Nahitaji nyumba ya kusimamia ujenzi

chapati mbili na chai

Senior Member
Joined
Jun 1, 2026
Posts
100
Reaction score
190
Nina uzoefu na kufanya kazi kwenye ujenzi kama Kuna mtu anataka mtu wa kusimamia ujenzi wa nyumba yake Niko hapa
 
unaomba kazi ya kusimamia ujenzi au chaka la kuiba cement, nondo na mchanga?
Sawa naomba kazi ya kujaza hata kifusi, au utasema nitaiba kifusi
Kwenye huo Uzi Kuna ubaya gani
 
Sijui kama unatania au upo serious,either way kama umeamua kufanya hiyo kazi hakikisha hata siku moja usije ukaungana na mafundi au engineer kumuibia aliyekupa kazi-kwa namna hiyo utafika mbali.
Nina mfano wa mtu moja anafanya kazi kama hizo za kusimamia ujenzi wa nyumba kwa niaba-jamaa hupo strictl sana na amejenga uaminifu mkubwa sasa hivi ninavuokueleza amisha simamia ujenzi wa nyumba za mawaziri zaidi ya 5.

Yeye binafsi kupitia kazi hiyo amejenga nyumba yake nzuri sana na ana familia na biashara yake.

Alimusimamia jamaa yangu nyumba aliokoa zaidi ya 7M,na baada ya nyumba kukamilika jamaa alilipwa 800K sio ya kusema yeye but jamaa aliamua kumpa.
Kwenye hiyo kazi uaminifu ndio msingi mkuu.
 
Boss kusimamia ujenzi sio kazi ndogo maana lazima uwe na Wewe unajua hata ufundi kidogo kwa sababu lazima fundi akusikilize wewe ila sio Fundi umsikilize. Mafundi wengi baadhi ya kazi uzikimbia kwa kukwepa muda, sasa wewe ukiwa mzimamizi lazima ushauri kitu bora kwa boss ili kazi iwe nzuri.

Unatakiwa kuwa makini kuanzia kwenye msingi mpaka finishing.
 
Unaweza kuokoa milioni 7.ila je nyumba itakuwa kwenye ubora ?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…