Fifty fifty. Tangazo lako ni jema...ila kufikiri kwako juu ya dhana ya ubaguzi..ndio hafifu. Ni mtizamo wangu.
Mimi mwanaume, napenda kwa kuwa sijakuona, basi utambulisho wako uzingatie tabia, sifa na uwezo wako ukilinganisha na tabia, sifa na uwezo wa mume umtakaye.
Ukisema age yangu ni 29, elimu yangu ni diploma, urefu wangu ni cm 55 au cm 65 au cm 70, rangi yangu ni maji ya kunde/ black beauty/ natural white au artificial white, mwembamba/mnene, mwenyeji wa kaskazini au kusini, niliwahi kuolewa na kuachika, nimezaa ninae mtoto mmoja, au mimi ni single lady pure, nipo Dar/ Tunduru/ Moshi n.k
Ni mwajiriwa/ mjasiriamali, naisha kwa wazazi wangu/ walezi/ najitegemea. Side B" Nahitaji mume mkristo age 31--39, awe mwenyeji wa Sengerema, awe na shughuli halali impayo kipato, awe mrefu cm kati ya 31--100, awe na uzito kg's 50--130, chagua na rangi uitakayo....Na bila shaka ungependa awe anaishi na kufanya kazi mkoa uliopo wewe.
Nadhani ukiainisha hivi atakaye ku-PM, atakuwa interested. Na atahitaji tu kukuona na kujiridhisha juu ya maswali alonayo moyoni mwake. Wewe umetangaza, atakayejitokeza atakuja kuku-interview, akiridhika atakuuliza kama uko tayari kuambatana naye, ukikubali...utapokea maelekezo na muongozo kutoka kwake.
Usiporidhika atakuacha uendelee kusailiwa na wengine ilhali ukiendelea kuchagua kadri watakavojitokeza. Chagua nikuchague...
Nakutakia kila la kheri.