Nahitaji Mwanasheria mbobezi ( Personal Lawyer)

nguzo1

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
349
535
Wakuu Salama?

Nakutana na changamoto mbalimbali katika maisha na huwa inafikia mahali natamani kuwa na Mwanasheria wa kudumu ili awe ananishauri kwa ukaribu sana kuhusu mambo mbalimbali.

Awe amefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali kwenye taaluma yake na awe na uelewa mpana kwenye fani hiyo.

Asiweke maslahi (fedha) mbele kwa kila jambo nitakalomshirikisha kwani ningependa awe karibu na mimi na familia yangu kwa ujumla na ningependa awe msaada mkubwa kwa familia yangu hata nitakapokuwa siko hapa duniani.

Kuhusu mimi ni kijana raia wa Tanzania na bado nina strugle kuboresha maisha yangu na familia yangu na kwa sasa nipo Dar es salaam.

Kwa yeyote atakayekuwa interested na badiko langu na kama atakuwa tayari naomba tuwasiliane kupitia PM.

Nilipanga kwenda kwenye hizi Law firm ila naona sitompata atakaenielewa kwa haraka ndio sababu ilionifanya nije hapa jf.

Nawasilisha
 
Kama unakabiriwa na kosa pendwa la uhujumu uchumi na utakatishaji Pesa usijisumbue kabisa yaani.
 
Kama unakabiriwa na kosa pendwa la uhujumu uchumi na utakatishaji Pesa usijisumbue kabisa yaani.
Hapana ndugu sijafikia huko nataka niweke tahadhari tu na pia kutatua changamoto za hapa na pale za kimaisha.

Asante kwa angalizo.
 
Sifa za mwanasheria unayemtaka anazo Tundu Lissu tu. Mfuate Brussels, Ubelgiji.
Hahah TAL nadhani ana mambo mengi kwa sasa so sintoweza kumsumbua mara kwa mara kuhusu ishue zangu but nashkuru kwa mchango wako.
 
Hapana ndugu sijafikia huko nataka niweke tahadhari tu na pia kutatua changamoto za hapa na pale za kimaisha.

Asante kwa angalizo.
Upo sahihi nilichokuwa natahadharisha hapo ni kuwa kesi kama Uhujumu uchumi na kutakatisha pesa ni kesi zenye maelekezo maalumu kuwa mtuhumiwa asichomoke hata kama umekodi wanasheria kutoka ulaya
 
Safi sana mkuu huu ni utaratibu unatumika san na familia zenye kipato huko mambele

Sisi waswahili kitu inaitwa loyality kidgo imetupita pemben kwa sabab tuna level kubwa ya ubinafs

Ila nisikukatishe tamaa pambana utamtapata
 
"Loyality" hichi ndiyo kitu kikubwa kilichonisukuma kuja Public na ndiyo maana nimeomba asiwe mtu wa kutanguliza maslahi mbele ili awe bega kwa bega na mimi/familia hata kwenye kipindi kigumu.

Yupo jamaa yangu alipata tatizo kazini kwake akatafuta mwanasheria na baada ya mazungumzo hapohapo huyo mwanasheria akampa jamaa yangu bili ya 450,000/= kwa ajili ya kuandaa sijui form za nini ili kesi iende mahakamani na aligoma kabisa kufanya process yoyote bila hela cash.

Jamaa akaenda kwa mwanasheria mwingine na akamtatulia tatizo lake ndani ya siku mbili kumbe ishu ilikuwa ni ndogo tu kwenye mikataba na wala haikupaswa kwenda mahakamani.

Sasa kumbe yule wa kwanza alikuwa anatengeneza mlolongo mrefu ili achume hela kiulaini bila kujali mteja wake alikuwa ni kijana mdogo tu anaetafuta maisha so hapo hakuna uaminifu.

Kwa upande wangu mimi familia yangu ina kipato cha kawaida sana ila naamini nitapata Mwanasheria mzuri wa kudumu. Nikishampata nitaanza mchakato wa kumtafuta Daktari wangu (Familly doctor).

Lazima uwe makini wapo wanasheria wa hovyo kama ilivyo kwa police,wanakula huku na kule,vilevile kujenga mazigira kesi iendelee kuwepo ili anufaike.Hizi tabia ndo wanasheria wakibongo wanazo!kitu ambacho anajua kabisa hakiwezekani atakwambia kinawezekana ili achume pesa zako tu.f....em
 
Mkuu unataka mwanasheria,mshauri nani?Maana kama unahitaji mwanasheria basi lazima ujue majukumu yake ni yepi na ofcourse pesa .Kitahusika.Kwa msaada nicheck PM au nipigie 0710323060 naweza kukupa mwongozo kuhusu hicho unachokitaka maana wengi wana kitaka ila hawajui jinsi ya kukikipata
 
We muhaya unamatatizo mengi Sana, matatizo na changamoto unazipata wapi wakati damu yako ina rangi ya kijani.
 
"Loyality" hichi ndiyo kitu kikubwa kilichonisukuma kuja Public na ndiyo maana nimeomba asiwe mtu wa kutanguliza maslahi mbele ili awe bega kwa bega na mimi/familia hata kwenye kipindi kigumu.

Yupo jamaa yangu alipata tatizo kazini kwake akatafuta mwanasheria na baada ya mazungumzo hapohapo huyo mwanasheria akampa jamaa yangu bili ya 450,000/= kwa ajili ya kuandaa sijui form za nini ili kesi iende mahakamani na aligoma kabisa kufanya process yoyote bila hela cash.

Jamaa akaenda kwa mwanasheria mwingine na akamtatulia tatizo lake ndani ya siku mbili kumbe ishu ilikuwa ni ndogo tu kwenye mikataba na wala haikupaswa kwenda mahakamani.

Sasa kumbe yule wa kwanza alikuwa anatengeneza mlolongo mrefu ili achume hela kiulaini bila kujali mteja wake alikuwa ni kijana mdogo tu anaetafuta maisha so hapo hakuna uaminifu.

Kwa upande wangu mimi familia yangu ina kipato cha kawaida sana ila naamini nitapata Mwanasheria mzuri wa kudumu. Nikishampata nitaanza mchakato wa kumtafuta Daktari wangu (Familly doctor).
sasa si kheri ungemuuliza jamaa yako ili akupe contacts za huyo mwanasheria ambaye ameonekana ni mzuri !!...
 
Back
Top Bottom