nishaandikia watu business proporsals zaidi ya moja japo hazikuwahi kuwa implemented kwa sababu watu nliwaendea hawakuwa watu sahihi.

Naamini wapo wengi zaidi yangu mimi humu ambao wanainvest much time on thinking about tech na entrepreneurship so nahisi itakuwa jambo jema kama nitapata team ya wazalendo kadhaa ambao tunaweza kukaa chini na kuunganisha tulivyonavyo ili tuweze kufikia malengo, pia kama kuna mtu atataka kuinvest kwenye ideas zetu asisite kusupport.

Mifano ya Successful Technology entrepreneurs kutoka Tz.

1)Andron Mendes

Huyu ni Mtanzania mwenye miaka 37, Aliuza kampuni ya Kopa gas kwa kampuni moja ya waingereza inayoitwa Circle gas kwa Tsh Bilion 57.4 mwaka 2018. Jamaa alishawahi kupresent Ideas 17 mara ya kwanza kwenye startup challenge uturuki but those had failed ila hakukata tamaa aliendelea kuamini ipo siku atakuja kutoboa kupitia mawazo yake tu. Aliacha kazi TRA kuukataa utumwa wa ajira, akashiriki idea searching challenge kadhaa mpaka hapo alipokuja kufanikiwa kuwa miongoni mwa nominees i think ni Denmark then akaenda kupitch his idea i nfront of the judges na kufanikiwa kushinda, idea ilikuwa inahusu usambazaji wa umeme vijijini nchini Tanzania. akapata almost 500 mil Tsh ambazo alikuja akafanya hiyo project ila haikufanikiwa kama walivyotegemea, then second chance aliyokuja kuipata ndiyo hiyo ya kopa gas akatoboa mazima.

2022-11-13 22.04.05.png

2) Eng. Juma Rajabu.
Huyu ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya maxcom limited, wamiliki wa maxmalipo . yeye pia alihustle kudevelop ideas tofauti but at the end ikafanikiwa hiyo ya maxmalipo, Kampuni yake ilishakuwa moja ya kampuni zilizoongoza kwenye mobile transaction.
2022-11-13 22.04.37.png

Na wengine kama akina Benjamin Fernandes mmiliki wa Nala money, Sameer Hirji mmililiki wa selcom na Maxence Mello.

Mifano ya successfull technology entrepreneur worldwide.

1). Elon Musk.

Wengi mnamfahamu Bilionea huyu mwenye degree ya uchumi na physics, Aliacha kusoma PHD ya physics kwa sababu ya ujasiriamali. moja ya mambo aliyoyafanya kwenye technology ni pamoja na kuanzisha system ya Zip2 1995 na kuiuza 1999 kwa dollar million 341, Pesa alizopata akaenda anzisha x.com ambayo ndani yake ikazaa paypal akaja uza 1.5 Billion usd, then alianzisha Tesla, Space x na solarcity.
kuna kipindi kabla hajawa famous sana nilisoma kitabu chake kimoja nimesahau jina jamaa alielezea kiundani kuhusu investmnt kwenye clean energy especially solar energy.

2022-11-13 22.48.14.png

2).Alexander Wang.
Huyu ni youngest self made Billionnaire akiwa na miaka 25 anamiliki utajiri wa zaidi ya 1 Billion Usd. anamiliki kampuni ya Scale AI inayodeal na mambo ya artificial inteligence. Alifeli MIT kabla ya kuanzisha kampuni yake.

2022-11-13 23.46.56.png

BAADHI YA IDEAS NINAZOFANYIA KAZI.

1) Pay as you use water meters.
[/B][/B][/B][/B][/B]
Hizi ni meter za maji ambazo zitakuwa kama Luku. Hapa nafikiria namna ya kudevelop water meters ambazo zitakuwa zinafanya kazi sawa na luku ambapo maji yatakatikana pale utakapolipia, na utaweka voucher pindi utakapohitaji maji, njia hii itapunguza malalamiko yatokanayo na madhaifu ya meters za sasa, pia yataongeza utumizi mzuri wa rasilimali maji.

2022-11-14 00.23.07.png

2) Pay as you use kwa gas ya kupikia.

Hii project tayari ishaanza kufanyika kuna kampuni inaitwa kopa gas aliyouza Mr. Andron Mendes na nyingine mpya inaitwa M-gas but efficiency zao sio kubwa kwa sababu mpaka sasa ina miaka zaidi ya mitatu lakini bado hazijafanikiwa kufikia watu wengi so nafikiri namna ya kudevelop through their weekness. na kuna investors wengi duniani wana hela za kutosha wao wanasubiri ideas how they can get profit through their investment.

2022-11-14 00.20.53.png

3)Soko Mtandao.
Hapa itakuwa ni center ya biashara Zote nchini kwa maana tutapunguza madhaifu yaliyo kwenye masoko mengine kama kupatana na zoom. tutapunguza Ugumu wa upatikanaji bidhaa, uhakika wa bidhaa na mteja, kupunguza scams wa mitandaoni.

2022-11-14 00.17.52.png

4) Smart Bill Payment.
App itakayodeal na monitoring, controlling and Payments of Bills and other transactions kama Malipo ya serikali, Malipo ya mikopo, Lipia bidhaa, Fines and Fees, Bank services, Bima na Huduma za simu. But App hii itakuwa based kwenye controlling and monitoring ya Huduma muhimu zitolewazo na serikali kama Huduma za maji, huduma za umeme, Huduma za afya na bima. Itamwezesha mtumiaji kuweKa records za transactions alizofanya, kujua matumizi na gharama anazotumia kwenye huduma hiyo kwa siku, mwezi na mwaka. Kurahisisha malipo ya huduma na kuweza kuingiza vouchers alipo.

2022-11-14 00.19.17.png

Note: Nipo hapa kusikiliza kutoka kwenu mawazo, Ushauri na maoni, nasubiri mniongezee maarifa na naamini hapa kuna wajuzi zaidi, ASANTENI.

[/B][/B][/B][/B]
 
Hongera.. Kitu cha kwanza kukushauri ni kujiunga na moja ya tech hubs kama Sahara,Buni au yoyote Ile ambayo itakufaa zaidi utaongezewa maarifa yatakayo kuongoza kufungua na kusimamia kampuni yako..

Pili nakushauri kutafuta mwanasheria atakayesimamia mikataba yako(kuepuka kunywa na kuibiwa idea zako)...

Kitu cha Tatu nakushauri usianike idea yako kama hujaisajili wapo watu wanaenda kwenye hizo boot camps specific kwaajili ya kuiba idea za wanaochipukia so kuwa makini..

All the best..
 
bro Amigoh sorry naomba hii coment yako uihamishie huku Nahitaji support kwenye Tech entrepreneurship. hii thread niliikosea.
 
Amigoh bro i need your comment here kule nimefuta ile thread
Hongera.. Kitu cha kwanza kukushauri ni kujiunga na moja ya tech hubs kama Sahara,Buni au yoyote Ile ambayo itakufaa zaidi utaongezewa maarifa yatakayo kuongoza kufungua na kusimamia kampuni yako..

Pili nakushauri kutafuta mwanasheria atakayesimamia mikataba yako(kuepuka kunywa na kuibiwa idea zako)...

Kitu cha Tatu nakushauri usianike idea yako kama hujaisajili wapo watu wanaenda kwenye hizo boot camps specific kwaajili ya kuiba idea za wanaochipukia so kuwa makini..

All the best..
 
Story yako ya kupambana na startups haitofautiani na yangu. Hasa hapa Bongo kwenye Ecosystem wanaowezeshwa ni walewale. Ukifanikiea kupata co-partner kutoka nje itakuwa poa sana kama wakenya wanavyofanya. Kila la Kheri.
 
shukrani mkuu nilikuwa nasubiri hii coment yako hapa, nakuahidi kuyafanyia kazi yote uliyonishauri hapa kuanzia sasa, nitakupa mrejesho nitakapofikia mkuu.
 
Story yako ya kupambana na startups haitofautiani na yangu. Hasa hapa Bongo kwenye Ecosystem wanaowezeshwa ni walewale. Ukifanikiea kupata co-partner kutoka nje itakuwa poa sana kama wakenya wanavyofanya. Kila la Kheri.
pole sana mkuu, mazingira yetu watanzania si supportive kwa startups entrepreneurs na wengi huishia kukata tamaa ingali wana mawazo makubwa vichwani mwao, muhimu tusikate tamaa na kuendelea kuamini ipo siku utafika unapostahili.
 
Safi sana,tunataka kuona watu wenye ideas kama zako mkifanikiwa kwa wingi...
Siyo kila siku tunawaona wakata mauno na ndiyo wanapewa milage za kutosha

Ova
Nimefurahi sana kiongozi kwa support yako, naamini tutafanikiwa kupitia support za wadau wakubwa kama wewe, Asante.
 
Ahsante kwa historia! Ukiwa na wazo lako, hao unaosema hawakuwa wabia sahihi ni ulitegemea watakupa mtaji au nini? Sina uhakika, ila sijui kama umewajaribu hawa mabilionea wa Tz, kama wangependa kuwekeza kwenye nyanja zako?
 
Nice and innovative idea. Ila mimi binafsi natamani nichangie kidogo mkuu. Mafanikio mazuri ni kuweza kugusa asilimia kubwa ya watu. Nchi yako watu wengi wako kwenye hali ya chini. Wenye uwezo ni wachache sana.

Sasa kwa kila unachobuni...jaribu kufikiria jinsi gani itamfaidisha na yule mtu wa chini ili utupate wote. Hizi tech ni nzuri kweli. Lakin je zitatugusa sisi wenye hali zetu huku?? Maana naona zingne hapa zinahitaji mtu uwe na bundle za kutosha, sijui simu yenye internet and all the like. Sijajua mawazo yako but maybe try looking in that way too. Be blessed
 
Back
Top Bottom